Kaimu mkuu wa mkoa wa Morogoro
ambaye ni mkuu wa wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka akikabidhiwa zawadi
ya fulana na Mkurugenzi wa uhusiano na sheria wa TBL, Steven Kilindo
yenye ujumbe wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani baada ya mkuu huyo
kuzindua rasmi upimaji wa afya kwa madereva wa mabasi na malori ya
masafa marefu katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro, zaidi
ya madereva 200 wanatarajiwa kupimwa afya katika vituo vya Mikese
Morogoro, Mkata mkoani Pwani na Makuyuni mkoani Arusha. katikati ni
Mganga mkuu wa macho wa jeshi la polisi Dk Charles Msenga na kulia ni
kaimu mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Morogoro, Willie Mwamasika
Mganga
mkuu wa macho wa jeshi la polisi Dk Charles Msenga kulia akimpima uwezo
wa kuona macho dereva wa kampuni ya usafirishaji wa abirianya Abood
basi Morogoro, Augustino Mpepwa wakati wa uzinduzi wa afya kwa madereva
wa mabasi na malori ya masafa marefu ikiwa sehemu ya uzindui wa wiki ya
nenda kwa usalama barabarani katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa
Morogoro, zaidi ya madereva 200 wanatarajiwa kupimwa afya katika vituo
vya Mikese Morogoro, Mkata mkoani Pwani na Makuyuni mkoani Arusha.
DK YOHANA KIBONA KUMPIMA DC ANTHONY MTAKA AFYA KULIA NI DK CHARLES MSENGA MGANGA WA JESHI LA POLISI MAKAO MAKUU
DR YOHANA KIBENA akiwaandikisha
madereva tayari kupimwa afya zao katika Hospitali ya Polisi ya Morogoro.
TBL imefadhili upimaji wa afya hizo.
No comments:
Post a Comment