TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, December 20, 2014

BONDIA MAOKOLA AMDUNDA MKALAKALA KWA K,O YA RAUNDI YA 7 NA KUTETEA MKANDA WAKE

Mabondia Antony Peter kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hamidu Mussa wakati wa mpambano wao Mussa alishinda kwa point mpambano huo Picha na  SUPER D BOXING NEWES
 Mabondia Ibrahimu Maokola kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Selemani Mkalakala wakati wa kugombania ubingwa wa Taifa unaotambuliwa na chama cha TPBC Maokola alishinda kwa k,o ya raundi ya saba  Picha na  SUPER D BOXING NEWS
Bondia Selemani Mkalakala akiwa chini kwa konde zito alilotupiwa na Ibrahimu Maokola wakati wa mpasmbano wao wa ubingwa Picha na  SUPER D BOXING NEWES
IBRAHIMU MAOKOLA
 
Mgeni rasmi katika mpambano huo Joseph Vitalis kulia akimvisha mkanda wa ubingwa unaotambulika na chama cha TPBC bondia Ibrahimu Maokola baada ya kumdunda Seleman Mkalakala kwa k,o ya raundi ya 7 kushoto ni promota wa mpambano huo Shabani Adiosi Picha na  SUPER D BOXING NEWS

Serikali imejidhatiti katika kuboresha huduma za mawasilano kwa Njia ya Mtandao (TEHAMA)

unnamed
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wanne Kushoto) akifuatilia kwa umakini mazungumzo kwa njia ya mtandao na watu wa Kenya, alipotembelea ofisi ya Wakala wa Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLa), jijini Dar es Salaam.
unnamed1
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wanne Kushoto) akifuatilia kwa umakini mazungumzo kwa njia ya mtandao na watu wa Kenya, alipotembelea ofisi ya Wakala wa Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLa),leo jijini Dar es Salaam.
unnamed2
Wajumbe wa bodi ya Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao(TaGLa) wakifuatilia mazungunzo kwa njia ya mtandao na watu wa Kenya, Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLa),leo jijini Dar es Salaam
unnamed3
Menaja wa tecknolojia TaGLA ,Bwana Emmanuel Tessua wa kwanza kushoto, akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa pili kulia) ya namana mikutano inavyofanyika kwa kutumia mtandao katika chumba cha mikutano wakati wa Ziara yake leo jijini dare s Salaam , wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA Bwana Charles Senkondoleo jijini Dar es Salaam.
unnamed4
Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA Bwana Charles Senkondo akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika kituo cha taarifa za maendeleo(TDIC) alipotembelea ofisi hizo leo jijini Dar es Salaam.
unnamed5
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ( wa tatu kushoto) akiangalia namna majadiliano yanavyofanyika kwa mfumo wa kutumia mtandao katika ofisi za Wakala wa Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLa) wakati wa ziara yake leo jijini Dare s Salaam, wa kwanza kushoto ni Menaja wa tecknolojia TaGLA ,Bwana Emmanuel Tessua na wa pili ni Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA Bwana Charles Senkondo.
………………………………………………………………………………
Na Lorietha Laurence- MAELEZO

Serikali imejidhatiti katika kuboresha huduma za mawasilano kwa Njia ya Mtandao (TEHAMA) ili kurahisisha utendaji wa shughuli mbalimbali za kiserikali. Akiongea na wajumbe wa bodi ya Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema lengo la Serikali ni kuongeza ufanisi kwa watumishi na jamii kwa ujumla kujifunza na kuwasilisha mada mbalimbali kupitia mtandao. Balozi Sefua amesema kuwa serikali na taasisi zake mbalimbali hazina budi kutumia wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao kufanya shughuli zake zote zinazotekelezeka kwa njia ya Videoconference na Mafunzo ya Masafa ili kupunguza gharama. “Lengo kuu la Serikali ni kurahisisha mawasilino baina ya watumishi na jamii ili kupunguza usumbufu wa safari ndefu kutoka sehemu moja kwenda nyingine na pia kuokoa muda, na urahisi wa upatikanaji wa huduma kwa wananchi” alisema. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bwana Charles Sekondo, amesema ofisi yake imekuwa ikitekeleza majukumu kwa ufanisi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaojihusisha na mafunzo kwa njia ya mtandao ili kwenda sambamba na maendeleo ya teknolojia duniani katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kijamii na kiserikali. “Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao imerahisisha sana mawasiliano baina ya serikali, wizara, idara , wakala wa Serikali, pamoja na Sekta binafsi katika kuboresha uweledi kiutendaji kupitia utawala bora, anuai za jamii, maswala ya afya na mazingira” alisema Sekondo Katika Ziara hiyo Katibu Mkuu Kiongozi alitembelea maeneo mbalimbali ya ofisi ya Wakala wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao ikiwemo Sehumu ya Huduma za Video Conference, Chumba cha Maabara za Kompyuta na kituo cha taarifa za maendeleo (TDCI). Mtandao wa TaGLA,unajukumu la kuwajengea uwezo watumishi wa wizara, idara na wakala wa serikali pamoja na sekta binafsi katika nyanja mbalimbali ikiwemo , mafunzo ya midahalo kwa njia ya video ya hapa nchini na nchi nyingine, midahalo kwa njia ya mtandao, mafunzo ya ana kwa ana na mafunzo kwa njia ya uongozi.

