MSANII
wa muziki wa kizazi, kipya mjini Iringa, ONE LEE akitoa zawadi kwa
mwandishi wa Habari Frank Kibiki kwa niaba ya wasanii wenzake.
================================================
MSANII wa muziki wa kizazi, kipya
mjini Iringa, ONE LEE akitoa zawadi kwa mwandishi wa Habari Frank
Kibiki kwa niaba ya wasanii wenzake, ambaye hivi karibuni alitangaza nia
ya kugombea ubunge katika jimbo la Iringa mjini.
Akizungumza na waandishi wa habari
mjini Iringa, wasanii hao walisema wameamua kutengeneza wimbo huo
kutokana na mchango mkubwa wa mwanahabari huyo, katika fani yao.
Msanii huyo Richard Kayombo ‘One
Lee’ ambaye alikabidhi wimbo kwa niaba ya wasanii wenzake alisema wimbo
huo, unamtambulisha Kibiki, kama kiongozi wa kuigwa kutokana na tabia
yake ya ucheshi na kujichanganya na watu.akizungumza wakati wa kukabidhi
WIMBO huo msanii ‘One Lee’ alisema kuwa FRANK KIBIKI amekuwa akiwapa
elimu vijana juu ya kujitambua na kuwasaidia jinsi gani ya kujiajili wao
wenyewe na kuonyesha njia ya kutokea kimaisha na dio imekuwa sababu ya
wasanii wa mkoani hapa kutunga wimbo huo.
“Wimbo unaitwa ‘Kuwa mfano wa kuigwa’, tumempa kaka yetu kama zawadi, ili wengine waige mfano wake.
Awali tulitamani uitwe Kibiki, lakini kwa sababu tunataka kuuza tumeamua kuuita jina hilo,”alisema One lee.
Alisema miaka miwili iliyopita,
aliwahi kukutwa na jambo ambalo alihitaji msaada wa haraka, alihangaika
lakini alipokutana na Kibiki ambaye ni Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM
taifa, alisaidiwa jambo ambalo lilimfanya aanze kumuheshimu.
Alisema aliposikia kuwa Kibiki
ametangaza nia, aliamua kushirikiana na wenzake ili watengeneze wimbo
ambao hivi karibuni utaachiwa hewani.
‘One lee’alisena ngoma yake
itamtambulisha Kibiki kama alivyo, na kwamba wameamua kumsaidia bila
gharama yoyote kama sehemu ya mchango wao wakiamini ikiwa atafanikiwa
kupenya na kupata nafasi hiyo, ataweza kuwaunganisha na kuwainua
wasanii.
kwa upande wao wasanii wengine wa
mkoani irnga walisema kuwa imefika wakati sasa iringa mjini itawaliwe na
kiongozi mwenye uelewa juu ya kukuza uchumi wa mkoani na kuzingatia
vipaji vya vijana kwa kuwa vijana ndio taifa la leo.
No comments:
Post a Comment