Rais
wa Shirikisho la Dunia la mchezo wa Karate (UPAM), Profesa Martina
Maurizio (kulia), akiwaelekeza jambo wachezaji wa mchezo huo walioko
kambini Dar es Salaam jana. Wachezaji sita wa timu hiyo wanatarajia
kuondoka Septemba 28 mwaka huu kwenda nchini Albania kushiriki
mashindano ya dunia ya mchezo huo.
Wachezaji hao sita wakiwa wameshika bendera ya timu hiyo. Kulia ni Rais wa Shirikisho la Dunia la mchezo wa Karate (UPAM), Profesa Martina Maurizio.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Wataalamu wa Tiba za Michezo Tanzania (TASMA). Dk.
Nassoro Matuzya (kushoto), akimpima uzito mchezaji, Ramadhan Jangle
ikiwa ni maandalizi ya mashindano hayo.
Dk. Nassoro Matuzya (kushoto), akimpima presha mchezaji, Heri Msukile. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Mwalimu wa mchezo huo, Max (kulia), akimfua Master Dhabiti Athuman Msawila. ‘Master Hugu’
Mchezaji
Ramadhan Hassan (kulia), akikwepa kwanja la Heridini Mwinyiheri wakati
wakiendelea na mazoezi katika Klabu ya Yanga Jangwani jana.
Wachezaji Hamisi Magigo (kushoto) na Master Dhabiti Athuman Msawila. ‘Master Hugu’ wakirushia makonde katika mazoezi hayo.
Dotto Mwaibale
WACHEZAJI sita wa timu ya Karate wanatarajia kuondoka nchini kwenda Albania kushiriki mashindano ya dunia ya mchezo huo.
Washiriki
hao tayari wamefanyiwa vipimo vya afya zao pamoja na uzito Dar es
Salaam jana na Dk. Nassoro Matuzya ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha
Wataalamu wa Tiba za Michezo Tanzania (TASMA).
Kikosi hicho cha watu 20 kinatarajiwa kuondoka nchini Septemba 28 kuelekea nchini humo kwa mashindano hayo.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Rais wa Shirikisho la Dunia
la mchezo huo (UPAM) Profesa Martina Maurizio alisema wachezaji hao
wataungana wataungana na wenzao kutoka Mwanza, Unguja na Arusha ambapo
utafanyika mchujo ili kupata timu ya taifa.
Alisema
wachezaji hao wapo kambini na wamepata mafunzo ya kutosha na hivyo ni
lazima warudi na ushindi pamoja na kuitangaza Tanzania duniani.
“Watanzania
wengi bado hawajaupa kipaumbele mchezo huu jambo linalofanya usahaulike
lakini watajitahidi kuufanya mchezo huo ukubalike hapa nchini kama
ilivyo kwa nchi nyingine.
Maurizio alimpongeza Mkurugenzi wa Princecasino kwa kujitolea kwa hali na mali kudhamini safari hiyo.
No comments:
Post a Comment