Mwanamuziki Profesa J akiimba katika uzinduzi huo.
Mwanamuziki Vanessa Mdee akiimba katika uzinduzi huo.
……………………………………………………………………………………..
Tigo Tanzania leo imetangaza rasmi
uzinduzi wa Muziki wa Tigo ujulikanao kama “Tigo Music” kwa
kushirikiana na Deezer, ambayo ni huduma ya kimataifa inayorusha muziki
itakayowapa Watanzania muziki usiokuwa na kikomo.
Kutakuwa na hafla ya uzinduzi kwa
ajili ya Tigo Music katika viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam Tarehe
24 Januari ambapo wananchi watatumbuizwa na nyimbo tofauti tofauti
kutoka kwa wasaniii 18 wa hapa nchini kama Diamond Platinum, Ali Kiba,
Professor J, Weusi, Msondo, Ben Paul, Shillole Linah, Christian Bella,
AY hao ni kati ya 18.
Kuanzia Januari 24, wateja wa Tigo
wenye vifurushi vya malipo ya kabla ya intaneti wana uwezo wa kupata
nyimbo milioni 36 za wasanii wa Kitanzania na Afrika kwa ujumla katika
simu zao za mkononi za smartphone. Vilevile, Tigo itatafuta miziki mipya
ya kusisimua ya wasanii wa ndani kupitia ushirikiano mpya na kampuni ya
Africa Music Rights, ambayo inawezesha, kutafuta na kusimamia haki za
muziki katika bara la Afrika,
Meneja Mkuu wa Tigo Bi, Cecile
Tiano alisema, ‘Tuna furaha kuwa kampuni ya kwanza ya mawasiliano
Tanzania kuwapa wateja wetu muziki usiokuwa na kikomo”. Muziki unajukumu
kubwa katika Tanzania yetu tajiri na tamaduni tofauti kama starehe
katika matukio ya kijamii na hata wakati binafsi. Haya ni mafanikio
makubwa kwetu tukitarajia watu zaidi na zaidi kutumia smartphones katika
sehemu hii ya dunia’.
“Kama bidhaa yenye maisha ya kidijitali, lengo letu ni
kuiwezesha tasnia ya muziki kwa kujenga jukwaa ambalo si tu linaruhusu
kupata nyimbo za wasanii wa ndani kwa urahisi, lakini pia linawapa
mafunzo wanamuziki wetu kwenye masuala muhimu kama vile haki miliki na
masoko. Hii ni njia yetu ya kusaidia vipaji vya wasanii na kukuza tasnia
ya muziki wa ndani, “aliongeza.
Kuanzishwa kwa Muziki wa Tigo
(Tigo Music) nchini Tanzania kumetokana na mafanikio ya uzinduzi nchini
Amerika ya Kusini mwaka 2012 pamoja na Ghana mwaka 2014, na. Tangu
kuanzishwa kwake imekuwa ni sehemu muhimu kwa maisha ya kidijitali ya
watu ya kila siku na hii inaendana na matukio ya muziki wa ana kwa ana
yaliyowahi kufanywa na wanamuziki mashuhuri duniani, pamoja na yale
yaliyorekodiwa ndani ya studio.
Kama bidhaa, Tigo music imeongezeka kwa kiasi kikubwa huko
Colombia kama nchi inayoongoza kwa huduma ya urushwaji wa muziki, wakiwa
na watumiaji 600,000 wakisikiliza kwa wastani nyimbo zaidi ya 400 na
masaa 40 ya muziki kila mwezi.
Urushwaji wa muziki ni eneo
linalokua kwa haraka sana katika tasnia ya muziki kimataifa, na bidhaa
ya muziki tayari imekuwa ya pili kimaarufu kwenye vipengele vya simu za
mkononi katika Afrika.
No comments:
Post a Comment