Katibu
Bodi ya Filamu Tanzania Bi,Joyce Fissoo(kushoto) akifafanua jambo
wakati wa kikao kilichofanyika leo kuhusu suala zima la bei za
filamu,kulia ni Kaimu mkurugenzi wa idara ya Maendeleo ya Utamaduni
Bi.Lilly Beleku.
………………………………………………………………………
Na Frank Shija.WHVUM
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mukandala Lufufu inayojishughulisha na
kazi ya kutafsiri Filamu kwa Lugha ya Kishwahili Bw. Derick Mukandala
maarufu kwa jina la Mzee Lufufu amekiri kuwa kazi yake anaifanya
kienyeji ili hali akifahamu ni makosa.
Kauli hiyo ameitoa jana katika kikao baina yake na Bodi ya
Filamu ambapo alieleza kuwa amekuwa akifanya kazi hiyo kwa muda mrefu
bila kuzingatia utaratibu huku akijua kuwa ni makosa kwa mtu kutumia
kazi ya msanii mwingine bili idhini yake.
“Nikiri tu kwamba nimekuwa nikifanya makosa kwa kutafsiri Filamu bila kuwa na idhini ya wahusika wa filamu hizo” Alisema Lufufu.
Mzee Lufufu aliongeza kuwa amekuwa akifanya kazi hiyo ya kutafsiri Filamu bila vibali akiamini kuwa hakuna ubatili wowote.
Aidha Mzee Lufufu pamoja na kujua ni makosa kutafsiri Filamu
bila idhini alikuwa anatarajia kufanya kazi na Kampuni moja ya kutoka
nchini Norway ambapo kama amngefanikiwa kufanya Documentary ambayo
ingejulikana kwa jina la “The Film Dubber from Dar es Salaam – Mzee
Lufufu” hiyo ingeaminisha ulimwengu kuwa Tanzania inaruhusu uharamia wa
kazi za wasanii kitu ambacho siyo sahihi.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce
Fissoo amesema kuwa siyo dhambi kutafsiri Filamu, ila ni lazima
anayetaka kufanya kazi hiyo azingatie dheria za nchi na taratibu
zinaotakiwa kuzingatiwa.
Fissoo amesema kuwa sheria ya Filamu nchini kifungu namba 17
kinamtaka anayetaka kufanya kazi ya kutafsiri awasilishe muswada wake
katika ofisi za Bodi ya Filamu ili uhakikiwa na wataalamu kabla ya
kupewa idhini ya kuendelea na kazi hiyo.
Aliongeza kuwa ili kazi ya kutafsiri Filamu ni sharti mhusika
kupata idhini ya mwenye Haki Miliki ya filamu husika hivyo ni vyema
kuwasiliana na COSOTA ili kufanya utaratibu wa kupata uhalali akitolea
mfano wa Filamu ya Nelia iliyotengenezwa nchini Zimbabwe na baadaye
ilifanyiwa tafsiri katika lugha ya Kiswahili hapa jijini Dar es Salaam
baada ya kufuata taratibu zote.
No comments:
Post a Comment