Kipimo Abdallah
CHAMA
cha NCCR-Mageuzi kimesikitishwa na kitendo cha Bunge Maalum la Katiba
kuhitaji wajumbe ambao hawapo nchini au ndani ya Bunge kuruhusiwa kupiga
kura wakati ukweli ni kwamba ushiriki wao katika utengenezaji wa rasimu
hiyo ulikuwa mdogo.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi Faustin Sungura wakati
akizungumza na mwandishi wa habari hii jana jijini Dar es Salaam kwa
njia ya simu.
Alisema
utaratibu huo wa kuruhusu wajumbe walioko nje kupiga kura haujawahi
kutokea katika Bunge lolote hapa duniani jambo ambalo linatia aibu kwa
Taifa.
Kaimu
Katibu huyo alisema iwapo wajumbe hao ambao hawakushiriki katika
mchakato kwa kiwango cha kuridhisha wataruhusiwa kupiga kura hali hiyo
ingekuwa hata kwa wale wa UKAWA kwani uwepo wao nje una sababu kama hao
wengine.
“Jamani
Watanzania tuamke hii sasa aibu tunapopelekwa pabaya haiwezekani watu
wapo nje ya Bunge alafu wapewe nafasi ya kupiga kura jambo ambalo
haliwezi kuvumiliwa kwani linatia aibu nchi”, alisema.
Alisema
katika Bunge hilo linaloendelea mkoani Dodoma mambo mengi yamekiukwa
ila hapo walipofikia ni vema jamii ya Kitanzania ikafungua macho na
kuamua kufanya maamuzi mazito kwani kinachoonekana ni watu kuhitaji kwa
maslahi yao.
Sungura
alisema ni vema Wabunge waliopo Dodoma wakatambua kuwa mambo megine
hayalazimishwi kwani yanahusu jamii kubwa na sio kama wanavyofikiria
kuwa wao ndio wanahusika pekee.
Alisema
NCCR-Mageuzi imejipanaga kuhakikisha kuwa katiba hiyo inakataliwa
kutokana na ukweli kuwa kilichopo ndani sio yaliyokuwa mapendekezo ya
wananchi ambayo yaliwakilishwa na iliyokuwa Tume ya Katiba.
Sungura
alisema ukweli dhidi ya UKAWA kutoka Bungeni umedhihirika hivyo juhudi
zao ni kuhakikisha kuwa rasimu hiyo haipitishwi na wananchi kutokana na
kudharauliwa kwa maoni yao ambayo walipendekeza katika rasimu ya Jaji
Joseph Warioba.
Kaimu
Katibu Mkuu huyo alisema nguvu yao pia inaongezwa na maamuzi ya
Mahakama Kuu hivi karibuni ambapo imeweka bayana kuwa kitendo
kilichofanywa na Mwenyekiti wa Bunge hilo kupokea maoni mapya ni
ukiukwaji wa sheria.
Sungura
alisema mabadiliko na maingizo mapya yaliyofanywa na Bunge hilo ambalo
alilitaja kuwa ni la upande mmoja yamekiuka sheria kwa kiwango kikubwa
na cha kusikitisha.
Alisema
kwa sasa NCCR- Mageuzi ipo katika mikakati ya kuhakikisha wananchi
wanapata elimu sahihi juu ya mchezo mchafu unaofanywa na Bunge hilo
jambo ambalo litawajengea uwezo wa kufanya maamuzi sahihi katika upigaji
kura.
No comments:
Post a Comment