Wahitimu
wa kidato cha nne, Shule ya Sekondari Lilasia, iliyopo eneo la Kitunda
kwa Kibeberu, Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na wadau
mbalimbali wa shule hiyo, kwenye sherehe ya mahafali ya sita
iliyofanyika Dar es Salaam jana.Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari
Lilasia, iliyopo eneo la Kitunda kwa Kibeberu, Dar es Salaam, Beatha
Shembilu, akipokea cheti cha kuhitimu kidato cha nne kutoka kwa mgeni
rasmi, Samwel Lyimo, katika sherehe za mahafali ya sita ya shule hiyo,
zilizofanyika Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Shule hiyo,
Christina Lyimo, na Mkuu wa Shule, Silas Kamando. Wanafunzi wa Kidato
cha Nne nchini kote wanatarajia kuanza mitihani yao ya Taifa ifikapo
Novemba 3 mwaka huu.
Mwanafunzi
wa Shule ya Sekondari Lilasia, iliyopo eneo la Kitunda kwa Kibeberu,
Dar es Salaam, Flora Jeremiah, akipokea cheti cha kuhitimu kidato cha
nne kutoka kwa mgeni rasmi, Samwel Lyimo, katika sherehe za mahafali ya
sita ya shule hiyo, zilizofanyika Dar es Salaam jana. Kulia ni
Mkurugenzi wa Shule hiyo, Christina Lyimo, na Mkuu wa Shule, Silas
Kamando. Wanafunzi wa Kidato cha Nne nchini kote wanatarajia kuanza
mitihani yao ya Taifa ifikapo Novemba 3 mwaka huu.
Mwanafunzi
wa Shule ya Sekondari Lilasia, iliyopo eneo la Kitunda kwa Kibeberu,
Dar es Salaam, Peter Nyaikobe, akipokea cheti cha kuhitimu kidato cha
nne kutoka kwa mgeni rasmi, Samwel Lyimo, katika sherehe za mahafali ya
sita ya shule hiyo, zilizofanyika Dar es Salaam jana. Kulia ni
Mkurugenzi wa Shule hiyo, Christina Lyimo, na Mkuu wa Shule, Silas
Kamando. Wanafunzi wa Kidato cha Nne nchini kote wanatarajia kuanza
mitihani yao ya Taifa ifikapo Novemba 3 mwaka huu.
Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari Lilasia, Christina Lyimo.
Shule ya Sekondari Lilasia yafanya mahafali ya 6.
*Wataka kuwe na lugha maalum mashuleni
NA ANDREW CHALE
NJIA nyepesi ya kukabiliana na
tatizo kubwa la ajira kwa vijana nchini ni kuongeza kasi ya uwekezaji
kwenye viwanda, sanjari na kuutazama upya mtaala wa kufundishia kuanzia
shule za msingi hadi vyuo vikuu, hususan kwenye eneo la lugha, imeelezwa
Akizungumza kwenye mahafali ya
6, ya Shule ya Sekondari Lilasia, iliyopo Kitunda, Dar es Salaam jana
septemba 20, Mkurugenzi wa shule hiyo, Christina Lyimo, alisema kupitia
viwanda vijana kwa maelfu yao wataajirika na kujiajiri kwa mtiririko wa
fursa zitakazokuwepo, huku pato la taifa likizidi kukua.
“Sina shaka sana na rasilimali
tulizonazo..zinatosheleza, tuna uchumi mkubwa, hebu kama serikali
itanisikia niombe sasa tuwekeze nguvu kwenye viwanda, tupeleke surveyors
wakapime maeneo, sababu tuna nguvu kazi kubwa, tuna rasilimali..tuanzie
hapo,” alisema Lyimo.
Aidha, Lyimo, ambaye kitaaluma
ni mwalimu anayehudumu kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 25 sasa, ameshauri
yafanyike mabadiliko ya mtaala hususan kwenye lugha ya kufundishia, huku
akisisitiza ni wakati mwafaka sasa kwa taifa kuamua ni lugha ipi
itumike kufundishia kama ni Kiingereza au Kiswahili, tofauti na ilivyo
sasa kuchanganya changanya.
“Watoto wengi wanababaika kwenye
mitihani kwa sababu ya Lugha..watoto wengine wanafeli kwa kushindwa
kujieleza kwa lugha za kigeni!..shule ya msingi Kiswahili miaka
saba..sekondari kiingereza kwa kweli inachanganya, tuamue basi
kubadilisha kama ni medium basi ziwe kuanzia awali hadi vyuo vikuu, na
kadhalika kama Kiswahili iwe hivyo,” alisema
Hata hivyo, katika hatua
nyingine, aliwaomba wafadhili kujitokeza kuchangia shule hiyo kwenye
eneo la upatikanaji wa maabara ya kisasa, ikizingatiwa shule kwa sasa
pamoja na mambo mengine inasomesha watoto yatima bure na kusaidia kwa
kiasi utoaji wa elimu bora kwa watoto wa Kitunda na kwingineko nchini
“Tunaomba pia serikali igeuzie
macho kwenye shule hii, tuna watoto yatima hapa, itusukume kwenye kupata
ruzuku sababu tunasaidia taifa na hata ada tunazopokea ni ndogo mno,”
alisema
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya
Lilasia, Silas Kamando alisema katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi
36 wakiwemo wanaume 17 na wasichana 19 wamehitimu kidato cha nne mwaka
huu, na kwa sasa wanajiandaa na mtihani wao wa taifa unaotarajia
kufanyika Novemba 3 mwaka huu, nchini kote.
No comments:
Post a Comment