TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, January 26, 2015

KAMATI YA BUNGE NA HUDUMA ZA JAMII YATEMBELEA TAASISI YA TIBA YA MIFUPA , UPASUAJI WA UBONGO NA MISHIPA YA FAHAMU (MOI)

Picha ya pamoja Waziri wa Afya Seif Rashid (wa sita kulia) na wakiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya Huduma ya Bunge ,Kuduma ya Jamii Gregory Teu (wa nne kulia) na  Kaimu  Mkurugenzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI)  Dk,  Othman  Kiloloma (wa tatu kushoto) na wengine ni wajumbe wa kamati hiyo ya  wabunge.
Kaimu  Mkurugenzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI)  Dk,  Othman  Kiloloma (wa pili kulia) akiwa katika kikao hicho na kamati hiyo baada ya kutembelea Taasisi ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) na kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa majumuisho.
Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya Huduma ya Bunge ,Kuduma ya Jamii Gregory Teu (katika)  akifafanua jambo wakati wa kamati yiho ilipotembelea Taasisi ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI)  na kwenda kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)   na kufanya majumuisho katika  Hospitali hiyo ( kushoto)  ni Waziri wa Afya Seif Rashid
Mbunge wa Viti Maalum Rukwa  Abia Nyabakari (kushoto)  akisalimiana na Waziri wa Afya Seif Rashid, baada ya kutembelea Taasisi ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI)   , katikati anaye shuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo  Dk,  Othman  Kiloloma
Kamati ya Kuduma ya Bunge, Huduma za Jamii ilipo Tembelea Taasisi ya
Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) na
kutembelea Vyumba vya Wagogonjwa Mahututi (ICU) katika Taasisi hiyo.
Kamati ya Kuduma ya Bunge, Huduma za Jamii ilipo Tembelea Taasisi ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) na  kutembelea Vyumba vya Upasuaji katika Taasisi hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo  Dk,  Othman  Kiloloma (kulia) akionyesha mashine zilizo mbovu kwa Kamati ya Kudumu ya ya Bunge ,Huduma za Jamii. 
Kamati ya Kuduma ya Bunge, Huduma za Jamii ilipo Tembelea Taasisi ya
Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) na
kutembelea Vyumba vya Upasuaji katika Taasisi hiyo.
Mkurugenzi wa Blog ya UJIJIRAHAA Khamis Mussa (kulia) katika Picha ya pamoja na baadhi ya  Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge , Huduma za Jamii  (kushoto) ni Dk. Hamisi Shaban (kushoto).
Kaimu  Mkurugenzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI)  Dk,  Othman  Kiloloma (katikati), akimuonyesha Waziri wa Afya Seif Rashid, picha ya X-ray ya mgonjwa aliyekuwa akifanyiwa Upasuaji wa  mguu wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge , Huduma za Jamii  ilipotembelea Taasisi hiyo

KINANA APOKELEWA KWA MCHAKAMCHAKA WA NGUVU JIMBO LA DONGE


1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa nne kutoka kushoto  akipokelewa kwa mchakamchaka na Mbunge wa jimbo la Donge na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu  Sadifa Juma Khamis wa tatu kutoka kushoto pamoja na vijana wa jimbo hilo ambao walikimbia naye umbali wa kilomita moja wakiwa katika mapokezi hayo yaliyotia fora mara baada ya kuanza ziara yake katika jimbo hilo  mwishoni mwa juma akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana yuko katika ziara ya visiwa vya Unguja na Pemba Zanzibar akihimiza uhai wa Chama cha Mapinduzi na kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.2Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiwa sambamba na Nape Nnauye katika mchakamchaka wakati wa mapokezi hayo katika jimbo la Donge Kaskazini Unguja.

