Hatua
ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Taifa kwa Wanawake inachezwa
kesho (Januari 26 mwaka huu) na Januari 27 mwaka huu) kwenye Uwanja wa
Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam kwa mechi mbili kila
siku.
Mechi ya kwanza ya robo fainali ya
michuano hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Televisheni itaanza
saa 9 alasiri kwa kuzikutanisha Mwanza na Kigoma. Robo fainali ya pili
ambayo ni kati ya Tanga na Pwani itaanza saa 11 kamili jioni.
Ilala na Iringa watacheza robo
fainali ya tatu Januari 27 mwaka huu kuanzia saa 9 kamili alasiri, na
kufuatiwa na robo fainali ya mwisho saa 11 kamili jioni
itakayozikutanisha Temeke na Mbeya.
Nusu fainali za michuano hiyo
inayodhaminiwa na kampuni ya Proin zitachezwa Januari 29 mwaka huu
wakati Fainali itachezwa Februari Mosi mwaka huu kuanzia saa 10.15 jioni
ambapo itatanguliwa na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu (play off).
Timu zote zilizoingia hatua hiyo
ya nane bora ya michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini
zimefikia hosteli ya Msimbazi.
Wakati huo huo, Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litakuwa na mkutano na waandishi wa
habari. Mkutano huo utafanyika kesho (Januari 26 mwaka huu) saa 5
asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
No comments:
Post a Comment