TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, September 26, 2014

VYOMBO VYA HABARI VYATAKIWA KUJENGA MAADILI KUANZIA NGAZI YA FAMILIA ILI KULETA MAENDELEO NCHINI.

 
 
Vyombo vya habari vyatakiwa kujenga maadili
Suleiman Msuya
RAI imetolewa kwa vyombo vya habari, taasis mbalimbali, vikundi vya kijamii, wananchi na serikali kushirikiana kwa pamoja katika kujenga jamii yenye maadili kuanzia ngazi ya familia ili kuleta maendeleo katika nchi.
Hayo yamebainishwa na Afisa kutoka IQ Management Solutions Joel Nanamka wa wakati akizungumza na gazeti hili jana jiji Dar es Salaam.
Alisema iwapo kutakuwepo kwa ushirikiano baina ya sekta hizo ni wazi kuwa jamii itazingatia maadili katika suala lolote ambalo linafanyika kwa maslahi ya Taifa.
Nanamka alisema vyombo vya habari kama moja ya muhimili usio rasmi bado havijafanya kazi ya dhati ili kuweza kuibadilisha jamii ambayo inaonyesha dhahiri kupotea katika misingi ya utu.
Afisa huyo alisema ukosefu wa maadili hasa katika sekta mbalimbali za serikali kumekuwa kukichangia ukosefu wa huduma bora na zenye viwango kwa jamii.
“Kimsingi suala la kuwepo kwamaadili ni mtambuka ila kwa mtazamo wetu katika tafiti mbalimbali tunaona kuwa nafasi ya vyombo vya habari katika kufanikisha hilo ni kubwa hivyo vinapaswa kubadilika kutokana na ukweli kuwa watu wengi wanafikiwa”, alisema.
Alisema IQ Management Solutions imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali za kuhakikisha kuwa maadili yanakuwepo kwa kanuni, sheria, zawadi na matisha pamoja na adhabu ambazo zitakuwa katika mtazamo hasi.
Kwa upande wake Afisa Programu kutoka taasisi ya Afrika Leadership Initiative Foundation Limited Alice Mwiru alisema katika kuhakikisha kuwa kunakuwepo kwa jamii yenye maadili taasisi yao imejikita kufanya kazi na vijana ambao wanaonyesha nia za kuongoza.
Mwiru alisema wao wanaamini kuwa kuwepo kwa viongozi wenye maadili ni chachu ya kuwepo kwa jamii ambayo itakuwa katika misingi hiyo.
“Sisi ALI EAF tunaamini kuwa jamii ikikuwa kwa misingi ya maadili hasa kuanzia utotoni  ni wazi kuwa kila Mtanzania atakuwa kwenye misingi hiyo kwa faida yake na nchi kwa ujumla”, alisema

KUTOKUWEPO KWA UWAZI,UADILIFU NA UWAJIBIKAJI KATAKA MIKATABA.

Ukosefu wa Uwazi ni Chanzo cha Rushwa
Kipimo Abdallah
KUTOKUWEPO kwa uwazi, uadilifu na uwajibikaji katika mikataba mbalimbali ambayo serikali inaingia na wawakezaji kutoka nje ni moja ya sababu ya kuongezeka kwa rushwa kwa baadhi ya watumishi wa umma na wawekezaji.
Hayo yamebainishwa na Mwahadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Uchumi Profesa Humphrey Moshi wakati akizungumza na mwandishi habari hii kwenye kongamano ambalo linaratibiwa na taasisi ya Jukwaa la Sera (Policy Forum).
Alisema kukosekana kwa  uwazi katika  mikataba mbalimbali ni moja ya sababu ambayo imekuwa ichangia rushwa kwenye michakato na makubaliano mengi ambayo yanahusisha serikali na wawakezaji.
Profesa Mushi alisema Serikali imekuwa inapata kigugumizi katika kuweka wazi baadhi ya mikataba kwa kile kinachodaiwa kuwa ni siri baina ya mwekezaji na serikali jambo ambalo halina ukweli tofauti na rushwa.
“Mimi nimekuwa nikifanya tafiti mbalimbali hasa za mausuala ya kukua kwa uchumi ni wazi kuwa zipo fedha nyingi ambazo zinapotea ambapo mwanzo wake unaanzia kwenye uingia ji wa mikataba hadi katika utekelezaji  ambazo zinaelekezwa katika rushwa”, alisema Mushi.
Mwahadhiri huyo wa UDSM alisema kuonyesha kuwa serikali haina dhamira ya kuondoa hiyo changamoto imekuwa ikiwaruhusu wawekezaji hao kutoweka hata akaunti zao wazi kama ilivyo kwa nchi zingine duniani.
Profesa Mushi ambaye pia aliwahi kuwa mshauri wa masauala ya uchimi wa Rais wa Zanzibar Abeid Aman Karume pamoja na Ofisi ya Hazina ya Tanzania alisema iwapo Tanzania itajikita katika uwazi, uwajibikaji na uadilifu maendeleo yatapatikana kwa haraka.
Mchumi huyo mwandamizi alisema ni dhahiri kuwa kumekuwepo kwa ukiukwaji mkubwa katika maamuzi hivyo ni vema kujiangalia upya kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya kwa maslahi ya Taifa.
Alisema Tanzania ni nchi ambayo imebarikiwa fursa mbalimbali ila kukosekana kwa uadilifu na uwazi kwa baadhi ya watendaji rasilmali hizo zipo hatarini kupotea.

