Uongozi wa chama cha soka mkoa
wa Dar es salaam,DRFA,umewaomba,mashabiki na wote wenye mapenzi mema ya
kandanda,kujitokeza kwa wingi kuzishangilia timu za Dar es salaam
zinazoshiriki ligi kuu,Daraja la kwanza na michuano ya taifa Cup
wanawake ,ili kutoa hamasa kwa wachezaji.
Kesho (januari 28) kutakuwa na
mchezo mmoja wa ligi kuu kwa timu ya Simba ya Dar es salaam dhidi ya
Mbeya City ya Mbeya,mchezo ambao utakaopigwa katika uwanja wa taifa
jijini.
Itakumbukwa kwamba katika mechi
mbili za ligi msimu uliopita,Simba na Mbeya City hakuna aliyefanikiwa
kumfunga mwenzake,na kujikuta wakiambulia sare ya 1-1 kule uwanja wa
Sokoine,na ule wa marudiano uliopigwa kwenye uwanja wa taifa nao kwenda
sare ya 1-1.
Katika michuano ya taifa
Cup,Temeke na Ilala zimefanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali
baada ya kupata ushindi kila moja katika mechi za robo fainali
zilizopigwa leo (januari 27),ambapo Temeke imeiangamiza bila huruma
Mbeya mabao 3-0,huku Ilala ikiizodoa Iringa kwa mabao 2-1.
Aidha DRFA imeipongeza timu ya
Kinondoni ambayo haikufanikiwa kuingia katika hatua ya mtoano,kwa juhudi
kubwa na ushindani iliouonesha licha ya kuondolewa katika hatua ya
makundi.
Viongozi wa DRFA wamekuwa mfano
kwa kujitokeza kushuhudia mechi hizo za Taifa Cup,Ligi kuu na zile za
Daraja la kwanza,ili kuongeza chachu kwa timu za Dar es salaam kufanya
vizuri.
No comments:
Post a Comment