Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Dk.Helen Kijo-Bisimba.
Mratibu wa Dawati la Katiba LHRC, Anna Henga
Mwanasheria wa LHRC, Harold Sungusia
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Dk.Helen Kijo-Bisimba
(katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es
Salaam jana, wakati akitoa taarifa kuhusu awamu ya pili ya kampeni ya
kusambaza uelewa wa rasimu ya pili (Kampeni Gogota). Kulia ni Mratibu wa
Dawati la Katiba wa kituo hicho, Anna Henga na Mwanasheria wa Kituo
hicho, Harold Sungusia. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za
jamii.com-simu 0712-727062)
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Dotto Mwaibale
KITUO cha
Sheria na Haki za Binadamu kimedai kuwa Bunge Maalumu la Katiba
linaloendelea linaendeshwa kimabavu kwa na kutumia fedha za wananchi
bure wakati wakijua fika hakuna katiba itakayopatikana.
Hayo
yalisemwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria
na Haki za Binadam (LHRC) Dk. Helen Kijo-Bisimba, wakati akitoa taarifa
kuhusu awamu ya pili ya kampeni ya kusambaza uelewa wa rasimu ya pili
(Kampeni gogota) kwa wananchi.
“Cha
kusikitisha ni kwamba tumepoteza mabilioni ya fedha ambazo zingeweza
kusaidia kwenye sekta mbali mbali zikiwemo za afya na elimu kwa kuwalipa
wajumbe wa bunge la katiba,” alisema.
Alisema
wakati wa kampeni hiyo ambayo imefanyika kwenye mikoa 20 nchini kituo
hicho kimebaini kuwa wapo asilimia kubwa ya wananchi wanakerwa na
mwenendo wa mchakato wa bunge hilo kwa kuchakachua maoni yao
yaliyokusanywa na Tume ya mabadiliko ya katiba.
Alisema
wakati wa kampeni hiyo ya gogota kituo hicho kimefanikiwa kufika kwenye
wilaya zote, na kata tatu kwa kila mkoa ambapo kilifanikiwa kurudisha
ajenda ya katiba na uelewa wa rasimu ya pili ya katiba kwa wananchi.
Alisema
hiyo ni moja ya mafanikio waliyoyapata kuyajua kwa wananchi kwenye
kampeni hiyo ambayo ililenga kuhamasisha wananchi kushiriki katika
mchakato hususani kufuatilia bunge la katiba na upigaji wa kura ya maoni
muda utakapo fika.
Pamoja na
mafanikio hayo pia kitu hicho kimekutana na changamoto mbali mbali
ikiwemo ya uelewa mdogo kuhusu katiba hususani walio pembezoni mwa miji.
Alitaja
mikoa hiyo ni Arusha, Tanga, Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu, Mbeya,
Rukwa, Kilimanjaro, Manyara, Katavi, Iringa, Mara, Njombe, Ruvuma, Pemba
Kaskazini, Kusini, Pemba mjini Magharibi, Unguja Kusini na Kasazini.
Alitaja
changamoto nyingine ni kutokujua kusoma na kuandika kwa baadhi ya
wananchi, umangi meza kwa badhi ya viongozi wa mikoa, hofu ya kutopata
katiba na mfumo dume kwenye jamii.
No comments:
Post a Comment