TCAA YATUMIA ZAIDI YA MILIONI 200 KUFANYA MABORESHO YA MAWASILIANO.

bestina-aug17-2013TCAA yatumia zaidi ya Milioni 200 kufanya maboresho ya mawasiliano Mnyusi Tanga
Kipimo Abdallah
ZAIDI ya shilingi milioni 200 zimetumika katika maboresho ya kituo cha mawasiliano cha Mnyusi mkoani Tanga kinachotumika kupokea na kutuma mawasiliano ya radio zinazo tumika katika usafiri wa anga.
Hayo yamebainishwa na Afisa habari wa TCAA  Bestina Magutu wakati akizungumza na mwandishi wahabari hii leo jijini Dar es Salaam.
Alisema maboresho hayo yametokana na ukweli kuwa kituo hicho kilikuwa hakifanyi kazi kwa muda mrefu hali ambayo ilikuwa inaasababisha kukosekana kwa mawasiliano katika ukanda wa mashariki kutoka usawa wa bahari.
Kabla ya kukamilika kwa maboresho haya baadhi ya maeneo mchini yalikuwa hayapati mawasiliano ya kitekonologia kutoka nchini na badala yake walikuwa wanapata huduma hiyo kutoka nchi jirani,”alisema.
“Mradi huo umekamilika na kukabithiwa kwenye mamlaka ya usafiri wa anga mwezi agost mwaka huu na kukabithiwa kwenye kituo cha Mnyusi jijini Tanga,umegharimu shilingi za kitanzania milioni 292,887,921,” alisma.
Magutu aliongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo kumeongeza ufanisi wa usafirishaji wa anga kwa kurahisisha huduma ya kuongoza ndege,utaongeza mapato kwa mamlaka hiyo.
“Nimategemeo yangu kwamba kupitia maboresho haya mamlaka itajiongezea mapato kupitia tozo ya huduma ya uongozaji ndege,
Kwa upande wake Mkaguzi Mwandamizi,Redemptus Rugombe alisema mamlaka inandelea kupanua miondombinu ya kuongeza ndege sanjari na mabadiliko ya teknolojia ili kumudu ukuaji wa sekta ya usafirirshaji wa anga.
“Takwimu za mwaka 2031 zinaonyesha ongezeko la miruko ya ndege (flight movement) imeongezeka hadi kufikia miruko 230,458 sawa na ongezeko la asilimia3.6 kotoka miruko 222,430 mwaka 2012,
Kadharika katika kipindi hicho idadi ya abilia imeongezeka kutoka 4,056,925 hadi kufikia 4,626,016 sawa na ongezekola asilimia 14,kwa sasa idadi ya abilia inatarajiwa kuongezeka zaidi kufikia mwishoni mwa mwaka huu,” alifafanua.
Mkaguzi Mwandamizi huyo aliongeza kuwa katika kuhakikisha watanzania wanapata uelewa wa elimu ya mamlaka ya anga mamlaka inaendelea kuwapatia wanafunzi mafunzo kwa njia ya udhamini na hadi sasa kuna wamnafunzi watano wanaendelea ma mafunzo ya urubani.
“Kwa tarifa za wanafunzi wetu ambao wako Afrika ya kusini kwa masomo ya urubani chini ya udhamini wa mamlaka wanaendelea vizuri,huu mpango kwa mamlaka ni endelevu ili kusaidia kuwawezesha watanzania kpambana katika soko la ajira, “alisema.