Mtwara yapiga hatua upatikanaji wa maji safi na salama

 1Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendegu akiwakaribisha wajumbe wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji iliyowasili mkoani humo kukagua miradi ya maji.(Picha zote na Hussein Makame, MAELEZO)
2Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi akieleza lengo la ziara ya kamati hiyo mkoani Mtwara. 4Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara John Msengi akiwasilisha taarifa ya mradi wa maji wa Nanyamba kwa wajumbe wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji iliyotembelea kukagua mradi huo.
5Mwenyekiti wa kijiji cha Kibaoni kinachohudumiwa na Mradi wa Maji wa Nanyamba, Issa Bakari    akieleza jambo kwa wajumbe wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji iliyotembelea kukagua mradi huo.
6Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi akipanda ngazi za tanki la maji la mradi wa Maji wa Nanyamba.
7Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi akivuka kidaraja kuelekea kukagua tanki lingine la maji la mradi wa Maji wa Nanyamba.
9Afisa Mtendaji wa Mamlaka ya Mji wa Nanyamba, akitoa ufafanuzi kuhusu kisima cha mradi wa Maji wa Nanyamba.
10Msafara wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ukiwasili kwenye ofisi za wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara kukagua mradi wa Maji wa Matogoro. 12Mhandisi wa Maji Peter Malekia (katikati) akieleza jambo kwa Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi na wataalamu wa Wizara ya Maji wakiwa chini ya tanki la maji la Mradi wa Maji wa Matogoro linaloweza kuhifadhi maji lita 100,000.
14Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi akimpongeza mwenyekiti wa Kamati ya Maji ya Mradi wa Maji wa Matogoro Mzee Mwanya Natanga Bwanaheri.

Sunday, January 25, 2015

OBI KUWEKEZA KWENYE SOKO LA SMARTPHONE ZENYE GHARAMA NAFUU TANZANIA

DSC_0248Mkurugenzi Mtendaji wa Obi Mobiles, Afrika Mashariki na Kati na Afrika, Amit Rupchandani (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari )hawapo pichani) jijini Dar leo wakati wa utambulisho wa simu za aina ya smartphone zinazotengenezwa na Obi. Kushoto ni Mkurugenzi wa DESPEC Afrika, Farouk Jivani ambao ndio wasambazaji wakuu wa bidhaa hizo Tanzania na Afrika Mashariki na Kulia Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano wa Obi, Yusuf Khan.(Picha na Zainul Mzige).
………………………………………………………………………….
Kampuni mpya ya simu za Smartphone ya Obi Mobiles imezindua bidhaa zake katika soko la Tanzania pamoja na Nchi za Afrika Mashariki, kwa ubia na kampuni ya DESPEC wasambazaji wanaoongoza katika soko la usambazaji wa bidhaa za IT.
Wakizungumza na wandishi wa habari leo katika Hotel ya Serena, jijini Dar es Salaam, wakati wa utambulisho rasmi wa kampuni hiyo ya simu ya Obi iliyoanzishwa na mtaalam wa masoko na Mkurugenzi wa zamani wa kampuni ya Apple, John Sculley, Akizumgumza kwa niaba ya Sculley. Mkurugenzi Mtendaji wa Obi Mobiles, Afrika Mashariki na Kati na Afrika, Amit Rupchandani
Alisema kampuni hiyo kwa kushirikiana na DESPEC, Obi inategemea kuanza kusambaza bidhaa zake zenye ubora zaidi katika robo ya kwanza ya mwaka huku ikitarajia kuweza kukamata soko la Tanzania kwa asilimia tano (5%) ifikapo mwisho mwa mwaka huu.
DSC_0235Mkurugenzi wa DESPEC Afrika, Farouk Jivani (kushoto) ambao ndio wasambazaji wakuu wa bidhaa hizo Tanzania na Afrika Mashariki, akitolea ufafanuzi wa kituo cha huduma (services centre) ya simu hizo za Obi zitakazokuwa zikishughulikiwa hapa hapa nchini.
“Nia yetu ni kutumia Obi kwenye kila soko jipya ili kutengeneza bidhaa inayokubalika Kimataifa na hasa kwenye sehemu ambazo matumizi ya Smartphone yapo juu” alisema Amit Rupchandani.
Aliongeza kuwa, Katika uzinduzi uliofanyika India na Mashariki ya Kati, umeweza kuleta mafanikio makubwa kuliko walivyotegemea hivyo Obi imejiandaa na kuwekeza nguvu kupanua wigo wa biashara zake pia kwa soko la Tanzania.
Aidha, akielezea namna walivyojiandaa kushika soko la Afrika, Amit Rupchandani alisema soko la Afrika lina nafasi kubwa kwenye bidhaa za smartphone kutokana na ongezeko kubwa katika matumizi ya Teknologia na hasa miongoni mwa vijana.
DSC_0307Mkurugenzi wa DESPEC Afrika, Farouk Jivani (kushoto) ambao ndio wasambazaji wakuu wa bidhaa hizo Tanzania na Afrika Mashariki, akionyesha aina moja ya simu za Obi ambazo zitakuwa na garantii ya mwaka mmoja na miezi minne.
“Wateja wanataka kutumia Smartphone zilizo nzuri zenye bei nafuu bila kuathiri ubora wake. Pia kuna ongezeko la matumizi ya Iphone ukilinganisha na Smartphone. Utafiti wetu umeonesha ya kwamba wateja wanaweza kubadilisha matumizi ya bidhaa yeyote ilmradi wana imani nayo, hivyo Obi imejiandaa kukabiliana na hilo na hakika watazifurahia”. Alisema
Aidha, Amit Rupchandani alibainisha kuwa, licha ya soko la bidhaa za simu za mkononi kuwa bidhaa za bei kubwa, wao hawatakuwa hivyo kwani lengo lao ni kuongeza watumiaji wa simu za mkononi ambao wangependa kutumia smartphone zenye ubora bila kuingia gharama kubwa.
“Falsafa yetu ya ‘Kama ulivyo’ inamaanisha Obi haibagui, inakuwezesha ulivyo ambapo tuna bidhaa mbalimbali kwa watu wa aina tofauti”. alimalizia Amit Rupchandani.
DSC_0313Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano wa Obi, Yusuf Khan (kulia) akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) application mbalimbali zinazopatikana kwenye simu hizo.
Kwa upande wake, Mkurugezi wa DESPEC Afrika, Farouk Jivani alisema kampuni yake inayo furaha kuwa msambazaji wa kipekee wa bidhaa za Obi Mobiles Tanzania na Afrika Mashariki kwani wamejidhatiti kuhakikisha zinawafikia watumiaji sokoni.
“Kuingia kwa kwa bidhaa za Obi Mobiles sokoni kunaashiria ongezeko la matumizi ya simu za mkononi na pia matumizi ya intaneti, hivyo tunafanya juhudi kuhakikisha Obi inatengeneza jina la kudumu kwa bidhaa zake katika hili” alisema Farouk Jivani.
Obi Smartphone kwa soko la Afrika, inatarajiwa kuziduliwa mwezi Machi mwaka huu hapa Nchini ikifuatiwa na Nchi zingine za Afrika.
DSC_0318Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakikagua ubora wa simu za Obi.
DSC_0323Kipeperushi kikionyesha aina mbalimbali za simu za smartphone za kampuni ya Obi zitakazokuwa zikiuzwa kuanzia shilingi 120,000 mpaka 340,000.

KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHAZUNGUMZIA CHANGAMOTO ZA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA KURA YA MAONI YA KATIBA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Hellen Kijo-Bisimba (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam mwishoni mwa juma , wakati akitoa taarifa kuhusu changamoto za utekelezaji wa sheria ya kura ya maoni ya Katiba. Kulia ni Mratibu wa Katiba wa LHRC, Anna Henga na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Ezekiel Massanja.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo
 Wapiga picha na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
…………………………………………………………………………………………………………. Dotto Mwaibale
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesema kina wasiwasi na mchakato wa kura ya maoni inayotarajiwa kufanyika kwa sabau ya muda mdogo ulibaki ikizingatiwa daftari la wapigakura halijafanyiwa marekebisho pia watanzania wengi hawana uelewa na katiba iliyopendekezwa.
Kituo kimetoa mapendokezo kwa Serikali kuahirisha tarehe ya kupiga kura ya maoni kwa kile kilichodaiwa katiba inayopendekezwa inamapungufu na yasiporekebishwa muda huu yanaweza kuathiri kura ya maoni na kuwakosesha watanzania wengi kushiriki haki yao kikatiba.
Akizungumza Dar es Salaam mwishoni  wa juma , Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, DK. Hellen Kijo- Bisimba alisema kituo hicho kimekuwa na utaratibu wa kufuatilia mchakato wa katiba, kubaini mapugufu mengi likiwemo la muda mdogo na wananchi wengi kutoelewa vizuri katiba inayopendekezwa.
“Mchakato wa kura ya maoni unaenda kukamilika Februari 28 kwa mjibu wa sheria ya kura hiyo.Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapaswa kuboresha daftari la wapiga kura ndipo kura ipigwe, ukizingatia zimebaki siku takribani 25 kufikiaki hitimisho,sisi tunaona kuna changamoto ya muda na ni vyema zoezi hilo lisongezwe mbele,”alisema.
 Aliongeza kuwa vifaa vya BRV vinavyotarajiwa kutumika kwa mara ya kwanza na tume ya uchaguzi vimeonesha changamoto katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na hivyo kituo hicho kinawasiwasi na mchakato mzima wa upatikaji wa katiba iliyo bora.
“Kifungu cha 10 katika katiba inayopendekezwa kimezungumzia vituo vya kupigia kura, kwamba vitapangwa kulingana na maeneo yaliyo na watu wengi katika maeneo husika wasiwasi wangu hapa tume inaweza kutotumia majimbo ya zamani na kutengeza majimbo mpya,”alisema.
Bisimba alisema changamoto nyingine katika mchakatio huo ni Usajili wa kamati za kura ya maoni katika kuikubali au kuikataa kura hiyo katiba inaelekeza kamati ni lazima ipeleke maombi kabla ya siku 21 kupigwa kwa kura ya maoni.
“Utaratibu ambao sisi kulingana na uzoefu wetu wa kufanya kazi tunaona haya ni masharti magumu yanayoekekezwa kwenye kamati za kura, kwani inawataka pia kueleza vyanzo vya mapato yao kitu ambacho kinaweza kusababisha  kamati zingine kutopata usajili,”alisema.
Dk.Bisimba aliongeza kuwa changamoto ambayo kituo kinaona kuwa ni kiini macho ni pale inapoelezwa kwamba wanzazibar waishio Tanzania bara wakipiga kura kura zao zitahesambiwa upande wa zanzibar. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

Watendaji wa Shirika la Nyumba Wafanya ziara ya maeneo ya Matevez na USA River kutakakoanza kujengwa miji miwili ya kisasa


Baadhi ya watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa, waliokuwa katika kongamano la wiki nzima la Mameneja wa Mikoa na Watendaji wengine lililokuwa likifanyika katika hoteli ya Naura Springs, Arusha wakiwa katika eneo la NHC Burka/Matevez kutakakoanza kujengwa mji mpya wa kisasa‘satelite city’ wa Safari City jijini Arusha. Eneo hilo la ukubwa wa takriban ekari 500 ambapo zitajengwa nyumba zaidi ya 7000 utakuwa na mahitaji yote muhimu kama maduka makubwa, makazi ya watu, huduma za afya, shule, na ofisi.

 Baadhi ya watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa, waliokuwa katika kongamano la wiki nzima la Mameneja wa Mikoa na Watendaji wengine lililokuwa likifanyika katika hoteli ya Naura Springs, Arusha wakiwa katika eneo la NHC Burka/Matevez kutakakoanza kujengwa mji mpya wa kisasa wa Safari City jijini Arusha.

 Eneo la NHC Burka/Matevez kutakakoanza kujengwa mji mpya wa kisasa wa Safari City jijini Arusha.

  Eneo la NHC Burka/Matevez kutakakoanza kujengwa mji mpya wa kisasa wa Safari City jijini Arusha.

  Eneo la NHC Burka/Matevez kutakakoanza kujengwa mji mpya wa kisasa wa Safari City jijini Arusha.

 Baadhi ya watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa, waliokuwa katika kongamano la wiki nzima la Mameneja wa Mikoa na Watendaji wengine lililokuwa likifanyika katika hoteli ya Naura Springs, Arusha wakiwa katika eneo la NHC USA RIVER kutakakoanza kujengwa mji mpya wa kisasa wa USA River jijini Arusha.

  Baadhi ya watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa, waliokuwa katika kongamano la wiki nzima la Mameneja wa Mikoa na Watendaji wengine lililokuwa likifanyika katika hoteli ya Naura Springs, Arusha wakiwa katika eneo la NHC USA RIVER kutakakoanza kujengwa mji mpya wa kisasa wa USA River jijini Arusha.

  Baadhi ya watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa, waliokuwa katika kongamano la wiki nzima la Mameneja wa Mikoa na Watendaji wengine lililokuwa likifanyika katika hoteli ya Naura Springs, Arusha wakiwa katika eneo la NHC USA RIVER kutakakoanza kujengwa mji mpya wa kisasa wa USA River jijini Arusha.

