Ujumbe
wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu wakikagua eneo
lililotengwa kwa ajili ya NHC kujenga nyumba za gharama nafuukatika
Halmashauri ya Wilaya Serengeti-Mugumu. Eneo hili lina ekari 134 na
miundombinu ya maji na umeme.
Afisa
Mipango Miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mugumu Serengeti akimuonyesha
Mkurugenzi Mkuu wa NHC ramani ya mpango Miji inayoonyesha eneo la NHC la
kujenga nyumba za gharama nafuu.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akiongea na kikundi cha vijana
Wilayani Serengeti waliyosaidiwa mashine na NHC kwa ajili ya kujiajiri
kupitia utengenezaji wa matofali yanayofungamana
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake wakikagua jingo
la biashara lililojengwa na NHC eneo la Mukendo Musoma.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akitoa maelekezo ya matumizi
bora ya dari la jengo la biashara la Mukendo lililojengwa na NHC katika
Manispaa ya Musoma ili kuongeza mapato ya Shirika.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akikagua ujenzi wa nyumba za
gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Buhare Musoma. Jumla ya nyumba
50 zinatarajiwa kukamilika Julai 2015.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akijadili namna ya kuongeza
ubora wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC katika maeneo
mbalimbali nchini. Amesisitiza kupunguza gharama ya ujenzi ili nyumba
zinazojengwa ziwe nafuu.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake walipotembelea
Wilayani Tarime kujionea nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC
mwaka 1968 na ambazo hadi hivi sasa zinasaidia familia mbalimbali.
Nyumba hizi ni za vyumba viwili na zilipewa Halmashauri hiyo mwaka 1991.
Ujumbe
wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukiwa eneo la
Isibania nchini Kenya kujionea namna nchi hiyo ilivyopanga eneo lao la
mpakani.
Ujumbe
wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukiwa eneo la
Sirari kuona eneo la kujenga nyumba ili kuboresha taswira ya mpaka wa
nchi yetu. Ujumbuliongozwa na Maafisa Ardhi wa Wilaya ya Tarime.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake pamoja naongozi
wa Wilaya ya Butiama wakikagua eneo lililotengwa na Wilaya hiyo ili NHC
ijenge nyumba za gharama nafuu. Bw. Mchechu amesisitiza kuwa NHC
itajenga nyumba katika Wilaya hiyo ili kuenzi mchango wa Mwalimu Nyerere
wa kulianzisha Shirika la Nyumba la kwanza nchini Tanzania mwaka mmoja
tu baada ya uhuru.
Ujumbe
wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukiangalia mnara
wa kumbukumbu ya mahali ambapo ilikuwepo nyumba aliyozaliwa Baba wa
Taifa.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu aliwa amekaa sehemu maarufu
aliyokuwa akikaa Mwalimu Nyerere wakati wa kucheza bao.
Hapa
ndipo alipozikwa Hayati Mwalimu Nyerere. Ujumbe wa NHC ulizuru
makumbusho ya Mwalimu kama sehemu ya kuenzi mchango wake wa kulianzisha
Shirika la Nyumba mwaka mmoja tu baada ya uhuru wa Tanganyika.
Picha
ya pamoja ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na
kikundi cha vijana cha Samaritans Association cha Wilaya ya Bunda
kilichofadhiliwa na NHC mashine za kutengeneza matofali Bw.
Yoramu Salum ambaye ni Afisa Mipango Miji katika Halmashauri ya Busega
akionyesha ujumbe wa NHC eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa
nyumba.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akiwa katika picha ya pamoja na
mojawapo ya kikundi cha vijana kilichofadhiliwa na NHC mashine za
kufyatua tofali ili kukuza ajira Wilayani Magu
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akipokea risala aliyosomewa na
kikundi cha vijana Wilayani Magu. Anayekabidhi vijana hao fedha
zilizotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa NHC ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya
hiyo Mwalimu Naomi Nnko.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Magu Bibi Naomi Nnko wakikagua ramani inayoonyesha
viwanja vya NHC vya kujenga nyumba za gharama nafuu.
No comments:
Post a Comment