CHAMA CHA NCCR MAGEUZI YALIA NA WABUNGE WA BUNGE LA KATIBA.

ssNCCR yalia na Wabunge wa Bunge la Katiba
Kipimo Abdallah
CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimesikitishwa na kitendo cha Bunge Maalum la Katiba kuhitaji wajumbe ambao hawapo nchini au ndani ya Bunge kuruhusiwa kupiga kura wakati ukweli ni kwamba ushiriki wao katika utengenezaji wa rasimu hiyo ulikuwa mdogo.
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi Faustin Sungura wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii jana jijini Dar es Salaam kwa njia ya simu.
Alisema utaratibu huo wa kuruhusu wajumbe walioko nje kupiga kura haujawahi kutokea katika Bunge lolote hapa duniani jambo ambalo linatia aibu kwa Taifa.
Kaimu Katibu huyo alisema iwapo wajumbe hao ambao hawakushiriki katika mchakato kwa kiwango cha kuridhisha wataruhusiwa kupiga kura hali hiyo ingekuwa hata kwa wale wa UKAWA kwani uwepo wao nje una sababu kama hao wengine.
“Jamani Watanzania tuamke hii sasa aibu tunapopelekwa pabaya haiwezekani watu wapo nje ya Bunge alafu wapewe nafasi ya  kupiga kura jambo ambalo haliwezi kuvumiliwa kwani linatia aibu nchi”, alisema.
Alisema katika Bunge hilo linaloendelea mkoani Dodoma mambo mengi yamekiukwa ila hapo walipofikia ni vema jamii ya Kitanzania ikafungua macho na kuamua kufanya maamuzi mazito kwani kinachoonekana ni watu kuhitaji kwa maslahi yao.
Sungura alisema ni vema Wabunge waliopo Dodoma wakatambua kuwa mambo megine hayalazimishwi kwani yanahusu jamii kubwa na sio kama wanavyofikiria kuwa wao ndio wanahusika pekee.
Alisema NCCR-Mageuzi imejipanaga kuhakikisha kuwa katiba hiyo inakataliwa kutokana na ukweli kuwa kilichopo ndani sio yaliyokuwa mapendekezo ya wananchi ambayo yaliwakilishwa na iliyokuwa Tume ya Katiba.
Sungura alisema ukweli dhidi ya UKAWA kutoka Bungeni umedhihirika hivyo juhudi zao ni kuhakikisha kuwa rasimu hiyo haipitishwi na wananchi kutokana na kudharauliwa kwa maoni yao ambayo walipendekeza katika rasimu ya Jaji Joseph Warioba.
 Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema nguvu yao pia inaongezwa na maamuzi ya Mahakama Kuu hivi karibuni ambapo imeweka bayana kuwa kitendo kilichofanywa na Mwenyekiti wa Bunge hilo kupokea maoni mapya ni ukiukwaji wa sheria.
Sungura alisema mabadiliko na maingizo mapya yaliyofanywa na Bunge hilo ambalo alilitaja kuwa ni la upande mmoja yamekiuka sheria kwa kiwango kikubwa na cha kusikitisha.
Alisema kwa sasa NCCR- Mageuzi ipo katika mikakati ya kuhakikisha wananchi wanapata elimu sahihi juu ya mchezo mchafu unaofanywa na Bunge hilo jambo ambalo litawajengea uwezo wa kufanya maamuzi sahihi katika upigaji kura.

EVELYN BAASA NDIYE REDD’S MISS TANZANIA PHOTOGENIC 2014.

