Wanafunzi
wa shule ya sekondari Nanja wakionyesha vitabu vyao mara baada ya
Airtel kukabithi msaada wa vitabu vya sayansi kwa shule hiyo chini ya
mpango wake wa Airtel shule yetu.
Wanafunzi
na walimu wa shule ya Sekondari Nanja wamepokea msaada wa vitabu kutoka
Airtel, Msaada utakaoweza kuchangia katika kutatua tatizo la uhaba wa
vitabu shule ni hapo.
Akitoa
taarifa ya shule , Mkuu wa shule ya sekondari ya Nanja Bwana Yona luka
alisema” shule yetu ina jumla ya wanafunzi 549 na walimu 32, matokeo ya
shule ya kidato cha nne yanakuwa kila mwaka ufaulu wa asilimia 71%
pamoja na kukua kwa kiwango cha ufaulu bado shule inachangamoto nyingi
ikiwemo uhaba wa vitabu na walimu.
Meneja
Mauzo wa Airtel Kanda ya Kaskazini Brighthon Majwala akikabithi vitabu
kwa Afisa Elimu wa shule za sekondari halimashauri ya Monduli Bwana
Shaban Kasim Mgunya kwaajili ya shule ya sekondari Nanja iliyoko Monduli
mkoani Arusha. wakishuhudia ni baadhi ya wanafunzi wa shule ya
sekondari Nanja.
Meneja
Mauzo wa Airtel Kanda ya Kaskazini Brighthon Majwala akikabithi vitabu
kwa Afisa Elimu wa shule za sekondari halimashauri ya Monduli Bwana
Shaban Kasim Mgunya kwaajili ya shule ya sekondari Nanja iliyoko Monduli
mkoani Arusha wakishuhudia kulia ni Afisa uhusiano wa Airtel Jane
Matinde na kushoto ni mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Nanja Yona
Lukas.
Afisa
uhusiano wa Airtel Jane Matinde akipitia kitabu na baadhi ya wanafunzi
wa shule ya sekondari Nanja mara baada ya Airtel kukabithi msaada wa
vitabu vya sayansi kwa shule hiyo chini ya mpango wake wa Airtel shule
yetu.
Kwa
sasa uwiano wa vitabu vya sayansi ni kitabu 1 kwa wanafunzi 5 wakati
kwa vitabu vya sayansi ya jamii uwiano ni kitabu 1 wanafunzi 30.
Tunafurahi sana kupokea vitabu hivi toka Airtel kwani msaada huu umekuja
kwa wakati muafaka”.
Akiongea
wakati halfa hiyo fupi ya kukabithi vitabu , Afisa Elimu wa shule za
sekondari halimashauri ya Monduli Bwana Shaban Kasim Mgunya alisema”
napenda kuwashukuru sana Airtel kwa kufikisha msaada huu wa vitabu kwa
sekondari hii ya Naja , vitabu hivi vya sayansi havitachangia kuongeza
kiwango cha ufaulu tu bali vitawahamasisha wanafunzi wengi kujiunga na
masomo ya sayansi.
Natoa
wito kwa walimu kuwapatia wanafunzi vitabu hivi wavisoma ili kuwajengea
wanafunzi hawa tabia ya kusoma vitabu. Nawahasa wanafunzi kuvitunza
vitabu ili viweze kutumika na wanafunzi wengi zaidi shuleni hapa
Aliongeza kwa kusema” shule imeweza kujenga maktaba lakini
tunayochangamoto ya uhaba wa vifaa vya maktaba , nachukua fulsa hii
kuwaomba Airtel waendelee kutusaidia kwa kuchangia vifaa vya mahabara na
kuwezesha masomo ya sayansi ya vitendo”.
Akiongea
kwa niaba ya Airtel Meneja wa kanda ya kaskazini Brighton Majwala
alisema”wote tunatambua tatizo la uhaba wa vitabu katika shule za
sekondari ambapo hali halisi haiendani namahitaji, uwiano wa kitabu 1 ni
kwa wanafunzi 10. Kwa kuliona hilo Airtel tumejikita na kushirikiana na
serikali katika kuhakikisha tunatutua changamoto hii na kuongeza
kiwango cha ubora wa elimu nchini. Natoa wito kwa wanafunzi wa Nyala
kuzitumia vitabu hivi vizuri na kuboresha kiwango cha ufaulu.
Kwa
upande wa wanafunzi wameishukuru Airtel kwa kuboresha elimu na kusema
vitabu hivi vitawasaidia kuongeza ujuzi katika masomo ya sayansi na
kufanya vizuri zaidi.
Halfa
ya kukabithi vitabu katika shule ya sekondari Nanja ilimalizika kwa
zoezi la kupanda miti ambapo walimu, wanafunzi na Airtel walishiriki
katika kuboresha mazingira ya shule.
Airtel
chini ya mpango wake wa Airtel Shule yetu mpaka sasa imezifikia shule
zaidi ya 1300 nchini, shule nyingine katika kanda ya kaskazini
zitakazofaidika na vitabu hivi ni pamoja na Manyara, Moshi na Tanga na
shule nyingine katika maeneo mbalimbali ya nchi nazo zitaendelea kupata
msaada huu wa vitabu
No comments:
Post a Comment