TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Monday, January 26, 2015
KINANA APOKELEWA KWA MCHAKAMCHAKA WA NGUVU JIMBO LA DONGE
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa nne kutoka kushoto akipokelewa kwa mchakamchaka na Mbunge wa jimbo la Donge na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Sadifa Juma Khamis wa tatu kutoka kushoto pamoja na vijana wa jimbo hilo ambao walikimbia naye umbali wa kilomita moja wakiwa katika mapokezi hayo yaliyotia fora mara baada ya kuanza ziara yake katika jimbo hilo mwishoni mwa juma akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana yuko katika ziara ya visiwa vya Unguja na Pemba Zanzibar akihimiza uhai wa Chama cha Mapinduzi na kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akiwa sambamba na Nape Nnauye katika mchakamchaka wakati wa mapokezi hayo katika jimbo la Donge Kaskazini Unguja.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
katikati, Mbunge wa jimbo la Dole Sadifa Juma Khamis wakikabidhi mifuko ya saruji kwa Bakari Ame Hussein mwalimu mkuu wa skuli ya msingi ya Mahonda jimbo la Donge.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akizungumza na wanafunzi wa Skuli ya Awali Mahonda jimbo la Donge.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akifurahia jambo wakati Salum Gharib Salum Mwenyekiti wa kamati ya Skuli ya Sekondari ya Bumbwini Misufini jimbo la Dole mara baada ya kupokea mifuko 50 ya saruji kutoka kwa mbunge wao Sadifa Juma Khamis na Mabati 200 kutoka kwa Katibu Mkuu Abulrahman Kinana
Salum Gharib Salum Mwenyekiti wa kamati ya Skuli ya Sekondari ya Bumbwini Misufini jimbo la Dole
akishukuru mara baada ya kupokea misaada hiyo ya vifaa vya ujenzi kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na mbunge Sadifa Juma Khamis.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na mbunge Sadifa Juma Khamis wakishiriki ujenzi wa skuli ya Bumbwini Misufini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye wakikagua skuli ya skuli ya Mahonda.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akizungumza jambo mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushiriki ujezni wa ofisi ya CCM tawi la Muembe Jogoo.
Baadhi ya wanafunzi wa madarasa ya Amali huko Kinduni jimbo la Kitope wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati alipokagua na kujionea shughuli mbalimbali wanazofanya katika masomo yao .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi majiko ya genzi ya kupikia kwa wanafunzi vijana wa madarasa ya Amali huko Kinduni jimbo la Kitope
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakiangalia shughuli mbalimbali za vijana wa mafunzo ya Amali katika mambo ya mapishi..
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakiangalia shughuli mbalimbali za vijana wa mafunzo ya Amali katika mambo ya ushonaji wa nguo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akishiriki kazi za ushonaji huku Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiangalia shughuli mbalimbali za vijana wa mafunzo ya Amali katika mambo ya ushonaji wa nguo.
Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Maskani ya CCM Kizota jombo la Kitope.
Mbunge wa jimbo la Donge na Mwenyekiti wa UVCCM Ndugu Sadifa Juma Khamis akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.
Balozi Ali Karume akitema cheche zake kuhusu Katiba Mpya iliyopendekezwa na kuwashawishi wananchi waipigia kura ya ndiyo.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano huo uliofanyika Maskani ya CCM Kizota.
Makamu wa Pili wa Rais wa Rais wa Zanzibar Mh. Balozi Seif Ali Idd akiwahutubia wananchi wa jimbo la Kitope Kaskazini Unguja.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano huo na kuwsiki waipigie kura ya ndiyo katiba inayopendekezwa kwa kuwa ina mambo mengi yenye faida kwa wazanzibari.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd mara baada ya mkutano huo kumalizika, Kushoto anayefurahia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment