Tume imesikitishwa na matukio
yaliyotokea tarehe 27/01/2015 huko Mbagala Wilaya ya Temeke
Dar-es-Salaam, matukio ambayo yameoneshwa na Kituo cha Televisheni cha
“Channel Ten” ambayo yameashiria uvunjifu wa haki za binadamu.
Mnamo majira ya saa kumi na robo hadi kumi na nusu jioni, Kituo
cha TV cha “Channel Ten” kilirusha picha zilizoonesha kupigwa na Polisi
baadhi ya wananchi waliokamatwa kwa kile kilichoelezwa kushiriki mkutano
wa Chama cha Wananchi (CUF) uliosemekana kuwa si halali.
Tume tayari imeanza kuchunguza tukio hilo na taarifa kamili itatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.
Bahame T. M. Nyanduga
MWENYEKITI
No comments:
Post a Comment