By Abou Shatry Washington DC
Lori maalumu la usafishaji likiondoa theluji iliondoka barabara ya South Church Street, katika mji wa Hazleton, Pennsylvania siku ya Jumatatu Jan 26, 2015. Photo via .dailymail.co.uk
Zaidi
ya watu 60 million wataathirika kutokana na kimbunga kikubwa cha upepo
unaoambatana na unyeshaji wa theleji katika eneo la kaskazini mashariki
ya Marekani.
Lori maalumu la usafishaji likiondoa theluji iliondoka barabara ya South Church Street, katika mji wa Hazleton, Pennsylvania siku ya Jumatatu Jan 26, 2015. Photo via .dailymail.co.uk
Kwa mujibu wa kitengo cha hali
ya hewa nchini Marekani, imetaja maeneo ambayo yataathiriwa na dhoruba
hiyo, ya kihistoria ambayo itapelekea zaidi ya watu kadhaa kukosa huduma
ya umeme, pamoja na huduma za usafiri wa anga na nchi kavu.
Imetaja baadhi ya majimbo ambayo
yatakumbwa na kimbunga hicho kuwa ni New York, New Jersey,
Massachusetts, Connecticut na Rhode Island, ambapo imepelekea viongozi
wakuu wa majimbo hayo kutangaza hali ya hatari kwa tukio hilo ambalo
litatokea siku ya Jumatatu, Jumanne na Jumatano.
Imetabiriwa kiasi cha unyeshaji
wa theluji hiyo 36inches katika jimbo la New York 16 hadi 26 inches
katika jimbo la Boston, na kiwango kingine kama hicho katika baadhi ya
majimbo mengine
Zaidi ya safari za ndege 3,800
zimesimamishwa mapema leo Jumaatatu katika viwavya vya ndege vya JFK,
LaGuardia na Newark airports, pia huduma za shule kufungwa siku ya
jumanne na jumatano katika majimbo hayo.
Chanzo: swahilivilla
No comments:
Post a Comment