Wafanyabiashara
wanaondesha shughuli zao za kibiashara katika masoko zaidi ya matano
yaliyopo Jijini Mbeya, wakiwa nje ya mahakama ya Mwanzo ya Mbeya mjini,
wakishinikiza mahakama hiyo kumuachia huru, Mwenyekiti wa Soko la Soweto
Honola Mbogella ambaye alifikishwa mahakamani hapo na halmashauri ya
jiji la Mbeya kwa tuhuma za kuzuia watumishi wa umma kufanya kazi zao.
MWENYEKITI
wa Soko la Sowetojijini Mbeya, Honola Mbogella, amefikishwakatika
mahakama ya Mwanzo Mbeya mjinikwa tuhuma za kuzuia watumishi wa umma
kufanya kazi zao.
Kufuatia kukamatwa kwaMwenyekiti
huyo kulisababisha zaidi yawafanyabiashara 1000 wanaondesha shughuli
zao za kibiashara katika masokomatano yaliyopo Jijini Mbeya, kuandamana
na kuizunguka mahakama ya Mwanzo yaMbeya mjini, wakishinikiza mahakama
hiyo kumuachia huru.
Mwenyekiti huyo,amefikishwa
katika mahakama ya Mwanzo yaMbeya mjini, leo na kesi yake kusikilizwa
majira ya saa tatu asubuhi ambapo kesi hiyo ilivuta hisia za
watukutokana na kundi hilo la wafanyabiashara kuizunguka mahakama hiyo,
huku jeshila polisi likilazimika kuimarisha ulinzi.
Akisomewa mashitaka hayo Mbele
ya Hakimu wa Mahakama ya mwanzo ya Mbeya MjiniUbaswege Mathew, karani
wa Mahakama hiyo, Sioni Kasunga, alisema mtuhumiwa huyoalifanya kosa
hilo January 10 mwaka huu akiwa katika eneo lake la kazi la Sokola
Soweto lililopo Jijini Mbeya. Alisema, kwa mujibu wa kifungu
kidogocha cha sheria namba 101(a) sura ya 288iliyofanyiwa marekebisho
mwaka 2002, mtuhumiwa aliwazuia watumishi wa umma wahalmashauri ya Jiji
la Mbeya kufanya kazi yao ya kukusanya ushuru.
Alisema, mtuhumiwa
aliwazuiawafanyabiashara hao kugoma kutozwaushuru wa shilingi 200 hadi
300 na halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa maelezokwamba licha ya
wafanyabiashara hao kulipiatozo hiyo kwa kipindi kirefu bado soko hilo
limeendelea kukithiri kwa uchafu.
Aidha, kutokana na kosa
hilo,Hakimu wa mahakama hiyo, Ubaswege Mathew,baada ya kusikiliza
maelezo hayo,alitoanafasi kwa mtuhumiwa ambaye alikana shitaka hilo
hivyo, hakimu kuhairisha kesi hiyo mpaka kesho na kwamba dhamana kwa
mtuhumiwa ipo wazi.
“Kesi hii nimeihairisha mpaka
kesho asubuhi, mtuhumiwa anahaki ya kuwekewadhamana kwa masharti ya
kiasi cha fedha cha shilingi milioni mbili na wadhaminiwawili mmoja
akiwa ni mtumishi wa
serikali,”alisema Wakati kesi hiyo ikiendeleamahakamani hapo,
umati mkubwa wa wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zaokatika masoko
matano ya Soweto,Uyole, Mabatini, Sokomatola na Uhindiniulijitokeza na
kuizunguka mahakama hiyo kwa kile walichokidai kwamba Mwenyekityi huyo
ameonewa.
Wakizungumza naMbeya yetu ,nje ya
mahakama, wafanyabiashara hao ambao waligoma kutaja majina yao,
walisemawao wamegoma kulipa ushuru huo kutokana na halmashauri kushindwa
kuetekelezamajukumu yao ya ukarabati wa miundombinu pamoja na usafi wa
mazingira hivyoMwenyekiti huyo hausiki na suala lakuwashawishi kugoma
kama inavyodaiwa na halmashauri.
Hata hivyo, wafanyabiashara
haowamegoma kuendelea na shughuli zao mpaka suala hilo litakapo patiwa
ufumbuzikwa halmashauri kurekebisha miundombinu na usafi wa mazingira
katika maeneo yabiashara.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment