Ukosefu wa Uwazi ni Chanzo cha Rushwa
Kipimo Abdallah
KUTOKUWEPO kwa uwazi, uadilifu
na uwajibikaji katika mikataba mbalimbali ambayo serikali inaingia na
wawakezaji kutoka nje ni moja ya sababu ya kuongezeka kwa rushwa kwa
baadhi ya watumishi wa umma na wawekezaji.
Hayo yamebainishwa na Mwahadhiri
Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Uchumi
Profesa Humphrey Moshi wakati akizungumza na mwandishi habari hii kwenye
kongamano ambalo linaratibiwa na taasisi ya Jukwaa la Sera (Policy
Forum).
Alisema kukosekana kwa uwazi
katika mikataba mbalimbali ni moja ya sababu ambayo imekuwa ichangia
rushwa kwenye michakato na makubaliano mengi ambayo yanahusisha serikali
na wawakezaji.
Profesa Mushi alisema Serikali
imekuwa inapata kigugumizi katika kuweka wazi baadhi ya mikataba kwa
kile kinachodaiwa kuwa ni siri baina ya mwekezaji na serikali jambo
ambalo halina ukweli tofauti na rushwa.
“Mimi nimekuwa nikifanya tafiti
mbalimbali hasa za mausuala ya kukua kwa uchumi ni wazi kuwa zipo fedha
nyingi ambazo zinapotea ambapo mwanzo wake unaanzia kwenye uingia ji wa
mikataba hadi katika utekelezaji ambazo zinaelekezwa katika rushwa”,
alisema Mushi.
Mwahadhiri huyo wa UDSM alisema
kuonyesha kuwa serikali haina dhamira ya kuondoa hiyo changamoto imekuwa
ikiwaruhusu wawekezaji hao kutoweka hata akaunti zao wazi kama ilivyo
kwa nchi zingine duniani.
Profesa Mushi ambaye pia aliwahi
kuwa mshauri wa masauala ya uchimi wa Rais wa Zanzibar Abeid Aman
Karume pamoja na Ofisi ya Hazina ya Tanzania alisema iwapo Tanzania
itajikita katika uwazi, uwajibikaji na uadilifu maendeleo yatapatikana
kwa haraka.
Mchumi huyo mwandamizi alisema
ni dhahiri kuwa kumekuwepo kwa ukiukwaji mkubwa katika maamuzi hivyo ni
vema kujiangalia upya kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya kwa maslahi
ya Taifa.
Alisema Tanzania ni nchi ambayo
imebarikiwa fursa mbalimbali ila kukosekana kwa uadilifu na uwazi kwa
baadhi ya watendaji rasilmali hizo zipo hatarini kupotea.
No comments:
Post a Comment