Makamu Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa
Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula katikati akikata utepe kuashiria
ufunguzi rasmi wa Jengo jipya la Ofisi ya CCM wilaya ya Chato. Wengine katika
picha ni Mbunge wa Chato Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Geita
Said Magalula, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Msukuma.
Mbunge wa Chato ambaye
pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiwa pamoja na
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula kulia mara
baada ya kumpokea katika kata ya Buseresere Mkoani Geita. Kushoto ni mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Geita ndugu Joseph Msukuma
Mbunge wa Chato ambaye
pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akiwa pamoja na Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula juu ya gari akihutubia
mamia ya wakazi wa Buseresere mara baada ya kuwasili katika eneo hilo.
Wananchi wa Buseresere
wakimsiliza Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe
Magufuli wakati alipopita kwenda kumpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM kwa upande
wa Tanzania Bara Mhe. Philip Mangula
Makamu Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa
Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula akisalimiana na baadhi ya wananchama
wa CCM katika kata ya Bwanga wilayani Chato mara baada ya kusimama kwa muda
akiwa njiani kuelekea Chato kwa ajili ya Ufunguzi wa Ofisi Mpya ya CCM wilaya
ya Chato.
Taswira ya Jengo jipya la Ofisi ya Chama cha
Mapinduzi CCM wilayani Chato ambalo ilikuwa ni ahadi ya Mbunge wa Chato ambaye
pia ni waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli
Makamu Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa
Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula akihutubia wananchi wa Bwanga
waliofika kumsalimia wakati akiwa njiani kuelekea Chato ambapo alizindua jingo
jipya la Ofisi hiyo ya kisasa.
Kijana wa Kikundi cha
Ngoma cha Chato akionyesha umahiri wake wa kuzungusha ringi la Tairi la
baiskeli kwenye mboni yake ya jicho hali iliyowashangaza wananchi wengi
waliofika.
Mbunge wa Chato
ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kulia akifurahia jambo
pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip
Japhet Mangula.
Makamu Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa
Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula akivuta utepe kuashiria ufunguzi rasmi
wa Ofisi ya CCM wilaya ya Chato ambayo ilikua ahadi ya Mbunge wa Jimbo hilo.
Picha na Mpiga Picha Wetu
=====================================================================
Makamu Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa
Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula amempongeza Mbunge wa Jimbo la Chato
Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na utekelezaji mzuri wa wa Ilani ya Uchaguzi
ya CCM kwenye jimbo lake.
Mheshimiwa Mangula
alitoa kauli hiyo mara baada ya kufungua rasmi jengo la ofisi ya CCM Wilaya ya
Chato ambalo liliahidiwa kujengwa na Mbunge huyo.
Mangula aliongeza kuwa
CCM inajivunia mafanikio hayo ambayo ni hazina kubwa kwa taifa na kukijengea
chama heshima kubwa ndani na nje ya nchi.
“Magufuli kama
anavyoitwa jembe amefanya kazi kubwa ambayo kila mtu anaiona, miaka ya nyuma aliwahi
kuahidi kuwa mtu atatoka Mtukula hadi Mtwara kwa usafiri wa Tax lakini hakuna
ailiyeamini, leo hii hilo linawezekana”
Ndugu Mangula aliongeza
kuwa wakati alipokuwa Mkoa wa Kagera
miaka ya 90s, hali ya Barabara nchini hata hapo Chato ilikua mbaya sana,
ilimlazimu kutumia siku mbili hadi tatu ili kufika Njombe lakini leo hali ni
tofauti kutokana na miundombinu kuboreshwa sana.
Aidha, Ndugu Mangula
amepongeza mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa haraka katika sekta ya Elimu
jimboni hapo kwani kutoka shule moja hadi shule zaidi ya 120 ni jambo la
kujivunia sana.
Kwa upande wake Mbunge
wa Jimbo la Chato Dkt. John Pombe Magufuli alieleza kuwa Chato imetoka mbali sana
kimaendeleo kwani hapo mwanzo ilikua kijiji ikapiga hatua na kuwa Kata na kwa
sasa ni Wilaya jambo ambalo ni la kujivunia sana.
Mbunge huyo aliongeza
kuwa Jimbo hilo kwa sasa limepiga hatua kubwa sana katika Sekta ya Mawasiliano,umeme,maji
na miundo mbinu ya barabara ambapo awali maendeleo hayo hayakuwepo.
“Nakumbuka kipindi cha
nyuma kulikuwa na basi moja tu ambalo lilikuwalikifanya safari zake kuelekea
Mwanza, na likikuacha basi huwezi kusafiri tena, lakini kwasasa mabasi zaidi ya
40 yanapita hapa kwenda sehemu mbalimbali ikiwemo Uganda” alibainisha
Mheshimiwa Magufuli.
Mheshimiwa Magufuli
aliongeza kuwa kwa upande wa Sekta ya elimu jimbo hilo limepiga hatua kubwa
kwani kwa sasa kuna shule za sekondari zaidi ya 30 na shule za msingi 131.
Pia alitaja mfano wa
barara ambazo zinatengezwa katika jimbo lake kwa kiwango cha lami kuwa ni
pamoja na barabara ya kutoka Bwanga kuelekea Biharamulo na Bwanga Uyovu ambazo zinajengwa
na Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi ili kurahisisha maendeleo ya kiuchumi
jimboni hapo,”alifafanua Magufuli.
Mheshimiwa Magufuli
aliwaahidi wakazi wa Buseresere na Bwanga kuwa kero yao ya kukosa maji na
mipango miji ataiwasilisha Serikalini haraka iwezekanavyo ili kuweza
kushughulikiwa.
No comments:
Post a Comment