Bunge
Maalum la Katiba limependekeza muundo wa uongozi wa Serikali utakuwa na
Makamu watatu wa Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania.
Kauli
hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa
Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Andrew Chenge wakati akiwasilisha Rasimu
ya Katiba inayopendekezwa wakati wa kikao cha arobaini na mbili cha
Bunge hilo.
Amesema
kuwa katika mapendekezo hayo mgombea mwenza ndio atabaki kuwa Makamu
wa Kwanza wa Rais, na kwa upande wa Rais wa Zanzibar atakuwa Makamu wa
Pili na Waziri Mkuu atakuwa Makamu wa tatu wa Rais.
Amesema
kuwa Kamati hiyo ya uandishi imeona ni busara mgombea mwenza kuendelea
kuwa Makamu wa Rais kwa kuwa itakuwa rahisi kwake kukaimu uongozi kama
itatokea bahati mbaya Rais aliyemadarakani hatakuwepo kwa namna moja au
nyingine kwani ataendeleza ilani za mwenzake kuliko atakavyokuwa wa
kutoka Zanzibar kama kutakuwa na vyama viwili tofauti vinatawala.
Kwa
upande wa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa pili , Chenge amesema kuwa
hatua hiyo itasaidia kuimarisha muungano kwani kiongozi huyo ni kiungo
muhimu katika kudumisha Muungano.
“Suala
la Rais wa Zanzibar kuwa Makamu ni la msingi kwa kuwa ni kiungo muhimu
ikizingatia historia ya nchi tangu mwaka 1964 muungano ulipoasisiwa
ilikuwa hivyo hadi mfumo wa vyama vingi ulipoanza mwaka 1992,” alisema Mhe. Chenge huku akiongeza kuwa anakuwa hivyo kwa nafasi yake.
Ameongeza kuwa Waziri Mkuu anakuwa Makamu wa Tatu kwa mujibu wa Cheo chake.
No comments:
Post a Comment