Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Platinum Credit Ltd Bw. Elias Samwel
akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa vifaa vya
michezo kwa baadhi ya Timu za Wizara na Taasisi za Serikali leoj jijini
Dar es Salaam, vifaa hivyo vimetolewa ili kusaidia timu hizo
zinazoshiriki mashindano ya SHIMIWI ambayo mwaka huu yanatarajiwa
kufanyika kuanzia tarehe 27 Septemba hadi tarehe 11 Oktoba mkoani
Morogoro.Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa SHIMIWI Moshi Makuka.Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba
Nkinga akimtunuku cheti Mwakilishi wa Platinum Credit Ltd Bw. Ferdinand
Kambanyumba ikiwa ni kutambua na kuthamini mchango wao katika kuendeleza
michezo wakati wa hafla ya kuwaaga wachezaji wa Wizara watakaoshiriki
mashindano ya SHIMIWI 2014
Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bibi. Concilia Niyibitanga akipokea kwa niaba ya
Katibu Mkuu, msaada wa vifaa vya michezo kutoka kwa Meneja Mauzo wa
Kampuni ya Platinum Credit Ltd Bw. Ferdinand Kambanyuma wakati wa hafla
ya kukabidhi msaada huo kwa baadhi ya timu za Wizara na Taasisi za
Serikali zinazotarajia kushiriki mashindano ya SHIMIWI leo jijini Dar es
Salaam.Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza rasmi kuanzia tarehe 27
mwezi huu na kumalizika tarehe 11 Oktoba mkoani Morogoro.Kaimu
Katibu Mkuu wa SHIMIWI Bw. Moshi Makuka (kulia) akipokea msaada wa
vifaa vya michezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Platinum
Credit Ltd Bw. Elias Samwel wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo kwa
baadhi ya timu za Wizara na Taasisi za Serikali zinazotarajia kushiriki
mashindano ya SHIMIWI leo jijini Dar es Salaam.Mashindano hayo
yanatarajiwa kuanza rasmi kuanzia tarehe 27 mwezi huu na kumalizika
tarehe 11 Oktoba mkoani Morogoro.Mwenyekiti
Timu ya Utumishi Bw. Lumuli Mtaki (kushoto) akipokea msaada wa vifaa
vya michezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Platinum Credit
Ltd Bw. Elias Samwel wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo kwa baadhi
ya timu za Wizara na Taasisi za Serikali zinazotarajia kushiriki
mashindano ya SHIMIWI leo jijini Dar es Salaam.Mashindano hayo
yanatarajiwa kuanza rasmi kuanzia tarehe 27 mwezi huu na kumalizika
tarehe 11 Oktoba mkoani Morogoro.
No comments:
Post a Comment