Na Mwandishi wetu
Mwanamke
albino Mariam Stanford aliyepoteza mikono yake yote miwili wakati
iliponyofolewa na majahili asiowajua Oktona7, 2008 ameitaka serikali
kuwanyonga wote wanaopatikana na hatia ya kuua albino nchini.
Alisema
hata adhabu ya kifungo cha maisha haiwatoshi kwa jinsi wanavyosababisha
maisha ya mashaka na yenye uchungu kwa walemavu wa ngozi.
Akiongea
kwa uchungu huku hapa na pale akitulia kwa kuzidiwa na machozi kiasi
cha kushidwa kuzungumza Stanford ambaye alisema wakati akikatwa mikono
yake alikuwa na mimba ya miezi mitano na ambayo ilitoka alisema majahili
hao si wa kusamehewa.
Alisema akiwa mama wa familia kitendo cha kumuondolea mikono yake
kimemfanya kuwa tegemezi hali ambayo inaongeza maumivu juu ya maumivu
ambayo anayo ya kunyanyapaliwa na jamii.
Alisema
hayo wakati akitoa ushuhuda katika adhimisho la siku ya amani duniani
iliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es
Salaam.
Alisema
japokuwa Tanzania inaelezwa kuwa nchi ya amani wananchi wake wenye
ulemavu wa albino hawana amani kutokana na kuwindwa kama digidigi.
Alisema kwa sasa Tanzania ni kisiwa cha matatzio kwa kundi hilo ambalo
sasa linajificha na wala kutokujua kesho ikoje au siku hiyo ikoje.
Alisema
ni vyema jamii ikawatazama na kuwasaidia kwa kuhakikisha kwamba
wanasaidia kuwafichua watenda maovu hao hasa ikizingatiwa kwamba watu
wenye albinizimu ni watu na watu kama watu wengine na hawawezi kuwa
chanzo cha utajiri kwa binadamu wenzao.
Alisema
anatamani kuona waliotiwa hatiani wakiuuawa hadharani au hata watu hao
nao kukatwa viungo vyao ili watambue jinsi isivyofaa kuwafanyia binadamu
wenzao matendo hayo.
Alishukuru
taasisi ya Under the Same Sun kwa kumsaidia toka aliponyofolewa mikono
mpaka leo na kuhimiza serikali kuona namna ya kuwasaidia waliokatwa
viungo vyao ili waweze kusihi maisha ya kawaida.
Pamoja
na kuomba watu hao wanyongwe Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali George
Masaju aliitaka jamii kutambua kwamba sheria ya kuua anayeua ipo lakini
inakabiliwa na mashindano na wanaharakati huku watoa ushahidi
wakishindwa kuisaidia mahakama kufikia maamuzi katika kesi za maalbino.
Alisema ni wajibu wa wananchi kusimamia amani kwa kuhakikisha wanaisaidia serikali kutekeleza wajibu wake.
Naye
Balozi wa Uturuki nchini alisema kwamba Ali Davutoglu amesema kwamba
ujenzi wa kituo cha maalbino Bagamoyo utaanza hivi karibuni ili
kuwapatia nafasi wananchi hao kuwa katika hali ya kawaida.
Kituo hicho ambacho kitakuwa na uwezo wa kuchukua watu 500 na kuwa chemchem ya maarifa kwa watu wenye albinizimu.
Katika
adhimisho hilo watoto wenye albuinizim walitoa shoo ya nguvu
iliyowafanya watu mbalimbali kujimwayamwaya katika eneo la wazi na kutoa
zawadi kwa vijana hao.
Aidha
bendi ya vijana ilitumbuiza na kwaya ilikuwepo kutoa ushaiwishi wa
kuelewa umuhimu wa amani huku wazungumzaji wengine wakitaka wanasiasa
kuhudhura maadhimisho hayo na kupeleka ujumbe kwa wananchi ambao
wanawasikiliza.
Katika
adhimisho hilo wanasiasa waliokuwepo ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa dar
es salaam, Madabida, Kaimu katibu Mkuu NCCR-Mageuzi Faustin Sungura na
Naibu katibu mkuu CUF Magdalena Hamis Sakaya ambaye pia ni mbunge wa
viti maalumu Tabora.
No comments:
Post a Comment