Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wan Kijeshi mjini Riyadh,
Saudi Arabia, asubuhi ya Jumapili, Januari 25, kuhani kifo cha
Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita. Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah,Rais Kikwete ataendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.

PICHA NA IKULU Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akiwasili mjini Riyadh, Saudi Arabia,asubuhi ya leo, Jumapili, Januari
25, 2015, kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud
aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita.
Baada ya kuhani msiba wa Mfalme
Abdullah, Rais Kikwete ataendelea na safari yake kwenda nchi za
Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.
Mjini Berlin, Ujerumani ambako
Rais Kikwete alitarajiwa kuwasili kesho, Jumatatu, Januari Ishirini na
Sita, akitokea Riyadh, Saudi Arabia, anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa
Kimataifa wa Global Alliance for Vaccines and Immunization (Gavi
Alliance) ambako viongozi mbali mbali duniani watajadili jinsi ya
kuboresha mipango ya utoaji chanjo kwa watoto wadogo hasa katika nchi
zinazoendelea.
Baada ya kumaliza ziara yake
Ujerumani, Rais Kikwete atakwenda Ufaransa ambako miongoni mwa mambo
mengine atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Ufaransa.
Aidha, Rais Kikwete atafungua jengo jipya la Ubalozi wa Tanzania katika Ufaransa na pia nyumba ya balozi.
Rais Kikwete baada ya kumaliza
ziara zake za kikazi katika Ujerumani na Ufaransa atakwenda Addis Ababa,
Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa
Afrika (AU).
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
25 Januari, 2015
No comments:
Post a Comment