Afisa
Habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bi. Bestina Magutu
akiwaeleza waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu kukamilika kwa
maboresho ya kituo cha Mawasiliano ya Radio kwa ajili ya usafiri wa anga
kilichopo Mnyusi mkoani Tanga, kilichojengwa na kampuni ya JATRON ya
Norway, wakati wa Mkutano Uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mhandisi Mkuu toka Mamlaka
Hiyo Bi. Valentine Kayombo.Mhandishi
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bi. Valentine
Kayombo akiwaeleza waandishi wa Habari(Hawapo pichani) faida
zitakazopatikana kutokana na kukamilika kwa Kituo hicho ikiwamo kuongeza
ufanisi wa utoaji huduma za uongozaji ndege, wakati wa Mkutano
Uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es
Salaam.Kulia ni Afisa Habari wa Mamlaka Hiyo Bi. Bestina Magutu. Inspeka
Mwandamizi Idara ya Udhibiti Usalama wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga
Tanzania (TCAA) Bw. Redemptus Bugumula akiwaeleza waandishi wa habari
kuhusu ongezeko la marubani wanawake nchini ambao wanafikia Takribani
Kumi kwa sasa wakati wa Mkutano Uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya
Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mhandisi Mkuu toka
Mamlaka Hiyo Bi.Valentine Kayombo.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga
Tanzania (TCAA) imekamilisha mradi wa kuboresha kituo cha kupokea na
kutuma mawasiliano ya radio zinazotumika katika usafiri wa anga
kilichoko Mnyuzi mkoani Tanga.
Mradi huo uliojengwa na kampuni ya
JOTRON ya NORWAY umegharimu Serikali zaidi ya shilingi milioni 200 na
ulikabidhiwa rasmi kwa TCAA mapema mwezi Agosti mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bi. Bestina Magutu wakati wa
mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
Magutu alisema kuwa kukamilika kwa
kituo hicho kumeongeza ufanisi wa utoaji huduma za uongozaji ndege na
kuimarisha zaidi usalama wa safari za anga hapa nchini.
Akifafanua zaidi Magutu amesema
hali hiyo itachangia kuongezeka kwa mapato ya Mamlaka hiyo yanayotokana
na tozo la huduma za uongozaji ndege.
Akizungumzia mikakati ya Mamlaka
hiyo Magutu amesema inaendelea kuwekeza katika miundo mbinu ya kuongozea
ndege hivyo kwenda sanjari na mabadiliko ya teknolojia pamoja na kumudu
ukuaji wa Sekta ya usafiri wa anga hapa nchini.
Katika hatua nyingine Mamlaka hiyo
imesema kuwa wanafunzi watano waliopewa ufadhili wa kusomea urubani
nchini Afrika ya Kusini wameendelea kupata ufaulu wa juu na kushika
nafasi ya kwanza hadi ya tano katika darasa la watu 14 katika shule ya
urubani nchini Afrika ya Kusini.
Takwimu za mwaka 2013 zinaonyesha
ongezeko la miruko ya ndege ( flight movements) kutoka 222,430 mwaka
2012 hadi kufikia miruko 230,458 sawa na ongezeko la asilimia 3.6
kadhalika katika kipindi hicho idadi ya abiria imeongezeka kutoka
4,056,925 hadi kufikia 4,626,016 sawa na ongezeko la asilimia 14.Idadi
ya abiria inatarajiwa kufika zaidi ya milioni 5 kufikia mwishoni mwa
mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment