Waziri wa Nishati na Madini Mhe.
George Simbachawene (kushoto) akipokea maua kutoka kwa mmoja wa
watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini Lilian Aroko mara baada ya
kuwasili kwenye ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini
(Nishati) Mhe. Charles Mwijage (Kulia) akimpokea Waziri wa Nishati na
Madini Mhe. George Simbachawene (kushoto) mara waziri huyo alipowasili
kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini.
Waziri wa Nishati na Madini
Mhe. George Simbachawene (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa
Idara ya Sheria, Salome Makange mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za
Makao Mkuu ya Wizara.
Waziri wa Nishati na Madini Mhe.
George Simbachawene (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari mara
baada ya kupokelewa na uongozi wa Wizara hiyo. Kulia ni Kaimu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava. Mhe.
Simbachawene amesisitiza umuhimu wa sekta za nishati na madini kama
mhimili mkuu wa ukuaji wa uchumi wa nchi na kuomba ushirikiano kutoka
kwa wadau mbalimbali wa sekta za nishati na madini
No comments:
Post a Comment