Na Samia Mussa
WAKATI wakazi wa mikoa kadhaa
hapa nchini wakiomba Tamasha la Pasaka lipite kwenye mikoa yao, baadhi
ya waimbaji wakongwe wa tamasha hilo linalotimiza miaka 15 tangu
kuanzishwa kwake, wametoa mapendekezo yao kwa wandaaji Kampuni ya Msama
Promotions.
Wakizungumza hivi karibuni
wimbaji hao, walianza kwa kuipongeza Kampuni hiyo kufikisha miaka hiyo
bila kutetereka huku wakitoa mapendekezo mbalimbali yatakayoboresha
zaidi matamasha yajayo.
Moja ya mapendekezo hayo ni
pamoja na kutaka kila mwimbaji apate nafasi angalau ya kuimba nyimbo
mbili ukizingatia waimbaji hao wana albamu zaidi ya tatu jambo ambalo
kwao linawapa ugumu kwao pamoja na mashabiki.
Hayo alisemwa na mwimbaji nguli
Upendo Nkone ambapo alisema licha ya kampuni hiyo kujitahidi kufanya
vizuri ikiwa pamoja na kuimba kwa kutumia vyombo hivyo Kamati ya
Maandalizi inatakiwa kubadilisha vitu vichache ikiwemo kupewa dakika za
kuimba kama wanavyofanya nchi zilizoendelea si moja kama ilivyozoeleka.
“Kile ambacho naona kiwekewe
mkazo tunaposema tutaimba’live basi tufanye live kweli na mazoezi
yaanze mapema wiki mbili kabla ili mwimbaji afanyie mazoezi nyimbo
atakazoimba halafu tunaomba kila mwimbaji angalau aimbe nyimbo mbili,
lakini utakuta unaimba nyimbo moja tu kama mimi nina albamu nne nina
nyimbo nyingi ambazo watu wanazipenda unapoimba nyimbo moja, watu
wanakuwa hawajatosheka kwa sababu wamelipa kiingilio,” na kuongeza.
“Idadi ya nyimbo ingozeke,
wenzetu nchi nyingine wanatoa dakika 20-30 kwa kila muimbaji kwa hiyo
unangalia nyimbo zenye dakika kati ya 5-7 unachanganya kwa hiyo nusu
saa unaweza ukaimba nyimbo mbili au tatu,” alisema Nkone.
Nkone pia alitoa pendekezo
kupata wajuzi wa muziki ili nyimbo hizo zipigwe kama zilivyo huku
akitolea mfano kuwa yeye nyimbo zake zinatengenezwa na wenye upeo wa
muziki hivyo lazima zipigwe vile ninavyotengenezewa kwenye CD yake,
kwenye ‘live’ kuna vitu vinapungua hivyo awawekee wajuzi wa hali ya juu.
Alisema kuwa sababu nyingine
itakayofanikisha maendeleo zaidi katika Tamasha hilo la 15 itafanya
Msama Promotions iwe katika kiwango cha juu kwa sababu inabeba waimbaji
vingunge waimbaji wazito ni kuanza mazoezi mapema na kwa taratibu
zilizopangwa, kupatiwa ratiba ya kila muimbaji ajitambue cha kufanya
kabla ya kupanda jukwaani.
Upendo Kilahiro anaipongeza
Msama kwa kutimiza 15 tangu imeanza kuandaa tamasha hilo kubwa hapa
nchini, huku akiiomba kampuni hiyo kubwa kumiliki vyombo vyake ambavyo
vitatumika katika matamasha yake.
“Naomba Mungu Msama ingepata
vyombo vyake kwa sababu ni kampuni ya muda mrefu na muda huu wote
tunakodisha, ingepata vyombo katika ule ubora wake tunaohitaji
tukivimiliki wenyewe tutajua muda gani tutavifunga na injinia wenu
atakaa sawa avirekebishe kwa hiyo hadi tamasha linanza hakuna
ucheleweshaji”.
“Kwa sababu vifaa vitakuwa
vimekaa vizuri na kwa kuwa ni vyenu mnakuwa mnavijua na mtakuwa mnajua
udhaifu mmepiga hatua kubwa, miaka 15 mmeweza kumiliki vyombo vyenu
ambavyo vikafaa uwanja wa wazi na ndani itakuwa ni hatua moja na
tutawakilisha vizuri kazi zetu mara nyingi sauti zimekuwa
zikituchelewesha kuanza,” alisema Kilahiro.
Mwimbaji huyo alisema kuwa
endapo vyombo vitapatikana Saundi ikiwa nzuri mwimbaji yeyote atafurahi
na kazi yake itaonekana na hata watu watafurahi.
No comments:
Post a Comment