WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali haitataifisha shule, zahanati,
hospitali wala Vyuo Vikuu vinavyoendeshwa na taasisi za kidini na
amewahimiza wajenge zaidi na zaidi ili kuisaidia jamii kubwa ya
Watanzania.
Ametoa
wito huo wakati akizungumza na walimu, wazazi na wahitimu wa kidato cha
nne wa shule ya sekondari Magnificat iliyoko Sanya Juu, wilayani Siha
mkoani Kilimanjaro.
Waziri
Mkuu ambaye aliwasili Sanya Juu jana asubuhi (Jumamosi, Septemba 20,
2014) akitokea Dodoma, alisema huko nyuma Serikali ilitaifisha shule na
vyuo lakini kwa kiasi fulani ilishindwa kuviendesha ikaamua kuvirudisha
kwa wamiliki wake ambao ni taasisi za kidini.
“Ni
kweli huko nyuma tulikuwa navyo, lakini tumevirudisha kwenu tunataka na
ninyi ni washirika katika kuleta maendeleo kwa wananchi walio wengi,”
alisema Waziri Mkuu.
“Nilishawahi
kusema huko nyuma na leo nasisitiza tena kwamba hatutaifisha shule,
zahanati, hospitali wala Chuo Kikuu chochote cha taasisi ya kidini.
Ninawasihi mjenge zaidi na zaidi,” aliongeza.
Waziri
Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa shule hiyo
iliyoanzishwa Januari 15, 2011, aliwakabidhi vyeti wanafunzi 42 wa
kidato cha nne wanaotarajia kufanya mtihani wa kidato cha nne Novemba,
mwaka huu ikiwa ni mara ya kwanza kwa shule ya sekondari ya Magnificat
kufanya mtihani huo.
Waziri
Mkuu aliwapongeza wanafunzi hao kwa kushika nafasi ya kwanzawilayani
Siha kwenye mitihani ya utamirifu (yaani mock) katika kidato cha nne.
“Vilevile, shule hii imekuwa ya 12 kati ya shule 316 za Mkoa wa
Kilimanjaro na ya 16 kati ya shule 564 kwa Kanda ya Kaskazini Mashariki
zilizofanya mtihani huo. Mimi napata imani kuwa watafanya vizuri kwenye
mtihani wao wa kidato cha nne Novemba 2014,” aliongeza.
Mapema,Mkuu
wa Shirika la Masista la Kazi ya Roho Mtakatifu na Meneja wa Shule
hiyo, Sista Inviolata Kessy alisema shule hiuo ilianzishwa kwa lengo la
kutoa elimu bora na kuwashawishi watoto wa kike wa Kimasai waone umuhimu
wa elimu na hivyo kuwaepusha na ndoa za utotoni. Vile vile, kuwapa
msingi mzuri wa elimu kama sehemu ya maandalizi yao ya kupata elimu ya
juu.
Alisema
shule hiyo ambayo ni ya mchanganyiko na ya mchepuo wa sayansi na
biashara, imefanikiwa kujenga maabara tatu za kemia, fizikia na
baiolojia pamoja na chumba cha kompyuta.
Akisomarisalakwa
niaba ya wahitimu, Anastazia Kimaro alisema shule hiyo inakabiliwa na
changamoto nyingi zikiwemo ukosefu wa jengo la utawala pamoja na basi la
shule la kuwapeleka wananfunzi kwenye ziara za mafunzo.
Aliomba
pia wawe wanapelekewa magazeti ya kila siku na kila wiki ili wanafunzi
wa shule waweze kupata taarifa mbalimbali za mambo yanayojiri nchini na
duniani.
No comments:
Post a Comment