MAAJABU YA KIFO CHA MAMA YAO AKINA MWAIBALE ALIFARIKI SIKU ILE ILE ALIYOZALIWA

Ankal Muhidin Issa Michuzi akimfariji Dotto Mwaibale wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Jijini Dar es salaam kabla ya kusafirishwa Mbeya kwa mazishi, wengine katika picha ni pamoja na Asha Kigundula, Anna Nkinda na Erick Shigongo anayeonekana kwa mbali
Mshereheshaji mashuhuri nchini Charles Mwakipesile akimfariji mfiwa Nicco Mwaibale mara baada ya kuwasili kijiji cha Newland Kiwira, Tukuyu kwa ajili ya mazishi.

Nicco Mwaibale akijifuta machozi huku akifarijiwa na kaka yake Kulwa Mwaibale mara baada ya kuwasili kijijini

Kulwa Mwaibale akimfariji shangazi yake kwa kumfuta machozi  mara baada ya kuwasili msibani hapo wakati wa mazishi

Kulwa (kulia) na Dotto Mwaibale wakati wa mazishi ya mama yao mpendwa
Vijana wa Skauti wakiusindikiza mwili wa Bibi Twitikege Mlagha katika nyumba yake ya milele.

Vijana wa Skauti wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Twitikege wakiusindikiza kwenye nyumba yake ya milele

Baadhi ya watoto na wajukuu wa Bibi Twitikege wakilia kwa uchungu wakati wa mazishi yaliyofanyika kijiji cha Newlanda Kiwira.

Jeneza lenye mwili wa marehemu Twitikege likishushwa kwenye nyumba yake ya milele

Baadhi ya watoto wa marehemu wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mama yao kipenzi

