2- Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiwaeleza jambo Maafisa
Mawasiliano Serikalini kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara. Katika
kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini Januari 26, 2015 Mjini
Mtwara
Picha zote na Hassan Silayo
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano
wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wa kikao kazi hicho Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara.
Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiwaeleza washiriki wa
Mkutano huo umuhimu wa kuelimisha umma kuelekea upigaji kura ya maoni na
kuwataka wahariri wa vyombo vya habari nchini kuwa mstari wa mbele
katika kutekeleza suala hili la kitaifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni
ya JL Communication inayochapisha magazeti ya Jambo leo na StaaSpoti
Bw. Theophil Makunga akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara pia aliwataka
Maafisa Mawasiliano kutengeneza mazingira yatayowezesha kufanya kazi na
wanahabari.
8- Mhadhiri wa Chuo kikuu cha
Tiba na Sayansi Shirikishi(MUHAS) Dkt.Ave Maria Semakafu akimueleza
jambo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella
Mukangara(mwenyekoti jekundu) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Sihaba
Nkinga.
Katibu wa Jukwaa la Wahariri
akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bi. Sihaba Nkinga wakati wa kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano
Serikalini leo Mjini Mtwara.
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha
Maafisa Mawasiliano Serikalini(TAGCO) Bw. Innocent Mungy akiwasilisha
Mada kwa washiriki wa Mkutano huo kuhusu wajibu wa Maafisa Mawasiliano
Serikalini katika kuimarisha mawasiliano ya serikali kwa umma.
Mjumbe wa Jukwaa la wahariri Bw. Salim Salim akiwaeleza washiriki wa mkutano huo Umuhimu wa kuwa na Usiri katika utendaji kazi.
…………………………………………………………………………….
Na Frank Mvungi-MAELEZO
Serikali imevitaka vyombo vya Habari nchini kuwaelimisha
wananchi kuhusu Katiba inayopendekezwa ili waweze kujitokeza kwa wingi
kuipigia kura
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Vijana utamaduni na Michezo
Mh.Dkt Fenella Mukangara wakati wa akifungua kikao Kazi cha Maafisa
Mawasiliano Serikalini kinachofanyika Mkoani Mtwara.
Akifafanua Mh.Dkt Mukangara amewataka Maafisa Mawasiliano
Kushirikiana na vyombo vya habari katika kuuelimisha umma kuhusu Katiba
nayopendekezwa ili wananchi waweze kufanya uamuzi sahihi wakati wa
kupiga kura ya maoni.
Akizungumzia swala la wananchi kujiandisha ili wapate fursa ya
kupiga kura ya maoni Dkt Mukangara amesema ni vyema Maafisa Mawasiliano
wakashirikiana na vyombo vya habari kuwahamasisha wananchi kujiandisha
kwa wakati muafaka.
Pia Waziri Mukangara alisisitiza kuwa Serikali kwa kutambua
umuhimu wa kuimarisha uhuru wa wajibu wa vyombo vya habari pamoja na
wajibu wa Maofisa Mawasiliano kutoa taarifa kwa umma ndio maana imeandaa
kikao kazi hicho.
Aidha Dkt. Fenella alisema kuwa ushirikiano kati ya Maafisa
Mawasiliano Serikalini na Wahariri wa vyombo vya habari hapa nchini
utasaidia kutafuta namna bora ya kutoa habari kwa umma na kwa usahihi na
weledi unaohitajika.
Kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinafanyika Mkoani
Mtwara kuanzia Januari 26,hadi februari Mosi 2015 katika ukumbi wa NAF
Hotel Mkoani Mtwara kikiwashirikisha wahariri wa vyombo kutoka vyombo
mbalimbali vya Habari hapa nchini.
No comments:
Post a Comment