Mkuu wa Wilaya Temeke, Sofia Mjema, kulia akimkabidhi cheti Mr Yakubu
kwa kutambua mchango wake kwa maendeleo ya shule ya Twayyibat Islamic
Seminary, iliyopo Temeke, jijini Dar es Salaam jana.
Meneja wa Skywadrs Construction, Saeed Pirbaksh Mulla, akipokea cheti
cha kutambua mchango wa kampuni yao kwenye shule hiyo. Cheti hicho
anakabidhiwa na Mkuu wa Wilaya Temeke, Sofia Mjema, kulia.
Wadau
wa Elimu, Abdulaziz Jaar kulia, akizungumza jambo katika matembezi ya
Shule ya Kiislamu ya Twayyibat Islamic Seminary ya Temeke jijini Dar es
Salaam. Katikati ni mdau kutoka Yukubu Chamber&Associate.
MKUU wa wilaya Temeke, DC Sophia Mjema, ameipongeza shule ya
Sekondari ya Kiislamu inayojulikana kama Twayyaibat Islamic Seminary Secondary
School kwa kufanya ada nafuu inayoweza kuwafanya wazazi na walezi wamudu
gharama za kusomesha watoto kwenye shule binafsi.
mwanafunzi
kutoka Twayyibat Islamic Seminari akisoma Quraan katika shule hiyo
walipotembelewa na Mkuu wa Wilaya Temeke, Sofia Mjema, hayupo pichani.
DC Mjema aliyasema hayo alipofanya ziara katika shule hiyo na
kukuta uongozi wa Twayyaibat, ukitoa ada ya Sh 200,000 tu kwa mwaka, jambo
ambalo ni agharabu mno hususan kwa shule za kulipia na zinazomilikiwa na
taasisi za kidini.
Akizungumza kwa mshangao mkubwa mbele ya wadau wa elimu, DC
Mjema alisema ameshangazwa na shule hiyo kufanya ada nafuu, hivyo ni jukumu la
wazazi na walezi kujitokeza kuwasomesha watoto wao kwa nguvu zote.
Alisema pamoja na ada hiyo kuwa nafuu, ni jukumu la serikali
hususan Halmashauri ya Wilaya Temeke kupanga mbinu bora zinazoweza kuisaidia
shule hiyo kwa hali na mali ili waweze kufanya kazi ya kutoa elimu kwa kiwango
cha juu.
“Hii naweza kuiita shule ya sekondari ya mshangao hasa baada
ya kuona unafuu wa ada yake, nikiamini kuwa Dunia ya leo kukuta unafuu wa namna
hii unaonyesha namna gani kuna wadau wana mtazamo wenye maendeleo.
“Naomba wadau, walezi, wazazi na serikali kupanga namna wanavyoweza
kuisaidia Twayyaibat ili waweze kuhakikisha kuwa vijana wetu wanasoma kwa bidii
kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi kwasababu Dunia ya leo elimu ni lazima,”
alisema DC Mjema.
Naye Mkuu wa Shule hiyo, Juma Omari, alisema shule yao
imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na kutoa ufaulu wa kufurahisha, huku
akiihakikishia serikali kuwa watajitahidi kuwapa mwanga wa kielimu watoto
wanaosoma kwenye shule hiyo.
“Tangu shule hii ilipoanzishwa mwaka 1996 imekuwa na
mafanikio makubwa kutokana na matokeo yake ya Taifa, hili linatufanya tuongeze
bidii katika kufundisha wanafunzi wetu tukiamini ndio mpango sahihi,” alisema.
Katika hatua nyingine, DC Mjema alitumia muda huo kukabidhi
vyeti vya kuthamini mchango wa wadau wanaoisaidia shule hiyo, huku waliopewa
vyeti hivyo ni Skywards Construction, Yakubu Chamber&Associate, Mheshimiwa
Adam Malima, Sheimar Kweigir, Zainabu Vulu, Alosco.
Kazumari Nambeya, akiiwakilisha Home Shooping Centre katika kupokea
cheti cha kutambua mchango wa shule hiyo, mbele ya Mkuu wa wilaya
Temeke, Sofia Mjema, jana, jijini Dar es Salaam.
Alisema pamoja na ada hiyo kuwa nafuu, ni jukumu la serikali
hususan Halmashauri ya Wilaya Temeke kupanga mbinu bora zinazoweza kuisaidia
shule hiyo kwa hali na mali ili waweze kufanya kazi ya kutoa elimu kwa kiwango
cha juu.
“Hii naweza kuiita shule ya sekondari ya mshangao hasa baada
ya kuona unafuu wa ada yake, nikiamini kuwa Dunia ya leo kukuta unafuu wa namna
hii unaonyesha namna gani kuna wadau wana mtazamo wenye maendeleo.
“Naomba wadau, walezi, wazazi na serikali kupanga namna wanavyoweza
kuisaidia Twayyaibat ili waweze kuhakikisha kuwa vijana wetu wanasoma kwa bidii
kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi kwasababu Dunia ya leo elimu ni lazima,”
alisema DC Mjema.
Naye Mkuu wa Shule hiyo, Juma Omari, alisema shule yao
imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na kutoa ufaulu wa kufurahisha, huku
akiihakikishia serikali kuwa watajitahidi kuwapa mwanga wa kielimu watoto
wanaosoma kwenye shule hiyo.
“Tangu shule hii ilipoanzishwa mwaka 1996 imekuwa na
mafanikio makubwa kutokana na matokeo yake ya Taifa, hili linatufanya tuongeze
bidii katika kufundisha wanafunzi wetu tukiamini ndio mpango sahihi,” alisema.
Katika hatua nyingine, DC Mjema alitumia muda huo kukabidhi
vyeti vya kuthamini mchango wa wadau wanaoisaidia shule hiyo, huku waliopewa
vyeti hivyo ni Skywards Construction, Yakubu Chamber&Associate, Mheshimiwa
Adam Malima, Sheimar Kweigir, Zainabu Vulu, Alosco.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema, akizungumza na wanafunzi na
wadau wa shule ya Twayyibat, iliyopo Temeke, jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Wilaya Temeke, Sofia Mjema, akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau
mbalimbali wa elimu na wasaidizi wa shule ya Twayyibat Islamic, iliyopo
Temeke, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment