Kipimo Abdallah
ZAIDI
ya shilingi milioni 200 zimetumika katika maboresho ya kituo cha
mawasiliano cha Mnyusi mkoani Tanga kinachotumika kupokea na kutuma
mawasiliano ya radio zinazo tumika katika usafiri wa anga.
Hayo
yamebainishwa na Afisa habari wa TCAA Bestina Magutu wakati
akizungumza na mwandishi wahabari hii leo jijini Dar es Salaam.
Alisema
maboresho hayo yametokana na ukweli kuwa kituo hicho kilikuwa hakifanyi
kazi kwa muda mrefu hali ambayo ilikuwa inaasababisha kukosekana kwa
mawasiliano katika ukanda wa mashariki kutoka usawa wa bahari.
Kabla
ya kukamilika kwa maboresho haya baadhi ya maeneo mchini yalikuwa
hayapati mawasiliano ya kitekonologia kutoka nchini na badala yake
walikuwa wanapata huduma hiyo kutoka nchi jirani,”alisema.
“Mradi
huo umekamilika na kukabithiwa kwenye mamlaka ya usafiri wa anga mwezi
agost mwaka huu na kukabithiwa kwenye kituo cha Mnyusi jijini
Tanga,umegharimu shilingi za kitanzania milioni 292,887,921,” alisma.
Magutu
aliongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo kumeongeza ufanisi wa
usafirishaji wa anga kwa kurahisisha huduma ya kuongoza ndege,utaongeza
mapato kwa mamlaka hiyo.
“Nimategemeo yangu kwamba kupitia maboresho haya mamlaka itajiongezea mapato kupitia tozo ya huduma ya uongozaji ndege,
Kwa
upande wake Mkaguzi Mwandamizi,Redemptus Rugombe alisema mamlaka
inandelea kupanua miondombinu ya kuongeza ndege sanjari na mabadiliko ya
teknolojia ili kumudu ukuaji wa sekta ya usafirirshaji wa anga.
“Takwimu
za mwaka 2031 zinaonyesha ongezeko la miruko ya ndege (flight movement)
imeongezeka hadi kufikia miruko 230,458 sawa na ongezeko la asilimia3.6
kotoka miruko 222,430 mwaka 2012,
Kadharika
katika kipindi hicho idadi ya abilia imeongezeka kutoka 4,056,925 hadi
kufikia 4,626,016 sawa na ongezekola asilimia 14,kwa sasa idadi ya
abilia inatarajiwa kuongezeka zaidi kufikia mwishoni mwa mwaka huu,”
alifafanua.
Mkaguzi
Mwandamizi huyo aliongeza kuwa katika kuhakikisha watanzania wanapata
uelewa wa elimu ya mamlaka ya anga mamlaka inaendelea kuwapatia
wanafunzi mafunzo kwa njia ya udhamini na hadi sasa kuna wamnafunzi
watano wanaendelea ma mafunzo ya urubani.
“Kwa
tarifa za wanafunzi wetu ambao wako Afrika ya kusini kwa masomo ya
urubani chini ya udhamini wa mamlaka wanaendelea vizuri,huu mpango kwa
mamlaka ni endelevu ili kusaidia kuwawezesha watanzania kpambana katika
soko la ajira, “alisema.
No comments:
Post a Comment