 
Miss Tanzania Photogenic 2014, Evelyn Baasa.
 Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya
Redd’s Miss Tanzania Photogenic 2014, wakiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa taji hilo, Evelyn Baasa (katiakti) jana. Wengine kutoka kushoto ni Nicole Sarakikya, Lilian Kamazima, Lilian Timothy na Dorice Mollel.
 Warembo wakilisakata rumba kabla ya kuatangzwa kwa matokeo hayo.
 Baadhi ya warembo wakipiga picha ya pamoja na mshindi huyo wa Taji la Miss Tanzania Photogenic 2014
MlimbwendeEvelyn Baasa (19) jana aliibuka kidedea kati ya walimbwende wenzake 30 na kutwaa taji la Redds Miss Photogenic 2014.
Kwa kushinda taji hilo Baasa ambaye alinzania mbio za taji la Miss Tanzania katika Kitongoji cha Karatu naabadae kuingia Miss Arusha na Kanda ya Kaskazini amekuwa mrembo wa kwanza kuingia Nusu Fainali ya mashindano Miss Tanzania 2014.
Shindano hilo ni moja kati ya mataji matano ambayo yanashindaniwa na warembo hao ambapo washindi wake wanapata tiketi ya kuingia Nusu Fainali ya shindano hilo litakalo fanyika mapema mwezi ujao.
Miongoni mwa mataji hayo ni Miss Tanzania Photogenic, Miss Tanzania Top Model, Miss Tanzania Personality, Miss Tanzania Sports Lady na Miss Tanzania Talent.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Lino International Agency, waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga ‘Uncle’ amesema jopo la majaji watatu ambao ni wapiga picha na wadau wa masuala ya urembo  wa masuala ya urembo Tanzania walikaa na kumchagua mshindi huyo kupitia picha mbalimbali za warembo hao.
Majaji waliowezesha kupatikana kwa mshindi huyo ni Mpigapicha mkongwe wa masuala ya
urembo nchini Mroki Mroki ambaye anafanyakazi na Magazeti ya Serikali ya Daily
News na Habarileo, Mtayarishaji wa vipindi Elliud Pemba wa True Vision na Afisa
Itifaki Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha, Mukhsin Kassim.
Taji la
Redd’s Miss Tanzania Photogenic lilikuwa linashikiliwa na Redd’s Miss Tanzania
2013 Happyness Watimanywa.
Warembo wengine
waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya Miss Photogenic ni Dorice Mollel, Nicole
Sarakikya, Lilian Timothy na Lilian Kamazima.
Kesho warembo hao watachuana tena kuwania taji la Miss Top Model katika shindano
litakalofanyika Triple A jijini Arusha.

UJUMBE WA CHUO CHA WATAALAMU WA MAGONJWA CHA NCHI ZA MASHARIKI,KATI NA KUSINI MWA AFRIKA IKULU MJINI ZANZIBAR.

IMG_7103Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Prof. Ephata Kaaya (kulia) akiongoza Ujumbe wa Chuo cha Wataalamu wa Magonjwa cha Nchi za Mashariki,kati na Kusini mwa Afrika ulipofika Ikulu mjini Zanzibar kwa mazungumzo na Rais leo. [Picha na  Ramadhan Othman,Ikulu.] IMG_7125Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Chuo cha Wataalamu wa Magonjwa cha Nchi za Mashariki,kati na Kusini mwa Afrika unaoongozwa na Prof. Ephata Kaaya, (wa pili kulia)katika ukumbi Ikulu Mjini Zanzibar leo, [Picha na  Ramadhan Othman,Ikulu.] IMG_7130Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipokea Shahada ya Heshima kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Wataalamu wa Magonjwa cha Nchi za Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika Prof. Ephata Kaaya,  aliyotunukiwa na chuo hicho kumtambua kuwa yeye ni mwanataaluma wa fani hiyo na pia  katika kukuza na kuimarisha fani hiyo katika Ukanda huu wa Afrika. [Picha na  Ramadhan Othman,Ikulu.]

AFRICA;WINNERS OF MEDIA AWARDS ELECTRICAL COUNTERFEITING IN AFRICA RECEIVE AWARDS IN FRANCE.