Umati wa waombolezaji waliohudhuria mazishi ya Bibi Twitikege katika kijiji cha Newland Kiwira Tukuyu wilayani Rungwe.
Na Rashid Mkwinda
 Asubuhi  ya Disemba 13, 1940 huko katika kijiji cha Katumba wilayani Rungwe, familia ya mzee Mafumu Mlagha ilikuwa katika  furaha kwa kumpata mtoto wa kike baada ya kiu ya muda mrefu ya kuwa na mtoto wa kike.
Ilikuwa ni siku ambayo familia hii ilibahatika kuwa na mtoto wa kike waliyempa jina la Twitikege.
 Anga la kijiji cha Katumba lenye jua lililowakia mandhari nzuri ya kijani kwenye kijiji kilichoshamiri kilimo cha Migomba na Chai binti wa kike
alizaliwa,Ndege wa angani na vipepeo wenye rangi nzuri walioruka kutoka mti mmoja kwenda mti mwingine ilikuwa ni sehemu ya kukamilisha furaha iliyoigubika familia hiyo na kijiji kwa ujumla.
 Twitikege aliliona jua kwa mara ya kwanza, familia ya Mzee Mafumu Tabulo Mlagha wa kijiji cha Katumba wilayani Rungwe walijipatia mtoto wa kike waliyempa jina la Twitikege,walijivunia kuwa na uwiano wa watoto wa jinsi mbili,  kutokana na kuwa na mtoto wa kiume katika zao la kwanza.
 Twitikege kama walivyo watoto wengine wa familia ya kabila la Kinyakyusa alikuzwa na kulelewa katika maadili yanayoshabihi  mila na desturi za wenyeji wa maeneo hayo.
 Aliishi na kulelewa katika familia ya ukoo wa kichifu, makuzi yake yalikuwa ni sawa na makuzi ya watoto wengine wa kiafrika waishiyo maeneo ya vijijini. Katika zama hizo neema ilitawala kutokana na ardhi ya kaya hizo kustawi kila aina ya chakula na hivyo kumfanya binti Twitikege akue katika neema.
 Maeneo mengi ya vijijini kwa zama hizo ardhi`ilikuwa na rutubna tele na hivyo kusheheni mazao ya kila aina na hivyo kufanya uzawa wa wakati huo kuwa na maisha yenye afya bora kutokana na wingi wa chakula kilichopatikana katika maeneo hayo.
 Kama ilivyo desturi na mila za kiafrika binti anapofikisha umri wa kuvunja ungo aliangaliwa na kutunzwa kwa kila hali ambapo Twitikege kulingana na makuzi ya kimaadili aliyokulia alipofikisha umri wa miaka 13 mwaka 1953 alichumbiwa na kijana wa kijiji jirani na nyumbani kwao cha Mpuga.
 Alikuwa ni  Anyitike Gwalamba Mwakwama Mwaibale ambaye kama walivyo vijana wengi wa wakati huo naye alitokea katika familia iliyostaarabika ya wazazi wachamungu walioishi kwa maadili kulingana na mila na desturi za maeneo hayo.
 Baada ya kufunga ndoa Twitikege na mumewe Anyitike alichukua dhamana ya kumlea Twitikege wakaishi vyema nao walirithi desturi njema ya wazazi wao,waliishi kwa wema na uadilifu na kuahidi kuishi kwa raha mustarehe katika kipindi chote cha Uhai wao.
 Matunda ya ndoa yao yalibarikiwa na hatimaye wakajaaliwa kupata watoto wake kwa waume ambao nao waliwalea na kuwasomesha kama walivyolelewa wao enzi za ujana wao.
 Kwa takribani miaka 50 ya ndoa yao  walifanikiwa kupata watoto 9 wa kike na kiume,watatu kati yao walitangulia mbele ya haki na kubaki watoto sita.
 Kama ilivyokuwa katika malezi yao katika familia zao Twitikege na Mwakwama waliwalea watoto wao kwa maadili na miongozo ya  dini bila kusahau  mila na desturi za Kinyakyusa ambazo ziliwafanya wamudu kuishi na watu tofauti na kabila tofauti.
