SERIKALI Mwishoni mwa juma ilisema kuwa mradi wa
ujenzi wa Chuo cha Tiba cha Kimataifa cha Muhimbili eneo la
Mloganzila nje kidogo ya jiji la Dar es salaam utagharimu kiasi cha Dola
za kimarekani Milioni 61.
Katika mradi huo serikali ya
Tanzania imechangia dola za
kimarekani milioni 18 na serikali ya Jamhuri ya Korea imetoa mkopo wa
dola za kimarekani milioni 43 ili kufanikisha ujenzi wa chuo hicho
katika eneo la Mlonganzila jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya
kukamilisha ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho jana
jijini Dar es salaam Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt.Shukuru
Kawambwa alisema kuwa mradi huo na unatarajiwa kukamilika mwezi Machi
mwakani.
“Tumejipanga vizuri kujenga
Chuo hiki cha Tiba ambacho kitakua mji wa tiba hapa nchini, sisi kama
serikali tumeiona changamoto ya wataalam wa afya nchini na kuona ni
vyema kujenga chuo cha kisasa kitakachokua na uwezo wa kupokea zaidi ya
wanafunzi 15,000 kwa mwaka watakaosaidia kuondoa tatizo la wataalamu
wa afya.” alisema Dkt.Kawambwa.
Dkt. Kawambwa alisema kuwa mbali
na ujenzi wa chuo hicho, serikali itajenga hospitali nyingine ya
Muhimbili ambayo ujenzi wake utamalizika sambamba na ujenzi wa chuo
hicho ili kuwawezeha wananchi kupata huduma bora za afya.
Alibainisha kuwa hospitali hiyo
pindi itakapokamilika itakuwa kubwa zaidi na yenye vifaa vya kisasa
itakayosaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa uliopo katika hospitali
ya Taifa Muhimbili pamoja na kuwasaidia wanafunzi kupata sehemu ya
mafunzo kwa vitendo.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa
Chuo cha Tiba Muhimbili Prof. Ephata Kaaya alisema mradi huo
umegawanyika katika awamu mbili, awamu ya kwanza ikihusisha ujenzi wa
chuo cha tiba na Hospitali ya kisasa ya muhimbili na awamu ya pili
itakuwa ujenzi wa hospitali kubwa ya kutibu magonjwa ya Moyo na mishipa
ya fahamu.
“ Tayari Benki ya Maendeleo
Afrika imetoa kiasi cha zaidi ya dola za kimarekani milioni 9 kwa ajili
ya ujenzi wa Chuo na hospitali ya kimataifa ya magonjwa ya moyo na
mishipa ya fahamu itakayokuwa na ubora wa hali ya juu katika nchi za
Afrika Mashariki” alisisitiza Prof.Kaaya .
Aliongeza kuwa gharama ya vifaa
tiba ikiwemo vya uchunguzi na upasuaji utagharimu zaidi ya dola za
kimarekani Milioni 27 na kueleza kuwa mkandarasi wa kufunga vifaa tiba
vya mradi huo ameshapatikana na anatarajia kuanza kufanya kazi hiyo
hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment