Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na waandishi
wa katika mkutano uliofanyika mchana huu kwenye ukumbi wa mikutano wa
ofisi za Wizara hiyo,zilizopo kwenye Mtaa wa Samora,Jijini Dar es
salaam.
Waziri
Muhongo ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo,kufuatia shinikizo la muda
mrefu la kumtaka afanye hivyo au awajibishwe, kufuatia mapendekezo ya
Bunge lililopita, lililoagiza serikali kuchukua hatua dhidi yake na
wengine kadhaa kufuatia kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow. Kwa hisani
ya http://issamichuzi.blogspot.com/ Waziri
Muhongo akikazia kujiuzulu kwake huko amesema kuwa yeye sio mla rushwa
bali ni mchapa kazi tu na akilizungumzia swala la akaunti ya Tegeta
Escrow ambalo ndilo lililopelekea kujiuzulu kwake huko,Waziri Muhongo
amesema kuwa sakata hilo lilitawaliwa na mambo makuu manne ambayo
aliyataja kuwa ni Mvutano wa kibiashara, Mvutano wa kisiasa, Mvutano wa
uongozi na madaraka pamoja na Ubinafsi.
No comments:
Post a Comment