 Mwaka 2007  ni siku ambayo Bimkubwa huyo Twitikege Mlagha  akiwa ametimiza jumla ya miaka 53 ya ndoa yake na mumewe alipata pigo ambalo kamwe hakuweza kulisahau katika maisha yake.
 Alimpoteza mumewe Mzee Anyitike Mwakwama Mwaibale ambaye alifariki na kumuachia ukiwa, ingawa alipata faraja kwa uwepo wa wajukuu na vitukuu lukuki waliotokana na watoto wake yeye na mumewe bali  pengo la kumpoteza mumewe kamwe halikuweza kuzibwa.
 Halikuzibwa pengo la mumewe ndani ya moyo wake, majonzi na fikra za kumpoteza mwenzi wake vilitawala katika fikra zake ingawa alipata faraja ya kutembelewa na wanawe waliokuwa wakiishi maeneo ya mbali na kijijini kwake.
Mara kadhaa niliwasikia wanawe wakihitaji kuomba ruhusa katika kazi zao ya kuja kumuona mama yao na kumpa faraja, ilikuwa ni katika jitihada za kumsahaulisha machungu aliyokuwa nayo ya kumpoteza mwenza wake aliyeishi naye tangu akiwa kijana hadi anazeeka.
 Alimkumbuka Anyitike, alikumbuka walivyokuwa vijana, alikumbuka siku ya kwanza kuchumbiwa na Anyitike, alikosa raha akajikuta akilia peke yake na kuongezeka majonzi ya kumkosa mumewe ambaye kadri walivyoishi walizoeana na hata kufikia hatua ya kuwa kama ndugu waliotokana na baba na mama mmoja.
 Ni takribani miaka saba tangu aondoke mumewe Anyitike, Twitikege kwa kipindi cha miaka miwili alianza kukumbwa na maradhi ya Uzee na hivyo kushindwa kujihudumia kwa shughuli alizozoea kujihudumia mwenyewe na kujikuta akilazimika kuomba msaada kutoka kwa wajukuu na wanawe walio karibu.
 Bimkubwa huyo aliendelea kuugua na kupata matibabu katika hospitali mbalimbali za ndani na nje ya mkoa wa Mbeya na hatimaye mwaka 2014 alichukuliwa na wanawe kuelekea Jijini Dar es salaam kwa ajili ya matibabu.
 Ijapokuwa alikuwa katika maradhi bali aliendelea kuwa faraja kwa wanawe kila walipomuona wakiwa pamoja wakizungumza naye hili na lile.
Kila mtoto alipenda kuwa karibu na mama yao ili apate baraka zake hata hivyo kutokana na maradhi aliyokuwa nayo hakumudu kukaa kwa watoto wote kwa wakati wote bali alianza kuzidiwa na homa na kulazimika kulazwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
 Kila nyumba ya wanaye alipoenda kuishi nyumba hiyo iligubikwa na furaha na Baraka,wajukuu na watoto wakitamani kuwa naye wakati wote wakifurahia uwepo wake katika familia hizo.
 Kulazwa kwake kuliacha simanzi kwa wajukuu na watoto wakikumbuka ucheshi wake na matarajio yao ya kumuombea walau arejee katikasiha njema ili arejeshe furaha na Baraka katika nyumba zao kama ilivyokuwa awali.
 Haikuwa bahati tena kwa vitukuu, wajukuu na watoto kumuona Bimkubwa huyu akiwa katika hali yake ya awali,Mwenyezi Mungu aliamua kumuita.
 Kama ilivyokuwa wakati wa kuzaliwa kwake,tarehe ileile aliyozaliwa ya Disemba 13 ndiyo hiyo hiyo Disemba 13, 2014  akiwa na jumla ya miaka 74  aliaga dunia usiku wa saa 5:00 Jijini Dar es salaam akiacha majonzi makuu na vilio kwa vitukuu, wajukuu na wanawe sita waliopo.
Marehemu aliagwa Jijini Dar es salaam na mwili wake kusafirishwa 
Mkoani Mbeya katika kijiji cha Newland kilichopo kata ya Kiwira wilayani Rungwe na kuzikwa Disemba 17,2014  katika makaburi yaliyopo katika mashamba ya familia mkabala na kaburi la mumewe kipenzi.
Apumzike kwa amani!!Aamen!!

