Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi
Tanzania, Meja Jenerali GS Milanzi(kushoto) akisalimiana na baadhi ya
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza walipofanya ziara ya mafunzo
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo Januari 27, 2015(wa pili kushoto)
ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi
Tanzania, Meja Jenerali GS Milanzi (kushoto) akisaini katika kitabu cha
wageni mapema leo alipowasili Makao Makuu ya Jeshi la Magereza kwenye
ziara ya mafunzo kuhusu uendeshaji wa Jeshi la Magereza(kulia) ni
Kamishna wa Magereza, Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji
wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiwasilisha mada yake ya uchokozi kuhusu
Historia na Muundo wa Jeshi la Magereza mbele ya Wakufunzi na Wanafunzi
Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (hawapo pichani)
Wakufunzi kutoka Chuo cha Taifa
cha Ulinzi Tanzania wakifuatilia mijadala katika uwasilishaji wa mada
kuhusu Mafanikio na Changamoto katika uendeshaji wa Jeshi la Magereza
katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga Dar es Salaam.
Kamishna wa Magereza, Huduma za
Urekebishaji, Deonice Chamulesile (katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na Maafisa Wakufunzi na Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa
cha Ulinzi Tanzania walipofanya ziara ya mafunzO(wa pili kushoto) ni
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali GS Milanzi(wa
kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt.
Juma Malewa(wa pili kulia) ni Bregedia Jenerali Sylivester Minja.
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)
No comments:
Post a Comment