  Baadhi ya watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa, waliokuwa katika kongamano la wiki nzima la Mameneja wa Mikoa na Watendaji wengine lililokuwa likifanyika katika hoteli ya Naura Springs, Arusha wakiwa katika eneo la NHC USA RIVER kutakakoanza kujengwa mji mpya wa kisasa wa USA River jijini Arusha.

Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara David Shambwe na Meneja wa Uendelezaji Biashara, William Genya wakiwa katika eneo la NHC USA RIVER kutakakoanza kujengwa mji mpya wa kisasa wa USA River jijini Arusha.

  Baadhi ya watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa, waliokuwa katika kongamano la wiki nzima la Mameneja wa Mikoa na Watendaji wengine lililokuwa likifanyika katika hoteli ya Naura Springs, Arusha wakiwa katika eneo la NHC USA RIVER kutakakoanza kujengwa mji mpya wa kisasa wa USA River jijini Arusha.

Eneo la NHC USA RIVER kutakakoanza kujengwa mji mpya wa kisasa wa USA River jijini Arusha.

SEKTA YA UMMA YAOMBWA KUIMALISHA UBUNIFU KWENYE SAYANSI HAI

 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Hassan Mshinda (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi, kwenye  semina ya siku mbili iliyohusu matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika kuinua uchumi kupitia viwanda na uhifadhi wa mazingira na Sekta ya Umma kuimarisha ubunifu kwenye Sayansi hai.
 Mkurugenzi wa Sera na Utafiti Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), akichangia mada katika semina hiyo iliyoandaliwa na  Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech). Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dk.Hassan Mshinda.
 Profesa Tiisekwa Bendantungula kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), akichangia mada.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Banana Envestment ya Arusha, Adolf Olomi, akizungumza na waandishi wa habari. Kampuni hiyo imefanikiwa kutumia maji taka yanayotoka katika kiwanda hicho na kuyatumia kwa matumizi mengine kupitia utafiti uliofanywa na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye semina hiyo.
 Wanahabari wakiwa kwenye semina hiyo
Semina ikiendelea.
…………………………………………………………………………..
Dotto Mwaibale
UKUAJI wa Sekta ya Sayansi na Teknolojia umekuwa na mafanikio makubwa pamoja na msaada katika kuharakisha na kuboresha na urahisishaji wa kuleta maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Hayo yal

Ujenzi Chuo cha Tiba Mloganzila kugharimu zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 61.

indexNa Anitha Jonas – MAELEZO.
  Dar es salaam.
SERIKALI Mwishoni mwa juma ilisema kuwa mradi wa ujenzi wa  Chuo cha Tiba  cha Kimataifa cha Muhimbili  eneo la Mloganzila nje kidogo ya jiji la Dar es salaam utagharimu kiasi cha Dola za kimarekani Milioni 61. Katika mradi huo serikali ya
Tanzania imechangia dola za kimarekani milioni 18 na serikali ya Jamhuri  ya Korea imetoa mkopo wa dola za kimarekani milioni 43 ili kufanikisha ujenzi wa chuo hicho katika eneo la Mlonganzila jijini Dar es Salaam.
Akizungumza  mara baada ya kukamilisha  ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho jana jijini Dar es salaam Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi  Dkt.Shukuru Kawambwa  alisema kuwa mradi huo na  unatarajiwa kukamilika mwezi  Machi mwakani.
“Tumejipanga vizuri  kujenga  Chuo hiki cha Tiba ambacho kitakua mji wa tiba hapa nchini, sisi kama serikali tumeiona changamoto ya wataalam wa afya nchini na kuona ni vyema kujenga chuo cha kisasa kitakachokua na uwezo wa kupokea  zaidi ya wanafunzi 15,000  kwa mwaka watakaosaidia kuondoa tatizo la wataalamu wa afya.” alisema Dkt.Kawambwa.
 Dkt. Kawambwa alisema kuwa mbali na ujenzi wa chuo hicho, serikali itajenga hospitali nyingine ya Muhimbili ambayo ujenzi wake utamalizika sambamba na ujenzi wa chuo hicho ili kuwawezeha wananchi kupata huduma bora za afya.
Alibainisha kuwa  hospitali hiyo pindi itakapokamilika itakuwa kubwa zaidi  na yenye vifaa vya kisasa  itakayosaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa uliopo katika hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na kuwasaidia wanafunzi kupata sehemu ya mafunzo kwa vitendo.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha Tiba Muhimbili Prof. Ephata  Kaaya  alisema mradi huo umegawanyika katika awamu mbili, awamu ya kwanza ikihusisha  ujenzi wa chuo cha tiba na Hospitali ya kisasa ya muhimbili na awamu ya pili  itakuwa ujenzi wa hospitali  kubwa ya kutibu magonjwa ya Moyo na mishipa ya fahamu.
“ Tayari Benki ya Maendeleo  Afrika imetoa  kiasi cha zaidi ya dola za kimarekani milioni 9 kwa ajili ya ujenzi  wa Chuo  na hospitali ya kimataifa ya magonjwa ya moyo na mishipa ya fahamu itakayokuwa na ubora wa hali ya juu katika nchi za Afrika Mashariki” alisisitiza Prof.Kaaya .
 Aliongeza kuwa gharama ya vifaa tiba ikiwemo vya uchunguzi na upasuaji utagharimu zaidi ya dola za kimarekani Milioni 27 na kueleza kuwa mkandarasi wa kufunga vifaa tiba vya mradi huo ameshapatikana  na anatarajia kuanza kufanya kazi hiyo hivi karibuni.

