SERIKALI
inatambua na kuthamini mchango wa sekta ya hifadhi ya jamii nchini hasa
katika kusaidia kukuza na kuimarisha uchumi na kuinua hali za
watanzania kwa ujumla hasa wale wanaofikiwa na huduma hizo.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa
Mkoa wa Tanga,Salum Chima wakati akifungua semina ya mfuko wa Pensheni
wa PPF kwa maafisa wa makampuni mbalimbali katika (Kanda ya
Kinondoni)mkoa wa Tanga.
Amesema kuwa serikali inatambua kuwa huduma ya hifadhi ya jamii inawafikia watu wachache sana licha ya umuhimu wake kwa jamii.
Aidha amesema kuwa kwa kutambua
umuhimu huo serikali imekuwa ikiimarisha sekta hiyo ili iwez kupanua
wigo wa watu wanaonufaika na huduma hiyo kwa kurekebisha sheria na
kuweka mazingira bora kwa watu wote wanaojiunga na mfuko huo.
Alifurahishwa kusikia kuwa mfuko
wa Pensheni wa PPF ambayo ilianzishwa mwaka 1978 kwa ajili ya pensheni
za mashirika ya umma lakini pia kisheria inaweza kusajili hata makampuni
binafsi,taasisi za elimu na vyuo binafsi,taasisi za dini na
waliojiajiri wenyewe ikiwemo walioko kwenye sekta isiyo rasmi.
Amesema kuwa hatua hiyo itawafanya
watanzania wengi zaidi waweze kupata huduma bora za mfuko wa PPF na
kuwa na uhakika ya maisha bora ya sasa nay a baadae kama iliyokuwa kauli
mbiu ya PPF.
Kwa upande wake,Meneja wa PPF
Kanda ya Kinondoni,Pwani na Tanga,Zahra Kayugwa amesema kuwa
watawapeleka mahakamani waajiri wote ambao watakuwa hawawasilishi
michango ya wafanyakazi wao kwa wakati.
No comments:
Post a Comment