Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akikagua
viwanja vya NHC Wilayani Chato vinavyokusudiwa kujengwa nyumba za gharama nafuu
ikiwa ni program ya NHC ya kuzifikia Wilaya zote nchini.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu
ukikagua nyumba za makazi za NHC Wilayani Chato alipotembelea Wilaya hiyo jana.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akiongea
na kikundi cha vijana cha Mshikamano Wilayani Muleba alipokitembelea kuona
namna kinavtumia mashine zilizotolewa na NHC ili kuongeza ajira kwa vijana. Bw.
Mchechu amezitaka Halmashauri za Wilaya nchini kuunga mkono juhudi za NHC kwa
kuwapatia vijana maeneo ya kufanyia kazi zao.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu
ukiwa eneo la Mtukula linapojengwa jingo la kisasa la biashara na NHC ili
kuvutia na kuchochea ukuaji wa biashara katika eneo hilo la mpaka wa Tanzania
na Uganda. Eneo hili ndipo zilipokuwa nyumba ndogondogo zilizojengwa na NHC na
baadaye kuharibiwa na mabomu ya Nduli Iddi Amin alipovamia nchi yetu mwaka
1978. NHC iliiomba Halmashauri ya Wilaya
ya Misenyi kulirejeshea eneo hilo ili kujenga jengo hilo la kibiashara.
No comments:
Post a Comment