vvvvvvvvvv 
PRESS RELEASE
Winners of Media Awards on Electrical Counterfeiting in Africa Receive Awards in France
 A special ceremony held in Grenoble (France) in the presence of Mrs Tracy Garner, Global Anti-counterfeiting Manager at Schneider Electric
 PARIS, France,September 26, 2014/ — Winners of the first Media Awards on Electrical Counterfeiting in Africa on Thursday received their awards during a special ceremony held in Grenoble (France) in the presence of Mrs Tracy Garner, Global Anti-counterfeiting Manager at Schneider Electric (http://www.schneider-electric.com).
zzzzzzzzzz 
 Photo2: http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=1403 (Adedeji Ademigbuji, senior correspondent at The Nation newspaper (Nigeria) and Tracy Garner, Global Anti-counterfeiting Manager at Schneider Electric)
 Photo 3: http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=1404 (Birame Faye, reporter at Le Quotidien newspaper in Senegal and Tracy Garner, Global Anti-counterfeiting Manager at Schneider Electric)
 The Media Awards on Electrical Counterfeiting in Africa was established by Schneider Electric (http://www.schneider-electric.com), the global specialist in energy management. It recognises African journalists who publish or broadcast outstanding investigative reports on issues relating to electrical counterfeiting in Africa.
 The first Media Awards on Electrical Counterfeiting in Africa was won by Adedeji Ademigbuji, senior correspondent at The Nation newspaper (Nigeria), for his piece entitled “Checking the menace of fake electrical products” and by Birame Faye, reporter at Le Quotidien newspaper in Senegal, for his piece entitled “Electricité – Usage des produits contrefaits : De l’insécurité dans notre confort domestique”.
 “Schneider Electric is extremely proud to award the very first Media Awards on Electrical Counterfeiting in Africa. I would like to express my warmest congratulations to these two very talented journalists,” said Tracy Garner, Global Anti-counterfeiting Manager at Schneider Electric.
 Adedeji Ademigbuji started his journalism career in 2001 as an intern after completing a National Diploma Programme from The Polytechnic, Ibadan, Oyo State (Nigeria).
 In 2006, Adedeji joined the National Standard news magazine. Later that year, he left the National Standard as a senior correspondent to work as a freelance writer for The Sun newspaper. In 2011, Adedeji joined the National Mirror as a business correspondent. After winning the 2013 Social Enterprise Reporting Award (SERA) in the CSR category and the Nigerian Media Merit Awards (NMMA) Coca-Cola Prize in the Brands & Marketing category, setting records in the Newspaper Reporter of the Year and Telecom Reporter of the Year categories, he was sought out by The Nation newspaper to handle the paper’s Brands & Marketing pages.
 A graduate of the Institute of Science and Information Technology (CESTI) at Cheikh Anta Diop University in Dakar (Senegal), Birame Faye joined Le Quotidien newspaper immediately after completing his studies. Birame specialised in Online Journalism at the Berlin International Institute, before being assigned to his newspaper’s political section. He then took part in two training courses in Economic and Financial Journalism at the Thomson Reuters Foundation. In 2012, he also attended a training course in Investigative Journalism organised by the Panos Institute in West Africa (IPAO). On two occasions, he was awarded the First Prize for Investigative Journalism launched by the IPAO. Birame Faye holds a Master’s degree in Media and Communication, as well as a Master’s degree in Project Management.
 Distributed by APO (African Press Organization) on behalf of Schneider Electric SA.
 Contact:
APO (African Press Organization)
About Schneider Electric
As a global specialist in energy management with operations in more than 100 countries, Schneider Electric (http://www.schneider-electric.com) offers integrated solutions across multiple market segments, including leadership positions in Utilities & Infrastructure, Industries & Machines Manufacturers, Non-residential Building, Data Centres & Networks and Residential. Focused on making energy safe, reliable, efficient, productive and green, the Group’s 140,000 plus employees achieved sales of €24 billion in 2012 through an active commitment to help individuals and organisations make the most of their energy.
 SOURCE
Schneider Electric SA.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
XX
                                                                                                                                                                                                                                                                                                          
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” 
TAREHE                26.09.2014.
  • MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI KWA TUHUMA ZA WIZI WILAYA YA MBOZI.
  • JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA BHANGI JIJINI MBEYA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA MKAZI WA VWAWA MJINI WILAYA YA MBOZI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MWILE LISBON @ MANGEU (25) ALIUAWA KWA KUPIGWA NA KISHA MWILI WAKE KUCHOMWA MOTO NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BAADA YA KUMKAMATA KWA TUHUMA ZA KUVUNJA NA KUIBA KATIKA NYUMBA YA MTU MMOJA AITWAYE BRIGATE SICHALWE, MKAZI WA VWAWA MJINI.
 TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 24.09.2014 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO MAENEO YA FLORIDA VWAWA MJINI, KATA NA TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. AIDHA, TAARIFA ZA AWALI ZINADAI KUWA MAREHEMU ALIKUWA MHALIFU MZOEFU NA ALIKUWA AKISAKWA NA POLISI KWA MUDA MREFU KUTOKANA NA KUTUHUMIWA KWA VITENDO VYA UVUNJAJI NA KUIBA KATIKA MAENEO MBALIMBALI.
 KATIKA CHUMBA ALICHOKUWA AKIISHI MAREHEMU, KUMEPEKULIWA NA KUKUTWA MAGODORO MAWILI YALIYOTAMBULIWA KUWA NI YA WIZI. HAKUNA MTU/WATU WALIOKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA – MBOZI.
 TAARIFA ZA MISAKO:
 JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA CHRISTOPHER GEOFREY (23) MKAZI WA MBALIZI AKIWA NA MISOKOTO MITATU YA BHANGI SAWA NA UZITO WA GRAMU 15 IKIWA KWENYE GANDA LA SIGARA.
 MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 25.09.2014 MAJIRA YA SAA 16:30 JIONI HUKO MAENEO YA MSITU WA KILIMO, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MVUTAJI WA BHANGI HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
 Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA(TCAA) IMEKAMILISHA KITUO CHA KUTUMA NA KUPOKEA MAWASILIANO YA NDEGE.