Nikiri kuwa ni makosa kutafsiri Filamu bila idhini ya mmiliki –Mzee Lufufu

PIX2 Katibu Bodi ya Filamu Tanzania Bi,Joyce Fissoo(kushoto) akifafanua jambo wakati  wa kikao kilichofanyika leo kuhusu suala zima la bei za filamu,kulia ni Kaimu mkurugenzi wa idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bi.Lilly Beleku.
………………………………………………………………………
Na Frank Shija.WHVUM Mkurugenzi wa Kampuni ya Mukandala Lufufu inayojishughulisha na kazi ya kutafsiri Filamu kwa Lugha ya Kishwahili Bw. Derick Mukandala maarufu kwa jina la Mzee Lufufu amekiri kuwa kazi yake anaifanya kienyeji ili hali akifahamu ni makosa. Kauli hiyo ameitoa jana katika kikao baina yake na Bodi ya Filamu ambapo alieleza kuwa amekuwa akifanya kazi hiyo kwa muda mrefu bila kuzingatia utaratibu huku akijua kuwa ni makosa kwa mtu kutumia kazi ya msanii mwingine bili idhini yake. “Nikiri tu kwamba nimekuwa nikifanya makosa kwa kutafsiri Filamu bila kuwa na idhini ya wahusika wa filamu hizo” Alisema Lufufu. Mzee Lufufu aliongeza kuwa amekuwa akifanya kazi hiyo ya kutafsiri Filamu bila vibali akiamini kuwa hakuna ubatili wowote. Aidha Mzee Lufufu pamoja na kujua ni makosa kutafsiri Filamu bila idhini alikuwa anatarajia kufanya kazi na Kampuni moja ya kutoka nchini Norway ambapo kama amngefanikiwa kufanya Documentary ambayo ingejulikana kwa jina la “The Film Dubber from Dar es Salaam – Mzee Lufufu” hiyo ingeaminisha ulimwengu kuwa Tanzania inaruhusu uharamia wa kazi za wasanii kitu ambacho siyo sahihi. Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa siyo dhambi kutafsiri Filamu, ila ni lazima anayetaka kufanya kazi hiyo azingatie dheria za nchi na taratibu zinaotakiwa kuzingatiwa. Fissoo amesema kuwa sheria ya Filamu nchini kifungu namba 17 kinamtaka anayetaka kufanya kazi ya kutafsiri awasilishe muswada wake katika ofisi za Bodi ya Filamu ili uhakikiwa na wataalamu kabla ya kupewa idhini ya kuendelea na kazi hiyo. Aliongeza kuwa ili kazi ya kutafsiri Filamu ni sharti mhusika kupata idhini ya mwenye Haki Miliki ya filamu husika hivyo ni vyema kuwasiliana na COSOTA ili kufanya utaratibu wa kupata uhalali akitolea mfano wa Filamu ya Nelia iliyotengenezwa nchini Zimbabwe na baadaye ilifanyiwa tafsiri katika lugha ya Kiswahili hapa jijini Dar es Salaam baada ya kufuata taratibu zote.