Mtu mmoja mkazi wa kitongoji cha chang’ombe auawa kwa kupigwa na wananchi.
Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha
mkutano wilayani momba auawa na kisha mwili wake kutupwa shambani.mtu
mmoja mkazi wa ilomba jijini mbeya afariki dunia papo hapo baada ya
kugongwa na semi traller.
KATIKA TUKIO LA KWANZA
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina
la mwinzala sekele mwenye umri kati ya miaka 40 – 45 Mkazi wa kitongoji
cha chang’ombe – mshewe aliuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili
wake na kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi.
mwili wa marehemu ulikutwa
umetelekezwa mnamo tarehe 26.01.2015 majira ya saa 11:00 Asubuhi huko
katika kijiji na kata ya mshewe, tarafa ya bonde la usongwe, wilaya ya
kipolisi mbalizi,
Inadaiwa kuwa
chanzo cha tukio hilo ni kulipiza kisasi kufuatia marehemu kutuhumiwa
Kuhusika katika tukio la mauaji ya sekela kaini mkazi wa kijiji cha
mshewe ambaye alikutwa ameuawa na kutupwa katika shamba la mahindi
kijijini hapo tarehe 24.01.2015 majira ya saa 15:45 alasiri.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa
mbeya kamishna msaidizi wa polisi barakael n. masaki anatoa wito kwa
yeyote mwenye taarifa za mahali walipo watuhumiwa waliohusika katika
tukio hili Azitoe katika mamlaka husika kwa hatua zaidi za kisheria
wakati uchunguzi na upelelezi zaidi wa tukio hili unaendelea.
KATIKA TUKIO LA PILI:
Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha
mkutano wilayni momba aliyetambulika kwa jina la hamis Simwawa (25)
alikutwa ameuawa shambani kwa kukatwa shoka shingoni na kisha
kunyofolewa viungo vya mwili ambavyo ni ulimi, meno ya chini na jicho la
kushoto.mwili wa marehemu ulikutwa shambani mnamo tarehe 26.01.2015
majira ya saa 08:00 asubuhi Huko katika kijiji cha mkutano, kata ya
nzoka, tarafa ya ndalambo, wilaya ya momba, mkoa wa mbeya. inadaiwa kuwa
kabla ya watu hao kufanya tukio hilo walimwita marehemu ili awasaidie
kazi za shambani na kisha kumuua. inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni
imani za kishirikina. watuhumiwa wawili wamekamatwa kuhusiana na tukio
hilo ambao ni 1. kawawa sinkala (31) na 2. emanuel sinkala (15) wote
wakazi wa kijiji cha mkutano.
KATIKA TUKIO LA TATU:
Mtu mmoja mkazi wa ilomba jijini
mbeya aliyefahamika kwa jina la joshua andendekisye Mwaisanila (35)
alifariki dunia baada ya kugongwa na gari lenye namba za usajili t.189
blk/t.193 blk Aina ya semi traller lililokuwa likiendeshwa na dereva
aitwaye ahazi cheyo (24) mkazi wa iyunga jijini mbeya.
Aukio hilo limetokea mnamo tarehe
26.01.2015 majira ya saa 09:05 asubuhi huko forest katika Barabara ya
mbeya/tunduma. chanzo cha ajali kinachunguzwa. dereva amekamatwa. mwili
wa marehemu umehifadhiwa.
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa
mbeya kamishna msaidizi wa polisi barakael n. masaki Anatoa wito kwa
madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na
kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali
zinazoepukika.
imeasainiwa na:
[barakael n. masaki – acp]
kaimu kamanda wa polisi mkoa wa mbeya.
No comments:
Post a Comment