Baadhi ya Waamuzi waliochezesha michuano hiyo,
Baadhi ya Viongozi mbali mbali wakijiandaa kutoa zawadi kwa washindi wa michuano hiyo.
Baadhi ya Timu Zilizoshiriki
Jukwaa la Pespsi ambalo lilitumika kufanya matangazo Uwanjani
Wakazi wa Jiji la Mwanza wakifuatilia kwa Makini Mchezo wa Fainali
Baadhi ya Viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, pamoja na Meneja Mkuu wa Pepsi Mwanza, Nicolaus Coetz (wa kwanza kulia), wakifuatilia kwa Makini Fainali hiyo.
Meneja Mkuu wa Pepsi Mwanza, Nicolaus Coetz kulia akiangalia kwa Makini Mpambano wa Fainali
Meneja Mkuu wa Pepsi Mwanza, Nicolaus Coetz(kulia) akitafakari jambo wakati mpambano wa Fainali ukiendelea
Wasanii wa kundi la Bujora Traditional Group la jijini Mwanza wakionyesha vitu vyao kwa Mashabiki wa Soka waliofurika katika Uwanja huo wa Nyamagana jijini Mwanza.
Wasanii wa kundi la Bujora
Traditional Group la jijini Mwanza wakionyesha vitu vyao kwa Mashabiki
wa Soka waliofurika katika Uwanja huo wa Nyamagana jijini Mwanza.
Wasanii wa kundi la Bujora
Traditional Group
Meneja Mkuu wa Pepsi Mwanza, Nicolaus Coetz(kulia) akitafakari jambo wakati mpambano wa Fainali ukiendelea
Wasanii wa kundi la Bujora
Traditional Group
Meneja Mkuu wa Pepsi Mwanza, Nicolaus Coetz(kulia) akifafanua jambo wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi
Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula, akifafanua jambo wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi
Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa, akifafanya jambo wakati wa Fainali za Michuano hiyo.
Zawadi ya Bajaji almbayo ilishindaniwa
Shabiki wa Soka akiponyesha ukereketwa wake
Mkurugenzi
wa My Way Entertainment , Paul Mganga(kushoto) akifuatilia Fainali muda
mfupi kabla ya mpambano kumalizika, kushoto ni zawadi ya Vikombe vya
washindi.
Kiatu cha Dhahabu ambacho kilikuwa Gumzo kwa Wachezaji jijini Mwanza Meya Cup
Kocha wa Timu ya Mkolani, Wandiba Wandiba, akiinuliwa juu baada ya Timu yake kuchukua ubingwa wa Michuano hiyo |
Mashabiki wa Mkolani wakipagawa baada ya timu yao kuibuka kidedea
Meya wa jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula (kulia) akiongoza viongozi kueelekea kutoa zawadi(Kati kati ni mwenyekiti wa Chama cha mpira wilaya ya mwanza Jackison Songora)
Askari Polisi akionekana kuweka Ulinzi mkali kwenye Bajaji ambayo ilikuwa ni maalum kwa ajili ya zawadi kwa timu iliyoibuka mshindi
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakichukua moja ya kumbukumbu kwa ajili ya habari
mwenyekiti wa Chama cha mpira wilaya ya mwanza Jackison Songora, akifafanua jambo baada ya Fainali kumalizika.
Wachezaji wa Timu ya Mirongo (Wenye njano) wakisubiri kupokea zawadi ya Mshindi wa Pili
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakichukua moja ya kumbukumbu kwa ajili ya habari
mwamuzi bora kutoka Kituo cha Alliance, David Albert aliyepata zawadi ya Sh laki mbili
Meneja Mkuu wa Pepsi Mwanza, Nicolaus Coetz akikabidhi zawadi ya mfungaji bora kwa Paulo Godfrey |
TIMU
ya Kata ya Mkolani FC Mwishoni mwa juma imeibuka mabingwa wapya wa Kombe la Meya 2014
baada ya kuichapa timu ya Kata ya Mirongo bao 2-1 (jumamosi iliyopita) katika
mchezo wa fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Awali
katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu ulioanza mapema saa 8:00
mchana kwa timu ya Sokoni FC kuichapa Mnadani FC bao 3-0 na kuibuka
mshindi wa tatu wa michuano hiyo huku magori ya Sokoni yakifungwa na
Joseph Mwajalila dakika 33 kwa penati na Salimu Hamis dakika 39, 51 na
kuwapa tiketi ya ushindi wa tatu.
Fainali
hiyo iliyoshuhudiwa na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi
Evarist Ndikilo aliyeambatana na Katibu Mkuu wa TFF Selesitine Mwesigwa,
muasisi wa mashindano hayo Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza, Stanislaus
Mabula, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa Hida, Mwenyekiti wa Chama
cha soka Mkoa wa Mwanza (MZDFA), Jackson Songola na Katibu wa MZDFA,
Nasibu Mabrouk.
Ndikilo alisema kwamba mashindano hayo yamewasaidia vijana kuonyesha vipaji vyao, hivyo ni vyema sasa
Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiwatumia vijana walionesha uwezo kuunda timu ya Mwanza City FC kama ilivyofanya Jiji la Mbeya.
“Ni
bora mkaunda timu ya Mwanza City FC ili kushiriki ligi na huenda
ikatinga ligi kuu Bara kama walivyofanya wenzetu wa Mbeya na sasa timu
ya Mbeya City FC inashiriki ligi kuu, kwani timu zetu kongwe katika Mkoa
huu za Toto FC na Pamba FC zimeonekana kuishiwa mbinu na kufanya vizuri
ili kurejea ligi kuu,”alisema.
Katika
mchezo huo mkali wa vuta ni kuvute kilishuhudia timu hizo zikienda
mapumziko zikiwa hazijafungana na kipindi cha pili mchezaji
Siraji Juma aliwainua mashabiki kwa kuandika bao la kwanza na bao la
pili likifungwa na Paulo Godfrey huku katika hekaheka ya kuokoa mpira
ulioelekezwa langoni mwake akijikuta akijifunga na hadi mwisho wa mchezo
wadau wa michezo walishuhudia timu ya Mkolani ikitawazwa kuwa mabingwa
kwa kuinyuka Mirongo Fc bao 2 - 1.
Mashindano
hayo ya kombe la Meya 2014 yaliyodhaminiwa na Kampuni ya kutengeneza
vinywaji vya Pepsi (SBC), Ndikilo alikabidhi bingwa timu ya Mkolani FC
zawadi ya kombe, fedha tasilimu Sh milioni 1.5, medali ya dhahabu na
Bajaji ya mizigo yenye thamani ya Sh milioni 4.5, mshindi wa pili
alinyakuwa Sh milioni 2, kombe dogo na medali ya fedha.
Timu
ya Sokoni FC iliyoibuka mshindi wa tatu ilijinyakulia fedha tasilimu Sh
milioni 1, medali ya shaba na kombe dogo, mfungaji bora Paulo Godfrey
akiwa na bao nane na kunjinyakulia kiatu cha dhahabu na Sh laki mbili,
mwamuzi bora kutoka Kituo cha Alliance ilichukuliwa na David Albert na
kupata Sh laki mbili huku timu ya Kata ya Mahina FC ikipata Nidhamu bora
na Sh laki mbili.
No comments:
Post a Comment