.Mwenyekiti
wa Halmashauri ya wilaya ya.Mpanda Yasini Kibiriti akifungua kikao cha
Baraza la Madiwani kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Wilaya ya
Mpanda. Diwani
wa Viti Maaalum Tarafa ya Mwese inayojumisha Kata za Kapalamsenga Ikola
na Karema yenyewe akichangia kwenye kikao cha Madiwani wakati wa kikao
hicho wengine ni madiwani wa Halmashauri hiyo.
………………………………………………………………………….
Na Kibada Kibada-Katavi
Zaidi ya shilingi milioni 80 zimetengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba vya maabara ya Sayansi vilivyojengwa katika shule za Sekondari zilizoko kwenye Halmashauri hiyo.
Hayo
yamelezwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Yasini
Kibiriti wakati akifungua kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani kwa
mwaka 2014/2015 kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Halamsahuri
hiyo.
Akizungumza
katika Kikao hicho Mwenyekiti Kibiriti ameeleza ujenzi wa maabara kwa
Halmashauri ya Mpanda uko vizuri sana kwani wameishakamilisha ujenzi na
fedha hizo zilizotengwa ni kwa ajili ya ukamilishaji ikiwa ni pamoja na
kununua vifaa vitakavyotumika kwenye nmaabara hizo.
Akaongeza
kuwa hadi kufikia oktoba 15 mwaka huu anaimani watakuwa wamekamilisha
kila kitu na kwa Halmashauri za Mkoa wa Katavi Halamshauri ya Mpanda
inaonekana kufanya vizuri katika ukamilishaji wa ujenzi wa maabara
ingawa haipongezwi kwa juhudi inazozifanya katika kutekeleza kwa wakati
maagizo yanayotolewa na Viongozi wa juu wa serikali kuanzia ngazi ya
Mkoa na Taifa.
Mhe,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete
aliagiza ujenzi wa Maabara kwa shule zote za sekondari na ifikapo
mwezi novemba mwaka huu kila Halmashauri iwe imekamilisha ujenzi
huo,akawagiza wakuu wote wa Wilaya na Mikoa ambao hawatakamilisha ujenzi
wajiondoe wenyewe kwa upande wa Halmashauri ya Mpanda wao
wamefanikiwa kukamilisha ujenzi huo.
Katika
ujenzi huo zaidi ya shilingi milioni 560 zimetumika kujenga maabara
nane zenye vyumba viwili viwili kwenye shule za Sekondari
Mpandandogo,Karema,Ilandamilumba,Ikola,Mwese,naMishamo maabara zote hizo
ziko vizuri kweli kweli tofauti na inavyozungumuziwa na watu kuwa
Halmashauri iko nyuma katika utekelezaji wa ujenzi wa maabara siyo
kweli.
Awali
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpanda Estomih Chang’ah alieleza
changamoto inayoikabili Halmashauri katika utengenezaji wa barabara za
Halmashauri hiyo kutokana na wakandarasi kutokuwa na Vifaa vya kutosha
hali inayofanya ucheleweshaji wa kukamilika kwa barabara kwa wakati.
Chang’ah
akaeleza wakandarasi wengi wanapokuja kuomba kazi kwenye Halmashauri
hawakamilishi kazi zao kwa wakati ,ambapo wanatakiwa kutekeleza kazi zao
kwa wakati lakini ajabu bado unakuta wanaomba msaada wa kusaidiwa vifaa
vya ujenzi wakati walishapatiwa kazi kwa mjibu wa mkataba wanatakiwa
wakabidhi kazi siyo kuomba msaada tena wakusaidiwa vifaa vya
kukamilishia kahiyo kule waliko pewa kazi.
Wakiongea
katika kikao hicho Diwani wa Kata ya Kapalamsenga Moses Joseph alieleza
kuwepo ucheleweshaji wa kusambaza kifusi kwenye barabara ya
Kapalamsenga Ifume kazi inayofanywa na mkandarasi ambaye aliingia
mkataba na Halmashauri lakini kazi hiyo inaonekana kusuasua na
haifahamiki lini ataikamilisha.
No comments:
Post a Comment