KIKAO MAALUM CHA KAMATI KUU YA CHAMA CHA CHADEMA KILICHOKUTANA JB BELMONT JIJINI DAR

SERIKALI YAZINDUA RASMI USAMBAZAJI TAKWIMU ZA PATO LA TAIFA, PATO LA MWANACHI LAONGEZEKA.

unnamedWaziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum (katikati) akizindua rasmi   Takwimu za Pato la Taifa zilizorekebishwa kwa mwaka wa kizio wa 2007 leo jijini Dar es salaam. unnamed1 Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum (kulia)  akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servicius  Likwelile chapisho la lenye Takwimu za Pato la Taifa zilizorekebishwa kwa mwaka wa kizio wa 2007 wakati wa uzinduzi wa usambazaji wa takwimu hizo leo jijini Dar es salaam. unnamed2Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa(Kushoto) akitoa ufafanuzi wa kazi ya kurekebisha takwimu za Pato la Taifa iliyofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu iliyotumia tafiti za taifa zilizofanyika kwa kipindi cha mwaka 2001 hadi 2007.Kulia ni Waziri wa Fedha Mh. Saada Salum Mkuya. unnamed3Baadhi ya viongozi na wageni  waliohudhuria  uzinduzi wa usambazaji wa Takwimu za Pato la Taifa zilizorekebishwa kwa mwaka wa kizio wa 2007 wakimsikiliza Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa, Bw. Daniel Masolwa wakati akiwasilisha mada kuhusu Pato la Taifa leo jijini Dar es salaam.
……………………………………………………………………………………….
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
. Dar es salaam.
Serikali imesema kuwa Pato la Taifa kwa mwaka 2007 limeongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 26.8  ikilinganishwa na trilioni 20.9 za mwaka 2001, ambapo wastani wa pato la mwananchi mmoja mmoja limeongezeka kutoka shilingi milioni1,186,200/= mwaka 2001 hadi shilingi milioni 1, 561,050/= mwaka 2013. 
 Akizindua usambazaji wa takwimu hizo leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum ameeleza kuwa matokeo hayo  ni sawa na ongezeko la ukubwa wa Pato la Taifa kwa asilimia 27.8. 
Amesema ongezeko hilo ni matokeo ya juhudi za Serikali kuweka mazingira mazuri na kutengeneza  fursa za kuwawezesha wananchi kufanya kazi za kujiajiri na hatimaye kupata kipato halali kwa kazi wanazofanya.
Mh. Mkuya amesema kuwa kukua kwa uchumi wa Tanzania kumechangiwa na kujumuishwa kwa shughuli mbalimbali zikiwemo Sayansi na Teknolojia ambako kumetoa fursa kwa wananchi kujiongezea kipato hususan matumizi ya simu za kiganjani ambazo zimerahisisha mawasiliano na utafutaji wa masoko ya bidhaa ndani na nje ya nchi.
Amezitaja shughuli nyingine kuwa ni ukamilishaji wa miamala mbalimbali ya kibenki na mikopo ambazo zimekuzwa  na sekta ya mawasiliano , kuongeza ajira  na kupunguza muda wa kusubiri huduma za malipo katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha, amefafanua kuwa kuongezeka kwa thamani ya Pato la Taifa kunaiongezea Serikali uwezo kimapato kupitia kodi na kuiwezesha kugharamia ujenzi wa miundombinu na utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi.
“Serikali imeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya Binafsi ya mwaka 2012 unaonyesha asilimia 60 ya kaya zote nchini zinapata maji safi na salama hasa hususan maeneo ya mijini,zaidi ya asilimia 20 ya kaya zote nchini zinatumia nishati umeme haya ni mafanikio makubwa ya matokeo ya ukuaji wa uchumi nchini” Amesisitiza Mh. Mkuya.
Akizungumzia mchango wa Sekta Binafsi katika kukua kwa pato la taifa nchini amesema kuwa ajira zipatazo laki nne kati ya laki sita  katika sekta iliyo rasmi zimepatikana.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa  uzinduzi huo amesema  kuwa kazi ya kurekebisha takwimu za Pato la Taifa imetumia Tafiti za Taifa zilizofanyika kwa kipindi cha mwaka 2001 hadi 2007.
Amezitaja tafiti hizo kuwa ni pamoja na utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya wa mwaka 2007, Sensa ya Kilimo iliyofanyika mwaka 2008 na Takwimu nyingine za utawala kutoka katika Wizara na Idara za Serikali.
Aidha, amefafanua kuwa ukokotoaji wa takwimu hizo umefuata mfumo wa Umoja wa Mataifa wa kutayarisha takwimu za Pato la Taifa wa mwaka 1993 na 2008 kwa lengo la kuhakikisha kuwa takwimu hizo zinalinganishwa na takwimu nyingine duniani.

Rais kuzungumza na Wazee wa Dare s Salaam Jumatatu

indexRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete atazungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar Es Salaam, mchana wa Jumatatu, Desemba 22, 2014.
Wakati wa mazungumzo yake na Wazee hao, Rais Kikwete atazungumzia masuala mbali mbali ya kitaifa, yakiwemo yale ambayo yamekuwa yanasubiri maamuzi yake tokea alipokuwa anajiuguza kufuatia upasuaji aliofanyiwa mwezi uliopita, Novemba 2014.
Undani zaidi kuhusu mkutano huo kama vile mahali utakapofanyika, saa utakapofanyika na nani wataalikwa utatolewa na mamlaka zinazohusika na maandalizi ya mkutano huo.
Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu. Dar es Salaam. 19 Desemba, 2014

