Meneja Kiongozi wa Bima ya Afya
CHIF Kanda ya Ilala, Christopher Mapunda akifunga semina ya siku tatu ya
viongozi wa SACCOS za wajasiriamali zilipo Mansipaa ya Ilala
iliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.
PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWEBLOG
Afisa Matekelezo Bima ya afya NHIF
kanda ya Ilala, Hipoliti Lello akifafanua jambo kuhusina na kiwango cha
uchangiaji kwa wajasiriamali ni shilingi za kitanzania 76,800 ambacho
kinamwezesha mjasiriamali kuweza kupata matibabu kwenye zahanati, kituo
cha afya, hospital za wilaya, mikoa na za rufaa nchini.
Raymond akichangia mada yake wakati wa semina hiyo
Viongozi wa Bima ya afya NHIF pamoja na wajasiriamali wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa semina hiyo.
…………………………………………………………………………………………………
BIMA YA AFYA nchini (NHIF) imetoa
mafunzo ya umuhimu wa Bima ya afya kwa wajasiriamali wasiyokuwa katika
sekta rasmi lenye lengo la kuhamasisha jamii kwenye makundi mbalimbali
kujiunga na mfuko huo.
Akifunga semina ya siku tatu jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki,Meneja Kiongozi wa Bima ya Afya Kanda ya Ilala, Christopher Mapunda
alisema kwamba bima ya afya nchini itaendelea kutoa mafunzo kwa
wanajamii ili waweze kujiunga na mfuko wa bima ya afya nchini.
“Mfuko wa bima ya afya nchini utaendelea kutoa elimu kwa makundi
mbalimbali hasa yale yaliyopo kwenye sekta isiyo rasmi nchini kuweza
kuweka akiba kwa ajili ya bima ya afya kwa manufaa yao na vizazi vyao,”
alisema Bw, Mapunda
Bw Mapunda aliongeza kwamba mafunzo hayo ya siku tatu
yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa baada ya washiriki kujitokeza kwa wingi
na kuonyesha nia ya kujiunga na mfuko huo kwa maisha ya baadaye.
Aliongeza kwamba dhamira na dira ya mfuko huo ni kuwahikisha
watanzania wengi wanajiunga na mfuko sambamba na kupata elimu kuhusu
bima ya afya kwa maisha yao.
Alisema kwamba mfuko huo utaendelea kutoa mafunzo juu ya umuhimu
wa bima ya afya na wana mpango wa kuendelea na mafunzo mpaka visiwani
na si bara.
Kwa upande Hipoliti Lelo, Afisa Matekelezo Bima ya afya kanda ya
Ilala alisema kwamba wameamua kuleta bima hiyo afya kwa wajasiriamali
wasio katika sekta rasmi ili waweze kupata uhakika wa matibabu kupitia
mfuko wa bima ya afya nchini
Alisema kwamba kiwango cha uchangiaji kwa wajasiriamali ni
shilingi za kitanzania 76,800 ambacho kinamwezesha mjasiriamali kuweza
kupata matibabu kwenye zahanati, kituo cha afya, hospital za wilaya,
mikoa na za rufaa nchini.
Alifafafua kwamba hiyo ni fursa pekee kwa mjasiriamali nchini
kuweza kupata matibabu hata kama hayupo kwenye mfumo rasmi wa ajira
nchini.
Naye Mjumbe wa Bodi Saccos ya wajasiriamali, Bw, Adela Raymond
alisema kwamba waliona umuhimu wa kujiunga na mafunzo kwanza ya bima ya
afya kutokana na matatizo yaliyokuwa yanajitokeza kwa wanachama wao hasa
wakati wa marejesho.
“Mwanachama wetu wa Saccos akiumwa tu anakwambia hawezi kuleta
marejesho na fedha hizo ametumia kwa ajili ya matibabu kwa hiyo tukaona
kuna umuhimu wa chama kuijunga na mfuko wa bima ya afya nchini ,”
alisema
Alifafanua kwamba umuhimu wa bima hiyo kwa wanachama ni kwamba
wanaweza kurudisha marejesho na kuendelea kupata matibabu kupitia mfuko
huo wa bima nchini.
No comments:
Post a Comment