Wanafunzi wakiwa wanasukuma mashine kwaajili ya kutengeneza kisima cha maji
Picha ya pamoja
Wanafunzi wakiwa katika darasa la vitendo
=======================================================
Shule ya msingi ya kaloleni na
makumbusho iliyopo katika halmashauri ya jiji la Arusha inakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa uzio shuleni hapo hali
inayochangia utoro kwa wanafunzi.
Kutokana na changamoto hiyo
mwenyekiti mpya wa mtaa wa kaloleni Abdul Nassor juzi alikabidhi
matofali 100 kwa mwalimu mkuu wa shule ya kaloleni kwa ajili ya ujenzi
wa uzio utakaotumika pia kwa shule ya msingi ya makumbusho
Mwenyekiti Nassor alisema
aliguswa kuchangia mchango huo kutokana na hali halisi ya shule hiyo
kukosa uzio hali ambayo pia kiusalama kwa wanafunzi wanaosoma hapo kuwa
mdogo
Aliwataka wadau mbalimbali na hata waliowahi kusoma katika shule hizo kujitokeza kuchangia katika ujenzi wa uzio wa shule
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa
shule ya msingi Kaloleni mama Raymond Pudensian akipokea msaada huo
alikiri kuwepo kwa changamoto hiyo ya uzio shuleni hapo hivyo aliwaomba
wadau mbalimbali kujitokeza kuchangia matofali kwaajili ya ujenzi huo.
Bi Pudensiana alitaja makadirio
ya matofali 5000 yanahitajika kwaajili ya uzio wa shule hiyo na kwa
kukamilika kwa uzio huo itasaidia mauzurio mazuri kwa wanafunzi pamoja
na usalama wa kutosha
‘’Kutokana na shule yetu kupakana na mto kwakweli hali ya
kiusalama ni mdogo kwa kuwa hata wanafunzi wanaweza kwenda kujificha
huko ila uzio ukikamilika itakuwa imesaidia kwa kiwango kikubwa”alisema
Pudensiana
(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
No comments:
Post a Comment