Mkurugenzi
Mtendaji wa Obi Mobiles, Afrika Mashariki na Kati na Afrika, Amit
Rupchandani (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
)hawapo pichani) jijini Dar leo wakati wa utambulisho wa simu za aina
ya smartphone zinazotengenezwa na Obi. Kushoto ni Mkurugenzi wa DESPEC
Afrika, Farouk Jivani ambao ndio wasambazaji wakuu wa bidhaa hizo
Tanzania na Afrika Mashariki na Kulia Mkuu wa kitengo cha masoko na
mawasiliano wa Obi, Yusuf Khan.(Picha na Zainul Mzige).
………………………………………………………………………….
Kampuni
mpya ya simu za Smartphone ya Obi Mobiles imezindua bidhaa zake katika
soko la Tanzania pamoja na Nchi za Afrika Mashariki, kwa ubia na kampuni
ya DESPEC wasambazaji wanaoongoza katika soko la usambazaji wa bidhaa
za IT.
Wakizungumza
na wandishi wa habari leo katika Hotel ya Serena, jijini Dar es Salaam,
wakati wa utambulisho rasmi wa kampuni hiyo ya simu ya Obi
iliyoanzishwa na mtaalam wa masoko na Mkurugenzi wa zamani wa kampuni ya
Apple, John Sculley, Akizumgumza kwa niaba ya Sculley. Mkurugenzi
Mtendaji wa Obi Mobiles, Afrika Mashariki na Kati na Afrika, Amit
Rupchandani
Alisema kampuni hiyo kwa kushirikiana na DESPEC, Obi inategemea kuanza
kusambaza bidhaa zake zenye ubora zaidi katika robo ya kwanza ya mwaka
huku ikitarajia kuweza kukamata soko la Tanzania kwa asilimia tano (5%)
ifikapo mwisho mwa mwaka huu.
Mkurugenzi
wa DESPEC Afrika, Farouk Jivani (kushoto) ambao ndio wasambazaji wakuu
wa bidhaa hizo Tanzania na Afrika Mashariki, akitolea ufafanuzi wa kituo
cha huduma (services centre) ya simu hizo za Obi zitakazokuwa
zikishughulikiwa hapa hapa nchini.
“Nia
yetu ni kutumia Obi kwenye kila soko jipya ili kutengeneza bidhaa
inayokubalika Kimataifa na hasa kwenye sehemu ambazo matumizi ya
Smartphone yapo juu” alisema Amit Rupchandani.
Aliongeza
kuwa, Katika uzinduzi uliofanyika India na Mashariki ya Kati, umeweza
kuleta mafanikio makubwa kuliko walivyotegemea hivyo Obi imejiandaa na
kuwekeza nguvu kupanua wigo wa biashara zake pia kwa soko la Tanzania.
Aidha,
akielezea namna walivyojiandaa kushika soko la Afrika, Amit Rupchandani
alisema soko la Afrika lina nafasi kubwa kwenye bidhaa za smartphone
kutokana na ongezeko kubwa katika matumizi ya Teknologia na hasa
miongoni mwa vijana.
Mkurugenzi
wa DESPEC Afrika, Farouk Jivani (kushoto) ambao ndio wasambazaji wakuu
wa bidhaa hizo Tanzania na Afrika Mashariki, akionyesha aina moja ya
simu za Obi ambazo zitakuwa na garantii ya mwaka mmoja na miezi minne.
“Wateja
wanataka kutumia Smartphone zilizo nzuri zenye bei nafuu bila kuathiri
ubora wake. Pia kuna ongezeko la matumizi ya Iphone ukilinganisha na
Smartphone. Utafiti wetu umeonesha ya kwamba wateja wanaweza kubadilisha
matumizi ya bidhaa yeyote ilmradi wana imani nayo, hivyo Obi imejiandaa
kukabiliana na hilo na hakika watazifurahia”. Alisema
Aidha,
Amit Rupchandani alibainisha kuwa, licha ya soko la bidhaa za simu za
mkononi kuwa bidhaa za bei kubwa, wao hawatakuwa hivyo kwani lengo lao
ni kuongeza watumiaji wa simu za mkononi ambao wangependa kutumia
smartphone zenye ubora bila kuingia gharama kubwa.
“Falsafa
yetu ya ‘Kama ulivyo’ inamaanisha Obi haibagui, inakuwezesha ulivyo
ambapo tuna bidhaa mbalimbali kwa watu wa aina tofauti”. alimalizia Amit
Rupchandani.
Mkuu
wa kitengo cha masoko na mawasiliano wa Obi, Yusuf Khan (kulia)
akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) application
mbalimbali zinazopatikana kwenye simu hizo.
Kwa
upande wake, Mkurugezi wa DESPEC Afrika, Farouk Jivani alisema kampuni
yake inayo furaha kuwa msambazaji wa kipekee wa bidhaa za Obi Mobiles
Tanzania na Afrika Mashariki kwani wamejidhatiti kuhakikisha zinawafikia
watumiaji sokoni.
“Kuingia
kwa kwa bidhaa za Obi Mobiles sokoni kunaashiria ongezeko la matumizi
ya simu za mkononi na pia matumizi ya intaneti, hivyo tunafanya juhudi
kuhakikisha Obi inatengeneza jina la kudumu kwa bidhaa zake katika hili”
alisema Farouk Jivani.
Obi
Smartphone kwa soko la Afrika, inatarajiwa kuziduliwa mwezi Machi mwaka
huu hapa Nchini ikifuatiwa na Nchi zingine za Afrika.
No comments:
Post a Comment