1Afisa Habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bi. Bestina Magutu akiwaeleza waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu kukamilika kwa maboresho ya kituo cha Mawasiliano ya Radio kwa ajili ya usafiri wa anga kilichopo Mnyusi mkoani Tanga, kilichojengwa na kampuni ya JATRON ya Norway, wakati wa Mkutano Uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mhandisi Mkuu toka Mamlaka Hiyo Bi. Valentine Kayombo.2Mhandishi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bi. Valentine Kayombo akiwaeleza waandishi wa Habari(Hawapo pichani) faida zitakazopatikana kutokana na kukamilika kwa Kituo hicho ikiwamo kuongeza ufanisi wa utoaji huduma za uongozaji ndege, wakati wa Mkutano Uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Afisa Habari wa Mamlaka Hiyo Bi. Bestina Magutu. 3Inspeka Mwandamizi Idara ya Udhibiti Usalama wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Redemptus Bugumula akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu ongezeko la marubani wanawake nchini ambao wanafikia Takribani Kumi kwa sasa wakati wa Mkutano Uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mhandisi Mkuu toka Mamlaka Hiyo Bi.Valentine Kayombo.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imekamilisha mradi wa kuboresha kituo cha kupokea na kutuma mawasiliano ya radio zinazotumika katika usafiri wa anga kilichoko Mnyuzi mkoani Tanga.
Mradi huo uliojengwa na kampuni ya JOTRON ya NORWAY umegharimu Serikali zaidi ya shilingi milioni 200 na ulikabidhiwa rasmi kwa TCAA mapema mwezi Agosti mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bi. Bestina Magutu wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
Magutu alisema kuwa kukamilika kwa kituo hicho kumeongeza ufanisi wa utoaji huduma za uongozaji ndege na kuimarisha zaidi usalama wa safari za anga hapa nchini.
Akifafanua zaidi Magutu amesema hali hiyo itachangia kuongezeka kwa mapato ya Mamlaka hiyo yanayotokana na tozo la huduma za uongozaji ndege.
Akizungumzia mikakati ya Mamlaka hiyo Magutu amesema inaendelea kuwekeza katika miundo mbinu ya kuongozea ndege hivyo kwenda sanjari na mabadiliko ya teknolojia pamoja na kumudu ukuaji wa Sekta ya usafiri wa anga hapa nchini.
Katika hatua nyingine Mamlaka hiyo imesema kuwa wanafunzi watano waliopewa ufadhili wa kusomea urubani nchini Afrika ya Kusini wameendelea kupata ufaulu wa juu na kushika nafasi ya kwanza hadi ya tano katika darasa la watu 14 katika shule ya urubani nchini Afrika ya Kusini.
Takwimu za mwaka 2013 zinaonyesha ongezeko la miruko ya ndege ( flight movements) kutoka 222,430 mwaka 2012 hadi kufikia miruko 230,458 sawa na ongezeko la asilimia 3.6 kadhalika katika kipindi hicho idadi ya abiria imeongezeka kutoka 4,056,925 hadi kufikia 4,626,016 sawa na ongezeko la asilimia 14.Idadi ya abiria inatarajiwa kufika zaidi ya milioni 5 kufikia mwishoni mwa mwaka 2014.

”SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI SEKTA ZA HIFADHI YA JAMII NCHINI”