SIMBA YAVUNJA UONGOZI WA YANGA,NI KIPIGO CHA MTANI JEMBE,MANJI ATANGAZA UONGOZI MPYA

MWENYEKITI wa klabu ya Yanga Yusuph Manji ameitangaza Sekretarieti mpya ya Uongozi katika Klabu hiyo yenye Maskani Mtaa wa Jangwani Jijini Dar Es Salaam.
Sektretarieti hiyo ambayo itaongozwa na  Katibu Mkuu Dk Jonas B Tiboroha ambae atafanya kazi na Mkuu wa Idara ya habari na Mawasialiano bwana Jerry Cornel Muro,Bwana Omar Kaya yeye anakuwa Mkuu wa Idara ya masoko
Wengineo ni Bwana Frank Chacha anakuwa Mkuu wa Idara ya Sheria pamoja na bwana Charles Boniface ambae atakuwa Kocha Msaidizi
Akithibitisha Kuteuliwa kwa Viongozi hao wajuu Klabuni hapo mda  huu Jijini Dar Es Salaam wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari na  Mkuu wa Idara ya habari na Mawasialiano bwana jerry Cornel Muro pamoja na kutangaza Viongozi hao wapya alisema 
Wanachama,Mashabiki,Wapen  pamoja na wapenzi wa Klabu hiyo washirikiane na Viongozi hao wapya kuiletea maendeleo Klabu hiyo kubwa nchini.
Aidha,jery Murro alisema Mwenyekiti wa yanga anamshukuru sana Bwana aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo mbrazili MARCIO MAXIMO pamoja na msaidizi wake kwa ushirikiano wo waliouonyesha katika timu hiyo na kuwatakia heri katika maisha yao huko waendako.
Katika hatua nyingine amesema kuwa yanga imeamua kuongeza vijana katika uongozi  wake ili muda wa kustaafu ukifika yanga iyakuwa na waridhi bora watakaoendeleza mazuri waliyoyakuta..

MAAFISA WA POLISI WATAKIWA KUTUMISHA NIDHAM

indexNa Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi.
Maafisa, Wakaguzi,  na Askari wa Jeshi la Polisi hapa nchini, wametakiwa kudunisha nidhamu wakati wote, kutenda haki kwa kila mmoja na kuwaheshimu wananchi wa rika zote bila ya kujali dini, rangi ama itikadi zao kisiasa.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Chuo cha Polisi Dar es Salaam, SACP Ali Lugendo, wakati akizungumza na Wanafunzi wa Mafunzo ya Uofisa (Mrakibu Msaidiizi wa Polisi) na wale wa cheti na Stashahadi ya Sayansi ya Polisi kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.
Kamanda Lugendo amesema kuwa pamoja na kufundisha masomo ya sheria na haki za binadamu, lakini kazi kubwa inayofanywa na chuo chake ni kusisitiza nidhamu kwa kila afisa na askari wanaofika chuoni hapo.
Amesema kuwa nidhamu ni somo la kwanza analofundishwa askari anapokuwa katika mafunzo ya awali kwenye chuo cha Polisi Moshi kwani amesema nidhamu ni msingi wa kwanza kwa majeshi yote duniani.
“Hakuna Jeshi lolote duniani, likiwemo Jeshi letu la Polisi hapa nchini ambalo haliendeshi kwa misingi ya nidhamu”. Alisema Kamanda Lugendo na kuongeza kuwa bila nidhamu hakuna Jjeshi.
Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Nidhamu kwenye chuo cha Polisi Dar es Salaam (Dar es Salaam Police Academy) SSP Mussa Loyd, aliwataka Maafisa hao kuwa kioo cha jamii na kuwatendea haki wananchi  bila ya upendeleo wakati wote wanapokuwa kazini katika maeneo mbalimbali.
Alisema kuwa, mbali ya kuzuia vitendo vya kuhalifu, kushuku, kupeleleza na kuwakamata watuhumiwa, lakini kazi kubwa ya Jeshi la Polisi ni kuhakikisha kuwa kila Askari anatenda haki kwa kila anayemhudumia bila ya ubaguzi ama kumuonea mmoja wao.
“tunachotakiwa kufanya sisi Polisi ni kutenda haki kwa kila mmoja bila ya kujali dini, kabila, rangi ama itikadi ya mwananchi kisiyasa maana sisi hatuna chama”. Alisema Loyd.

