YANGA SC imeanza vibaya ligi kuu
soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015 baada ya jana kukubali kipigo cha
2-0 katika mechi ya ufunguzi iliyopigwa uwanja wa Jamhuri mkoani
Morogoro dhidi ya wenyeji Mtibwa Sugar.
Ikicheza mbele ya mashabiki
waliofurika kutoka Dar es salaam, Morogoro na mikoa ya jirani, Yanga
ilionesha kandanda safi na kupata nafasi nyingi za kufunga, lakini
washambuliaji wake walichemsha kuzibadili kuwa magoli.
Kikosi cha Mtibwa Sugar kilichoizamisha Yanga mabao 2-0 jana uwanja wa Jamhuri Morogoro. (Picha kwa hisani ya Globalpublisher)
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MARCIO Maximo aliwahi kumfundisha kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime akiwa na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Mexime kama ilivyo kwa makocha wengine ambao hupenda kuwaadhibu waalimu wao pale wanapokutana wakiwa na majukumu sawa, jana alifanikiwa kumtandika kwa mara ya kwanza Marcio Maximo mabao 2-0 akiiongoza Yanga.

No comments:
Post a Comment