FSERIKALI inatambua na kuthamini mchango wa sekta ya hifadhi ya jamii nchini hasa katika kusaidia kukuza na kuimarisha uchumi na kuinua hali za watanzania kwa ujumla hasa wale wanaofikiwa na huduma hizo.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Salum Chima wakati akifungua semina ya mfuko wa Pensheni wa PPF kwa maafisa wa makampuni mbalimbali katika (Kanda ya Kinondoni)mkoa wa Tanga.
Amesema kuwa serikali inatambua kuwa huduma ya hifadhi ya jamii inawafikia watu wachache sana licha ya umuhimu wake kwa jamii.
Aidha amesema kuwa kwa kutambua umuhimu huo serikali imekuwa ikiimarisha sekta hiyo ili iwez kupanua wigo wa watu wanaonufaika na huduma hiyo kwa kurekebisha sheria na kuweka mazingira bora kwa watu wote wanaojiunga na mfuko huo.
Alifurahishwa kusikia kuwa mfuko wa Pensheni wa PPF ambayo ilianzishwa mwaka 1978 kwa ajili ya pensheni za mashirika ya umma lakini pia kisheria inaweza kusajili hata makampuni binafsi,taasisi za elimu na vyuo binafsi,taasisi za dini na waliojiajiri wenyewe ikiwemo walioko kwenye sekta isiyo rasmi.
Amesema kuwa hatua hiyo itawafanya watanzania wengi zaidi waweze kupata huduma bora za mfuko wa PPF na kuwa na uhakika ya maisha bora ya sasa nay a baadae kama iliyokuwa kauli mbiu ya PPF.
Kwa upande wake,Meneja wa PPF Kanda ya Kinondoni,Pwani na Tanga,Zahra Kayugwa amesema kuwa watawapeleka mahakamani waajiri wote ambao watakuwa hawawasilishi michango ya wafanyakazi wao kwa wakati.

KAMPUNI YA PLATINUM YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO KWA AJILI YA SHIMIWI.

SH1 Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Platinum Credit Ltd Bw. Elias Samwel akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa vifaa vya michezo kwa baadhi ya Timu za Wizara na Taasisi za Serikali leoj jijini Dar es Salaam, vifaa hivyo vimetolewa ili kusaidia timu hizo zinazoshiriki mashindano ya SHIMIWI ambayo mwaka huu yanatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 27 Septemba hadi tarehe 11 Oktoba mkoani Morogoro.Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa SHIMIWI Moshi Makuka.SH2Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga akimtunuku cheti Mwakilishi wa Platinum Credit Ltd Bw. Ferdinand Kambanyumba ikiwa ni kutambua na kuthamini mchango wao katika kuendeleza michezo wakati wa hafla ya kuwaaga wachezaji wa Wizara watakaoshiriki mashindano ya SHIMIWI 2014
SH3a
SH3Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Concilia Niyibitanga akipokea kwa niaba ya Katibu Mkuu, msaada wa vifaa vya michezo kutoka kwa Meneja Mauzo wa Kampuni ya Platinum Credit Ltd Bw. Ferdinand Kambanyuma wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo kwa baadhi ya timu za Wizara na Taasisi za Serikali zinazotarajia kushiriki mashindano ya SHIMIWI leo jijini Dar es Salaam.Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza rasmi kuanzia tarehe 27 mwezi huu na kumalizika tarehe 11 Oktoba mkoani Morogoro.SH4Kaimu Katibu Mkuu wa SHIMIWI Bw. Moshi Makuka (kulia) akipokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Platinum Credit Ltd Bw. Elias Samwel wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo kwa baadhi ya timu za Wizara na Taasisi za Serikali zinazotarajia kushiriki mashindano ya SHIMIWI leo jijini Dar es Salaam.Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza rasmi kuanzia tarehe 27 mwezi huu na kumalizika tarehe 11 Oktoba mkoani Morogoro.SH5Mwenyekiti Timu ya Utumishi Bw. Lumuli Mtaki (kushoto) akipokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Platinum Credit Ltd Bw. Elias Samwel wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo kwa baadhi ya timu za Wizara na Taasisi za Serikali zinazotarajia kushiriki mashindano ya SHIMIWI leo jijini Dar es Salaam.Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza rasmi kuanzia tarehe 27 mwezi huu na kumalizika tarehe 11 Oktoba mkoani Morogoro.

SHUHUDA ALBINO ATAKA WAUAJI WANYONGWE HADHARANI.

