Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Hellen
Kijo-Bisimba (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari Dar es Salaam mwishoni mwa juma , wakati akitoa taarifa kuhusu
changamoto za utekelezaji wa sheria ya kura ya maoni ya Katiba. Kulia ni
Mratibu wa Katiba wa LHRC, Anna Henga na Mkurugenzi wa Fedha na
Utawala, Ezekiel Massanja.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo
Wapiga picha na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
………………………………………………………………………………………………………….
Dotto Mwaibale
KITUO cha Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC) kimesema kina wasiwasi na mchakato wa kura ya maoni
inayotarajiwa kufanyika kwa sabau ya muda mdogo ulibaki ikizingatiwa
daftari la wapigakura halijafanyiwa marekebisho pia watanzania wengi
hawana uelewa na katiba iliyopendekezwa.
Kituo kimetoa mapendokezo kwa Serikali kuahirisha tarehe ya kupiga kura ya maoni kwa kile kilichodaiwa katiba inayopendekezwa inamapungufu na yasiporekebishwa muda huu yanaweza kuathiri kura ya maoni na kuwakosesha watanzania wengi kushiriki haki yao kikatiba.
Akizungumza Dar es Salaam mwishoni wa juma , Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, DK. Hellen Kijo- Bisimba alisema kituo hicho kimekuwa na utaratibu wa kufuatilia mchakato wa katiba, kubaini mapugufu mengi likiwemo la muda mdogo na wananchi wengi kutoelewa vizuri katiba inayopendekezwa.

“Mchakato wa kura ya maoni
unaenda kukamilika Februari 28 kwa mjibu wa sheria ya kura hiyo.Tume ya
Taifa ya Uchaguzi inapaswa kuboresha daftari la wapiga kura ndipo kura
ipigwe, ukizingatia zimebaki siku takribani 25 kufikiaki hitimisho,sisi
tunaona kuna changamoto ya muda na ni vyema zoezi hilo lisongezwe
mbele,”alisema.
Aliongeza kuwa vifaa vya BRV
vinavyotarajiwa kutumika kwa mara ya kwanza na tume ya uchaguzi
vimeonesha changamoto katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na hivyo
kituo hicho kinawasiwasi na mchakato mzima wa upatikaji wa katiba iliyo
bora.
“Kifungu cha 10 katika katiba
inayopendekezwa kimezungumzia vituo vya kupigia kura, kwamba vitapangwa
kulingana na maeneo yaliyo na watu wengi katika maeneo husika wasiwasi
wangu hapa tume inaweza kutotumia majimbo ya zamani na kutengeza majimbo
mpya,”alisema.
Bisimba alisema changamoto
nyingine katika mchakatio huo ni Usajili wa kamati za kura ya maoni
katika kuikubali au kuikataa kura hiyo katiba inaelekeza kamati ni
lazima ipeleke maombi kabla ya siku 21 kupigwa kwa kura ya maoni.
“Utaratibu ambao sisi kulingana
na uzoefu wetu wa kufanya kazi tunaona haya ni masharti magumu
yanayoekekezwa kwenye kamati za kura, kwani inawataka pia kueleza vyanzo
vya mapato yao kitu ambacho kinaweza kusababisha kamati zingine
kutopata usajili,”alisema.
Dk.Bisimba aliongeza kuwa
changamoto ambayo kituo kinaona kuwa ni kiini macho ni pale inapoelezwa
kwamba wanzazibar waishio Tanzania bara wakipiga kura kura zao
zitahesambiwa upande wa zanzibar.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment