Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa
Dkt. John Magufuli akihutubia wataalamu mbalimbali wanaoshiriki katika mkutano
wa 22 wa Elimu endelevu ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi jijini Dar e
s salam.
|
Rais Mstaafu wa awamu
ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi akitoa hutuba yake katika mkutano huo
jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa awamu
ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi wapili kutoka kushoto akimshukuru Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli mara baada ya kupokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti
wa (AQRB) Dkt. Ambwene Mwakyusa.
Rais Mstaafu wa awamu
ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi akikabidhi cheti kwa mwanafunzi bora wa
Insha kutoka Mkoa wa Dodoma Consolata Chidabile. Kulia ni Waziri wa Ujenzi
akishuhudia tukio hilo.
Rais Mstaafu wa awamu
ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi katikati akiangalia moja ya tiles mara
baada ya kufungua mkutano huo.
Washiriki mbalimbali
wa Mkutano wa 22 wa Elimu endelevu ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi
jijini Dar e s salam wakisiliza kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi katika mkutano
huo.
Msajili wa bodi ya
Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi(AQRB),
Arch. Jehad A. Jehad akitoa hotuba yake.
Rais Mstaafu wa awamu
ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe
Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na
wanafunzi walioshinda katika shindano la Insha kutoka mikoa mbalimbali.
(Picha kutoka Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini - Wizara ya Ujenzi).
===========================================
Rais Mstaafu wa awamu
ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi amezungumzia kuridhishwa kwake na utendaji wa Bodi
ya Usajili wa wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi nchini (AQRB).
Akizungumza katika
Mkutano wa 22 wa Elimu endelevu wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi
jijini Dar Es Salaam, Mzee Mwinyi amesema ni wajibu wa bodi hiyo kuhakikisha
utekelezaji endelevu wa taratibu za mienendo ya kitaalamu dhidi ya usajili wa wataalam hao nchini unazingatiwa
kwa viwango vya ubora.
“Nimeridhishwa na Kitendo
cha Msajili wa Bodi hii kuwafutia leseni Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi
86, waliokiuka miiko ya utekelezaji wa taaluma hii, hivyo endeleeni kulisimamia
hili ili kuhakikisha taaluma hii haipati dosari”,amesisitiza Rais Mstaafu Mwinyi.
Aidha, Rais Mstaafu Mwinyi
amewataka watendaji na wataalam wa fani hiyo kupiga vita rushwa na ubadhirifu
ili kuhakikisha jamii inapata majengo yaliyo bora na ya kudumu kwa muda mrefu
na kuwataka wale watakaokiuka maadili ya taaluma hiyo wadhibitiwe kwa mujibu wa
sheria.
“Siku za hivi karibuni
tumekuwa tukishuhudia majengo mengi
yanaanguka nchini na hii inasababishwa na wataalam kutokufuatilia kikamilifu katika
maeneo yao ya kazi na kusababisha hasara na watu kupoteza maisha.
Katika hatua nyingine Rais
Mstaafu Mwinyi ameipongeza AQRB kwa kuandaa mashindano ya insha kwa shule za
Serikali kuhusu taaluma hiyo ambayo yatahamasisha wanafunzi kusoma masomo ya Science na kuongeza wataalam
hao nchini.
Kwa upande wake Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli ameipongeza Bodi hiyo kwa kazi nzuri za Ubunifu Majengo zinazofanywa na
wakandarasi nchini na kuwataka kushirikiana na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya
nchi ili kubuni majengo yaliyo bora na yatakayodumu kwa muda mrefu.
Waziri Magufuli amebainisha
kuwa zaidi ya kiasi cha shilingi milioni 150 zimetengwa ndani ya mwaka huu wa
fedha kwa ajili ya kusaidia wataalam wa fani hiyo wanaomaliza masomo yao.
Naye, Msajili wa Bodi
hiyo Bwana, Jehad A. Jehad amesema kuwa zaidi ya wataalam elfu moja (1000),
wamesajiliwa tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo mwaka 1998 na kuiomba Serikali
kuanzisha vitivo vya taaluma hiyo katika
vyuo vikuu mbalimbali nchini ili kukidhi haja ya wataalam elfu themanini na tano
(85,000) ifikapo mwaka 2025.
Mkutano huo wa siku
moja unaowakutanisha wadau mbalimbali wa ujenzi nchini una lengo la kajadili
‘sheria ya manunuzi namba 7 ya mwaka 2011 na athari zake katika mazingira ya
ujenzi.
No comments:
Post a Comment