Jokate asaini mkataba wa thamani ya Sh8.5 bilioni na kampuni ya Kichina

unnamed
Jokate Mwegelo akizungumza katika hafla hiyo
  unnamed3
Jokate na Guoxun wakibadilishana mikataba baada ya kusaini
unnamed2
Jokate na Guoxun wakionyesha mikataba baada ya kusaini
unnamed1
   Afisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya Rainbow Shell Craft Company Limited  (CEO), Deng Guoxun akuzungumza katika hafla hiyo
unnamed5
Wageni mbalimbali waalikwa wakishughudia hafla hiyo
unnamed4
Jokate akiteta jambo na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa kwenye hafla hiyo
…………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Mbunifu mavazi, Miss Tanzania wa namba mbili 2006,  mwanamuziki na muigizaji wa filamu, Jokate Mwegelo amesaini makubaliano yenye thamani ya Sh8.5 billion na kampuni ya Kichina,  Rainbow Shell Craft Company Limited kwa ajili ya kuzalisha na kuuza bidhaa mbalimbali za lebo yake ya Kidoti.
Makubaliano hayo yalisainiwa jana kwenye hotel ya  Serena baina ya Jokate na Afisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya Rainbow Shell Craft Company Limited  (CEO), Deng Guoxun.
Akizungumza katika hafla hiyo,  Jokate alisema kuwa makubaliano hayo ni ya kudumu na kampuni hizo mbili zitazalisha na kuuza bidhaa za kidoti Tanzania nzima na nje ya mipaka yake.
Alifafanua kuwa kampuni ya China itawekeza Tanzania na kuwafaidisha watanzania kwa kutoa nafasi ya ajira. Alisema kuwa pia wanatarajia kujenga kiwanda ili kuinua uchumi wa nchi na maisha ya watanzania.
 “Hii ni hatua kubwa ya maendeleo kwangu, kama unavyojua, wakati naanza kujishugulisha na masuala ya urembo, ubunifu na uanamitindo, sikutegemea kufikia hatua hii ya kuingiza bidhaa zangu kimataifa, lakini sasa, ndoto zangu zimetimia na najivunia mafanikio haya,” alisema Jokate.
Alisema kuwa mbali ya kutoa mitindo tofauti ya kisasa ya nguo, kampuni yake pia itazalisha aina mbali mbali za viatu, nywele ikiwa pamoja na  mawigi,  weaving, Rasta na viatu vya wazi (sandals) ambazo kwa sasa zipo tayari kwenye soko la Tanzania.
“Mpango wangu ni kupanua soko la bidhaa zangu kama Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Afrika Kusini na nchi nyingine za Afrika,” alisema.
Afisa Mtendaji wa Guoxun alisema kuwa wamefurahi kukamilisha ubia na kampuni ya Kidoti na haya ni matunda ya ushirikiano wa kudumu baina ya serikali yao na Tanzania.
 “Tumefurahi sana kukamilisha makubaliano haya, tunatarajia kuongoza katika soko la hapa nchini na wenzetu (wachina) watafaidika pia, ” alisema Guoxun.

KIWANDA CHA SUKARI KAGERA CHAZALISHA ZAIDI

SONY DSCMeneja wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Bw. Ashwin Rana akiwakaribisha wageni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipotembelea kiwanda hicho ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo nchini. Anayesalimiana naye ni Prof. Longinus Rutasitara (Naibu Katibu Mtendaji Uchumi Jumla). Katikati ni Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri. SONY DSCTimu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikikagua mitambo ya kuzalishia sukari katika Kiwanda cha Sukari cha KageraSONY DSCKiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Mwenye kofia ya bluu) akionja sukari inayozalishwa na Kiwanda cha Sukari cha Kagera. Kushoto ni Mratibu wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Senya Tuni. SONY DSCTimu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera. Nyuma ni shehena ya sukari iliyo tayari kuingia sokoni. SONY DSCTimu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakioneshwa mashine ya kumwagilia maji miwa ijulikanayo kwa kitaalamu kama Centre Pivot System. SONY DSCMeneja wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Bw. Ashwin Rana (Kulia) akiwaonesha Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mashine mpya zinazotumika kuvutia maji kwa ajili ya kumwagilia miwa.
SONY DSCMsimamizi Mkuu wa Mtambo wa maji wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Mhandisi Abdul Adinani (Kulia) akitoa maelekezo ya namna ya maji yanavyochujwa kabla ya kutumika kwa ajili ya umwagiliaji wa miwa. Wanaomsikiliza ni Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. SONY DSCMtaalamu wa uchongaji na usawazishaji wa ardhi kwa ajili ya mashamba ya miwa, Mhandisi Ali Khamis (Kulia) akitoa maelezo ya namna matrekta yanayotumia setalaiti (hayapo pichani) yanavyofanya kazi. Wanaomskiliza ni Prof. Longinus Rutasitara (Kushoto) ambaye ni Naibu Katibu Mtendaji anayeshughilikia masuala ya Uchumi Jumla na  Katikati ni Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri. SONY DSCTimu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakioneshwa kwa vitendo matrekta yanayotumia setalaiti kusawazisha shamba kwa ajili ya uzalishaji miwa.
(Picha Zote Na: Said Mkabakuli)

