Mwezeshaji kutoka Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa wa pili kushoto
akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Eng.
Harold D. Sawaki katikati walipofika Wilaya ya Rungwe jana kutoa elimu
ya ujasiriamali kwa vijana wa Wilaya hiyo. Kulia ni Afisa Maendeleo ya
Jamii Bw. Ason Nzowa, wa pili kulia ni Afisa Michezo na Vijana Mkoa wa
Mbeya Bw. George Mbijima na wa kwanza kushoto ni Afisa Maendeleo ya
Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina
Sanga.
Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga kulia
akizungumza na vijana wa Wilaya ya Rungwe wakati wa semina ya
Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana
jana karika Wilaya ya Rungwe. Katikati ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa na kushoto ni Mkuu
wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele.
Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda
Mbeya Bw. Laurean Masele akitoa mada wakati wa semina ya Ujasiriamali,
Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana karika
Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.
Kijana Daudi Essau Seme kutoka
katika kikundi cha Tukuyu Bodaboda Saccoss Limited akichangia wakati wa
semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya
Vijana jana karika Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.
Baadhi ya vijana wa Wilaya ya
Rungwe katika kikundi wakijadiliana namna ya kuandika andiko la mradi
baada ya kuelimishwa wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha,
Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana katika Wilaya ya Rungwe Mkoa
wa Mbeya.
Maafisa kutoka Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo wakimsikiliza kwa makini kijana Boniel Soka
(kushoto) kutoka kikundi cha Muungano Makandana kinachojishughulisha na
upandaji miti ya aina mbalimbali wakati wa ziara ya kukagua miradi ya
vijana wa Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.
Picha zote na : Genofeva Matemu – Maelezo. Rungwe, Mbeya
No comments:
Post a Comment