DSC_0519Shuhuda aliyenusurika kwenye mauaji ya Albino ambaye amekatwa mikono yote miwili, Mariam Stanford akitoa ushuhuda wake na killio chake mbele ya meza na wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mnazi mmoja.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
Na Mwandishi wetu
Mwanamke albino Mariam Stanford aliyepoteza mikono yake yote miwili wakati iliponyofolewa na majahili asiowajua Oktona7, 2008 ameitaka serikali kuwanyonga wote wanaopatikana na hatia ya kuua albino nchini.
Alisema hata adhabu ya kifungo cha maisha haiwatoshi kwa jinsi wanavyosababisha maisha ya mashaka na yenye uchungu kwa walemavu wa ngozi.
Akiongea kwa uchungu huku hapa na pale akitulia kwa kuzidiwa na machozi kiasi cha kushidwa kuzungumza Stanford ambaye alisema wakati akikatwa mikono yake alikuwa na mimba ya miezi mitano na ambayo ilitoka alisema majahili hao si wa kusamehewa.
Alisema akiwa mama wa familia kitendo cha kumuondolea mikono yake kimemfanya kuwa tegemezi hali ambayo inaongeza maumivu juu ya maumivu ambayo anayo ya kunyanyapaliwa na jamii.
Alisema hayo wakati akitoa ushuhuda katika adhimisho la siku ya amani duniani iliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Alisema japokuwa Tanzania inaelezwa kuwa nchi ya amani wananchi wake wenye ulemavu wa albino hawana amani kutokana na kuwindwa kama digidigi. Alisema kwa sasa Tanzania ni kisiwa cha matatzio kwa kundi hilo ambalo sasa linajificha na wala kutokujua kesho ikoje au siku hiyo ikoje.
DSC_0534Mke wa Balozi wa Uturuki nchini Yesim Davutoglu, akilia kwa uchungu baada ya kusikia shuhuda kutoka kwa mhanga wa mauaji ya Albino aliyekatwa mikono yote miwili, Mariam Stanford (hayupo pichani) ambaye hadi sasa anapewa matunzo na Shirika la Under The Same Sun.
Alisema ni vyema jamii ikawatazama na kuwasaidia kwa kuhakikisha kwamba wanasaidia kuwafichua watenda maovu hao hasa ikizingatiwa kwamba watu wenye albinizimu ni watu na watu kama watu wengine na hawawezi kuwa chanzo cha utajiri kwa binadamu wenzao.
Alisema anatamani kuona waliotiwa hatiani wakiuuawa hadharani au hata watu hao nao kukatwa viungo vyao ili watambue jinsi isivyofaa kuwafanyia binadamu wenzao matendo hayo.
Alishukuru taasisi ya Under the Same Sun kwa kumsaidia toka aliponyofolewa mikono mpaka leo na kuhimiza serikali kuona namna ya kuwasaidia waliokatwa viungo vyao ili waweze kusihi maisha ya kawaida.
DSC_05401Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema akimfariji mke wa Balozi wa Uturuki nchini Yesim Davutoglu, wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja hivi karibuni jijini Dar.
Pamoja na kuomba watu hao wanyongwe Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali George Masaju aliitaka jamii kutambua kwamba sheria ya kuua anayeua ipo lakini inakabiliwa na mashindano na wanaharakati huku watoa ushahidi wakishindwa kuisaidia mahakama kufikia maamuzi katika kesi za maalbino.
Alisema ni wajibu wa wananchi kusimamia amani kwa kuhakikisha wanaisaidia serikali kutekeleza wajibu wake.
DSC_0384Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mh. Ali Davutoglu akisoma ujumbe kwa niaba wa umoja wa mabalozi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani duniani.
Naye Balozi wa Uturuki nchini alisema kwamba Ali Davutoglu amesema kwamba ujenzi wa kituo cha maalbino Bagamoyo utaanza hivi karibuni ili kuwapatia nafasi wananchi hao kuwa katika hali ya kawaida.
Kituo hicho ambacho kitakuwa na uwezo wa kuchukua watu 500 na kuwa chemchem ya maarifa kwa watu wenye albinizimu.
Katika adhimisho hilo watoto wenye albuinizim walitoa shoo ya nguvu iliyowafanya watu mbalimbali kujimwayamwaya katika eneo la wazi na kutoa zawadi kwa vijana hao.
Aidha bendi ya vijana ilitumbuiza na kwaya ilikuwepo kutoa ushaiwishi wa kuelewa umuhimu wa amani huku wazungumzaji wengine wakitaka wanasiasa kuhudhura maadhimisho hayo na kupeleka ujumbe kwa wananchi ambao wanawasikiliza.
Katika adhimisho hilo wanasiasa waliokuwepo ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa dar es salaam, Madabida, Kaimu katibu Mkuu NCCR-Mageuzi Faustin Sungura na Naibu katibu mkuu CUF Magdalena Hamis Sakaya ambaye pia ni mbunge wa viti maalumu Tabora.
DSC_0575Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali, George Masaju, akizungumza kwenye maadhimisho hayo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar.
DSC_00521Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh. Seif Rashid (wa pili kushoto), Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia), Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Joseph Masasi, kwenye picha ya pamoja na binti mhanga wa mauaji ya Albino aliyekatwa mikono yote miwili, Mariam Stanford (kushoto).