……………………………………………………………………………….
Na:Saidi Mkabakuli, Kagera

Kiwanja cha Sukari cha Kagera kimeanza kuzalisha ziada ya sukari inayohitajika katika soko la sukari nchini hali inayopelekea kuweza kupunguza tatizo la upatikanaji wa sukari Tanzania na nchi za jirani zinazotumia sukari kutoka kiwandani hapo.
Hayo yamewekwa wazi na Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho, Bw. Ashwin Rana, wakati alipokuwa akizungumza na Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
“Kwa sasa tumeweza kuongeza mauzo katika kanda kufikia tani 40,000, pamoja na kuongeza ununuzi kutoka kwa wakulima wa miwa wa nje zaidi ya tani 100,000 kwa mwaka,” alisema.
Bw. Rana  aliongeza kuwa Kiwanda chake kimewekeza zaidi katika upanuzi wa eneo la shamba la miwa la umwagiliaji la hekta 3600 pamoja na kuwekeza zaidi katika teknolojia ya kisasa katika kilimo.
“Kampuni yetu imewekeza kwa kiasi kikubwa katika teknolojia na vifaa vya kisasa ikiwemo matrekta yanayotumia setalaiti katika ufanyaji kazi wake katika kuandaa mashamba,” aliongeza.
Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri amekipongeza Kiwanda hicho kwa  kuwekeza kwenye uzalishaji wa kisasa wa miwa hali inayoongeza uzalishaji wa sukari kuwa mkubwa kiwandani hapo.
Bibi Mwanri ameongeza kuwa Kiwanda hicho kinastahili pongezi za kipekee kwa kuweza kuongeza ajira zaidi ya watu 6000 waliopo kiwandani.
“Kwa kweli munastahili sifa kwa kutoa ajira kwa vijana wa Kitanzania pamoja na kuuza umeme kwenye gridi ya Taifa,” alisema.
Kwa mujibu wa Meneja wa Kiwanda hicho, kwa sasa kinakabiliwa na na changamoto za uuzaji haramu wa sukari zinazoingia kimagendo nchini ambao umechangiwa kushindwa kwa kiwanda kuuza sukari ili kurudisha gharama za uzalishaji kutokana bei za sukari zinazoagiwa kutoka nje kuwa bei ya chini sana.
“Bei ya Sukari Duniani imeshuka sana kutokana na Nchi kubwa duniani kusaidia wakulima katika uzalishaji na pembejeo (subsidies) na hivyo sukari kuuzwa katika soko la dunia kwa bei ya chini (Dumping) na kufanya kuwa bei kuwa ndogo kuliko gharama halisi ya uzalishaji,” aliongeza.
Aliongeza kuwa changamoto nyingine ni pamoja na kiwanda kushindwa kulipa mikopo iliyochokuwa benki kutokana na kuwepo sokoni kwa sukari ambayo ni ya magendo na bei ya chini hivyo kiwanda kushindwa kufikia malengo hata ya kiundeshaji na mipango mikakati.
Kiwanda cha Sukari cha Kagera kiko katika sehemu Kaskazini Magharibi ya Tanzania (karibu na mpaka wa Tanzania na Uganda) kilibinafsishwa na Serikali kwa sekta binafsi mwaka 2001. Malengo ya ubinafsishaji yalikuwa kuboresha upanuzi wa masoko ya ndani na kikanda, uwekezaji wa kisasa, upanuzi na ukarabati na majengo ili kuhakikisha shughuli za kiundeshaji zinaboreshwa.