Na Nathaniel Limu, Singida
JUMLA
ya watoto 284 hadi 300, huzaliwa kila mwaka katika hospitali ya mkoa
iliyopo mjini Singida wakiwa hawajatimiza umri wa kawaida wa kuzaliwa
(njiti).
Kati ya watoto hao,inakadiriwa 60 hadi 83 hufariki kutokana na sababu mbalimbali kila mwaka ikiwemo ya tatizo la kupumua.
Hayo
yamesemwa na kaimu mganga mfawidhi hospitali ya rufaa ya mkoa wa
Singida,Dk.Daniel Tarimo,wakati akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano
ya msaada wa vifaa tiba vitakavyotumika kwenye wodi ya watoto njiti
katika hospitali ya mkoa mjini hapa.
Kuhusu
watoto hao njiti wanaofariki dunia,Dk.Tarimo alisema vifo vingi
vinachangiwa na baadhi ya akina mama wajawazito kujifungulia nyumbani
mahali hakuna wataalamu wa huduma ya afya.
“Watoto
wa aina hii kwa kawaida wanakuwa na matatizo ya kupumua.Sasa mama
akijifungulia nyumbani,wakiwa njiani kukimbiza watoto/mtoto wa aina hiyo
hospitalini,mtoto/watoto husika hupata tatizo la kupumua linalopelekea
vifo vyao”,alifafanua zaidi Dk.Tarimo.
Kaimu
mganga huyo,alitumia fursa hiyo kuwakumbusha akina mama wajawazito
kujenga utamaduni wa kuanza mapema kuhudhuria kliniki ili endapo
watagundulika wana tatizo,waweze kuhudumiwa mapema kabla tatizo husika
halijaleta madhara makubwa.
Aidha,
Kaimu Mganga Huyo Mfawidhi,amemshukuru Miss Singida 2014 Dorice Mollel
kwa kutoa msaada huo wa vifaa tiba kwa ajili ya wodi ya watoto
njiti.Amewataka wadau wengine kuiga kitendo hicho.
Kwa
upande wake Miss Singida 2014, Dorice Mollel alisema amechukua hatua
hiyo ya kusaidia watoto njiti kwa madai kuwa na yeye alizaliwa akiwa
njiti pacha na kwa vyo vyote kuna watu walijitolea kuwasaidia katika
kipindi hicho.
Aidha,alisema
hatua hiyo ni kuiunga mkono serikali katika kupunguza vifo vya watoto
wachanga nchini.Ametaka wadau wengine kusaidia kundi hilo la watoto ili
kuwapunguzia matatizo mbalimbali yanayowakabili wakati wa ukuwaji waoa.
Kwa
mujibu wa Miss Singida 2014, Mollel baadhi ya vifaa hivyo ni suction
mashine-manual na electronic na mizani vyote vina thamani ya zaidi ya
shilingi 1.2 milioni.Mollel pia ni Miss kanda ya kati na alikuwa mshindi
wa tatu katika shindano la kusaka Miss Tanzania la mwaka jana.
No comments:
Post a Comment