Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akizungumza na vyombo vya habari jioni hii wakati akitangaza mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri,Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Mwishoni mwa juma ametangaza mabadiliko madogo
katika Baraza lake la Mawaziri,ambalo Aliliapisha siku hiyo Ikulu,Jijini
Dar es Salaam.
Akitangaza uteuzi huo muda mchache
kabla ya Mawaziri hao kuapishwa, Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni
Sefue alisema uteuzi huo ulihusu pia kujaza nafasi mbili zilizoachwa
wazi na Profesa Anna Tibaijuka Na Profesa Sospeter Muhongo.
Profesa Tibaijuka, aliyekuwa Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alieachishwa kazi kutokana na
kuhusika kwake katika sakata la akaunyti ya Tegeta Escrow.
Kwa upande wa Profesa Muhongo
aliachia ngazi mwenyewe mapema siku ya ijumaa , kwa kile alichotaja kuipisha
Serikali iendelee kuwatumikia Wananchi badala ya kuendelea na malumbano
ya Escrow.
Katika mabadiliko hayo,sura mpya za manaibu mawaziri zimeingia na baadhi ya mawaziri wamehamishwa wizara.
Akitangaza Mabadiliko hayo,Balozi Sefue aliwataja mawaziri hao kama ifuatavyo.
MAWAZIRI
1. Mh. George Simbachawene – Waziri wa Nishati na Madini
2. Mh. Mary Nagu – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mahusiano na Uratibu)
3.Mh. Christopher Chiza – Waziri Uwezeshaji na Uwekezaji
4. Mh. Harrison Mwakyembe – Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
5.Mh. William Lukuvi – Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi
6.Mh. Steven Wasira – Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika
7.Mh. Samwel Sitta -Waziri wa Uchukuzi
8.Mh. Jenista Muhagama – Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge
MANAIBU WAZIRI
1. Stephen Masele – Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu Rais – Muungano
2. Mh. Angela Kairuki – Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi
3. Mh. Ummy Mwalimu – Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
4. Mh. Anna Kilango – Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
5 . Mh. Charles Mwijage – Naibu Waziri wa Nishati na Madini
No comments:
Post a Comment