Vyombo vya habari vyatakiwa kujenga maadili
Suleiman Msuya
RAI imetolewa kwa vyombo vya
habari, taasis mbalimbali, vikundi vya kijamii, wananchi na serikali
kushirikiana kwa pamoja katika kujenga jamii yenye maadili kuanzia ngazi
ya familia ili kuleta maendeleo katika nchi.
Hayo yamebainishwa na Afisa
kutoka IQ Management Solutions Joel Nanamka wa wakati akizungumza na
gazeti hili jana jiji Dar es Salaam.
Alisema iwapo kutakuwepo kwa
ushirikiano baina ya sekta hizo ni wazi kuwa jamii itazingatia maadili
katika suala lolote ambalo linafanyika kwa maslahi ya Taifa.
Nanamka alisema vyombo vya
habari kama moja ya muhimili usio rasmi bado havijafanya kazi ya dhati
ili kuweza kuibadilisha jamii ambayo inaonyesha dhahiri kupotea katika
misingi ya utu.
Afisa huyo alisema ukosefu wa
maadili hasa katika sekta mbalimbali za serikali kumekuwa kukichangia
ukosefu wa huduma bora na zenye viwango kwa jamii.
“Kimsingi suala la kuwepo
kwamaadili ni mtambuka ila kwa mtazamo wetu katika tafiti mbalimbali
tunaona kuwa nafasi ya vyombo vya habari katika kufanikisha hilo ni
kubwa hivyo vinapaswa kubadilika kutokana na ukweli kuwa watu wengi
wanafikiwa”, alisema.
Alisema IQ Management Solutions
imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali za kuhakikisha kuwa maadili
yanakuwepo kwa kanuni, sheria, zawadi na matisha pamoja na adhabu ambazo
zitakuwa katika mtazamo hasi.
Kwa upande wake Afisa Programu
kutoka taasisi ya Afrika Leadership Initiative Foundation Limited Alice
Mwiru alisema katika kuhakikisha kuwa kunakuwepo kwa jamii yenye maadili
taasisi yao imejikita kufanya kazi na vijana ambao wanaonyesha nia za
kuongoza.
Mwiru alisema wao wanaamini kuwa
kuwepo kwa viongozi wenye maadili ni chachu ya kuwepo kwa jamii ambayo
itakuwa katika misingi hiyo.
“Sisi ALI EAF tunaamini kuwa jamii
ikikuwa kwa misingi ya maadili hasa kuanzia utotoni ni wazi kuwa kila
Mtanzania atakuwa kwenye misingi hiyo kwa faida yake na nchi kwa
ujumla”, alisema
No comments:
Post a Comment